Huu ni mpira wa kishamba sana

The Boss

JF-Expert Member
Aug 18, 2009
49,110
115,899
Kuna wakati inabidi tuachane na ushabiki wa wa hizi timu za kariakoo na kukosoa bila ushabiki

Kinachoendelea ni ushamba Na hakipaswi kabisa kushabikiwa.

Simba kujaribu kumchukua Morrison ni ushamba sana.

Yanga kumchukua CEO wa Simba ushamba pia sana, sana.

Hii vita ya kukomoana ushamba mtupu, haisaidii lolote kwenye mpira, sana sana linavunja moyo.

Wachezaji ambao ni decent na loyal kwa timu wanaona kumbe kuhamahama hizi timu ndo unapata hela unayotaka.

Tukemee huu ushamba.
 
Mpira wetu hauendelei kwa kuwa na viongozi wenye mitizamo ya kishamba na Karba za Ukurupu kurupu.

Mpira unaendeshwa kisayansi ngazi zote hadi usajili unafanyika kwa weledi mkubwa siyo kumaliza udhia na timu fulani kwa kumsajili mchezaji wa timu hiyo aliyekufunga hata kama hakuna hitaji lake au ilikuwa bahati tu akakufunga.

Tukiendelea kuwa na viongozi KURUPU KURUPU kama Manara hatutafika popote katika ngazi za kimataifa.

Huu ni muda wa kuwa na viongozi makini kwenye soka letu ili twende kwenye soka la kisasa viongozi wabovu na wasio na weledi wa kuendesha soka tuwaondoe bila kuwaangalia usoni.
 
Mi naamini hii yote inasababishwa na shirikisho hivi kuna nini ambacho kimrichelewesha hii kesi mpaka kifikia hatua hii na hii inaonyesha shilikisho halina maamuzi kwa wanachama wake
 
Mpira wetu hauendelei kwa kuwa na viongozi wenye mitizamo ya kishamba na Karba za Ukurupu kurupu.

Mpira unaendeshwa kisayansi ngazi zote hadi usajili unafanyika kwa weledi mkubwa siyo kumaliza udhia na timu fulani kwa kumsajili mchezaji wa timu hiyo aliyekufunga hata kama hakuna hitaji lake au ilikuwa bahati tu akakufunga.

Tukiendelea kuwa na viongozi KURUPU KURUPU kama Manara hatutafika popote katika ngazi za kimataifa.

Huu ni muda wa kuwa na viongozi makini kwenye soka letu ili twende kwenye soka la kisasa viongozi wabovu na wasio na weledi wa kuendesha soka tuwaondoe bila kuwaangalia usoni.
ukweli mkuu na watu wahuni wasiyokuwa na weledi wa soka kama kina Hans ndiyo wanaovuruga mpira kwa kuringia pesa na umaarufu wao.

Sasa leo wanalamika Yanga walifoji mkataba, wanasahau kuwa kuna audio Morrison alikuwa analamika kuwa amesain mkataba yanga ila boss wa simba kampa $10,000 za kumrubun! Na kama ndivyo Morrison mkataba wake umefojiwa, kulikuwa hakuna haja ya kwenda TFF sababu hiyo ni criminal case, Morrison angeishitaki yanga mahakaman na hukumu ya mahakama ndiyo ingeamua hatma ya mkataba wake.
 
Kuna wakati inabidi tuachane na ushabiki wa wa hizi timu za kariakoo na kukosoa bila ushabiki

Kinachoendelea ni ushamba Na hakipaswi kabisa kushabikiwa.

Simba kujaribu kumchukua Morrison ni ushamba sana.

Yanga kumchukua CEO wa Simba ushamba pia sana, sana.

Hii vita ya kukomoana ushamba mtupu, haisaidii lolote kwenye mpira, sana sana linavunja moyo.

Wachezaji ambao ni decent na loyal kwa timu wanaona kumbe kuhamahama hizi timu ndo unapata hela unayotaka.

Tukemee huu ushamba.
Unaweza kuwa na wazo kumbe kuna mwenzio Mji mwingine ana wazo Kama lako.
Huu ni ujinga ndo maana ushabiki wa Simba na Yanga niliacha 1994.
 
Mwakyembe kama waziri mwenye dhamana ya michezo hapa nchini amekaa kimya tuu, huku tim 2 'kubwa' na zenye washabiki wengi zaidi hapa nchini zikikomoana na kukomeshana, hiii si sawa hatakidogo, mwakyembe na wizara yake wanatakiwa kutoa 'neno' otherwise hii ni hujuma kwa maendeleo ya mpira, na kwa style hii maendeleo ya mpira wetu yanazidi kurudi nyuma……...wizara ya kazi nayo ipo wapi, futa hizo 'work permit' za senzo na huyo mvuta bange, wanapoelekea watahatarisha Amani nchi….over!
 
Mwakyembe kama waziri mwenye dhamana ya michezo hapa nchini amekaa kimya tuu, huku tim 2 'kubwa' na zenye washabiki wengi zaidi hapa nchini zikikomoana na kukomeshana, hiii si sawa hatakidogo, mwakyembe na wizara yake wanatakiwa kutoa 'neno' otherwise hii ni hujuma kwa maendeleo ya mpira
Mwenyewe anafurahi sababu ana beef na TFF....."adui muombee njaa".
 
Kuna wakati inabidi tuachane na ushabiki wa wa hizi timu za kariakoo na kukosoa bila ushabiki. Kinachoendelea ni ushamba Na hakipaswi kabisa kushabikiwa. Simba kujaribu kumchukua Morrison ni ushamba sana. Yanga kumchukua CEO wa Simba ushamba pia sana, sana. Hii vita ya kukomoana ushamba mtupu, haisaidii lolote kwenye mpira, sana sana linavunja moyo. Wachezaji ambao ni decent na loyal kwa timu wanaona kumbe kuhamahama hizi timu ndo unapata hela unayotaka. Tukemee huu ushamba.
Sidhani kama ni ushamba. Mchezaji mpya kusajiliwa ni kawaida, popote pale atakapotoka. Meneja, kocha au Mtendaji mpya kuajiriwa ni jambo la kawaida pia, bila kujali anapotoka.
 
Hans Pope,Manara na Magori ni kirusi cha Soka la Bongo,na pia sioni usomi na credibility ya MO katika hili amekubali kuendeshwa kama gari bovu na hao Waswahili.
Suala la Morrison inaweza kuwa chanzo cha anguko la Mo.

Mzee wa kususa hatakawia kufanya uamuzi mgumu. Kuwaachia timu yao akina Hans Poppe na Kaburu. Tusubiri. Muda utasema kama Mo ni mwekezaji au mfadhili aliyechangamka.
 
Ni kweli kama tutaweka ushabiki wetu na kukemea haya mambo vilabu vitaacha huu ujinga kwa wote tuliofatilia ligi Morison hakuwa hitaji la Simba ni kama usajili wa Ajibu sasa hivi anasugua benchi
Sijakataa. Mimi ni mshabiki wa mpira kwa timu zetu. Na napenda sana mafanikio ya Simba na Yanga na Azam na timu zote maana zinasaidia kukuza mpira wetu na kujenga timu ya Taifa. Ila upuuzi wa Simba na Yanga unaua mpira wetu na kuua timu ya Taifa. Maana wachezaji wote wazuri wanachukuliwa kutoka timu zao na baadaye wanawekwa benchi kipaji kinaisha huku tukitegemea maproo. Hapo tunajenga timu ya Taifa au tunaiua? Mfano ni Metacha, Gadiel Michael, Ndemla, Adam Salamba, Ally Ally, miongoni mwa wengine ambao ni tegemeo kwa timu ya Taifa. Cha ziada, Simba wasipokaa vizuri na Manara wataua mpira wa Bongo. Yuko tayari aue kipaji cha mchezaji kwasababu ya ligi ya kumtoa Yanga akakae benchi Simba.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom