Che Mkira
Senior Member
- Jul 8, 2014
- 117
- 152
NENO LA SHUKURANI
JE UNAIKUMBUKA HII?
"....ndoto yangu ilikuwa ni kupata elimu ya chuo kikuu lakini naona sitaweza kuipata tena kaka kwasababu familia yangu haina uwezo wa kunisomesha. Nilisoma kwa bidii nikafanikiwa kupata division 'one' na kuchagua kusoma uwalimu ili nipate mkopo lakini nimekosa mkopo. Kaka naishi maisha ya taabu ambayo siwezi kuyaelezea. Hapa Dar sina ndugu hata mmoja. Kwa ufupi nateseka sana toka nilipotoka nyumbani Tabora kuja chuo kikuu cha Dar es salaam"
Hayo ni maneno ya mwanafunzi aliyechaguliwa chuo kikuu cha DSM anayeitwa AGNES LEONARD KASANSA mwenye namba ya usajili 2016-04-00782, BAED.
Binti huyu amenifuata akiwa analia sana. Anaomba nimsaidie ili aendelee na masomo yake kwakuwa mpaaka sasa hajasajiliwa na wala hajalipa pesa ya makazi(hostel). Anasema hata chakula kwake ni taabu sana kupata. Kwakweli nimejisikia vibaya sana ikizingatiwa alisoma shule ya serikali inayoitwa Kishoju Muleba mkoani Kagera.
........….....…...................
Ni utamaduni wa wale waliostaarabika kusema ASANTE pale maombi yao yanapofanyiwa kazi. Kwa mara nyingine tena, nakuja mbele yenu kuwashukuru wote mliomsaidia Agnes kurejesha matumaini yake ya kitaaluma.
Alipoteza matumaini ya kuendelea na masomo yake na hata siku amenifuata hakuniomba nimsaidie ada kwasababu pengine alihisi nisingeweza kumsaidia, badala yake alisema kwa upole "kaka nisaidie tu nauli nirudi nyumbani Tabora"
Niliumia sana na kwa jeuri ya kikurya nikamwambia "Sitakusadia hata cent moja ya nauli, isipokuwa nitahakikisha unaendelea na masomo yako"
Kupitia Agnes nimejifunza kuwa, kuna wakati mtu anaweza kutoa asichokuwa nacho. Niliwashirikisha marafiki zangu mbalimbali kupitia mitandao ya kijamii, na hatimaye wakaguswa kumsaidia.
Tunashukuru sana kwa wote mliomtumia fedha kupitia namba yake ya simu ambayo tuliambatanisha kwenye ujumbe wa maombi.
Lakini kipekee sana na pengine kupunguza urefu wa andiko hili, ningependa kuwashukuru wafuatao;
1) Alberto Msando
Kwasababu niliwahi kumuona akiwa amemuunganisha mmoja wa wanafunzi wa UDSM na rafiki zake kwajili ya kumsadia, niliona niwasiliane naye kwajili ya kuona namna tunaweza kumsaidia Agnes. Alionesha kuguswa sana. Nashukuru kwamba alituunganisha na rafiki yake anayeitwa Andrew na rafiki wengine ambao wote kwa pamoja walimsadia Agnes kiasi cha 1,070,000.
Pia tunamshukuru kwa kuhimiza Rafiki zake kumsaidia Agnes kupitia ukurasa wake wa Instagram.
2)Mhe Elibariki Kingu mbunge wa Singida Magaribi.
Huyu kiongozi alijitoa kumsaidia Agnes katika masomo mpaka atakapomaliza. Tunamshukuru sana kwa moyo wake wa kujali.
3)Stitching Talent Development Tanzania.
Tunamshukuru sana ndugu Samson Nyahiri ambaye ni kiongozi wa shirika hilo, kutuunganisha na STDT na wao kuahidi kumsaidia Agnes mpaka atakapomaliza masomo yake.
4) Women Supporting Women.
Hawa kina mama walimchangia 500,000
5) Eng Paul Ndege & Angel
Walimchangia 300,000
6) Rukia Hussein
Walimchangia 300,000
7) Mwita Julius Gabriel
Julius ambaye pia ni katibu wa BAVICHA alimchangia 100,000
8) Suzan Simon
Alimchangia 30,000 na kuahidi kufanya hivyo kila mwezi.
9) Matiku wa Japan
Alimchangia 100,000
10) Rayson Shoo
Alichanga 100,000
11) Dr Mgisha
Alimchangia 500,000
12) Arene
Alimletea nguo.
13) David Lema
Alimsaidia hostel(makazi) mpaka atakapomaliza chuo.
14) Waliojitoa kutafuta watu wa kumsaidia Agnes kwa njia ya kusambaza ujumbe na kuwasiliana na watu wenye uwezo wa kumsaidia.
Wako wengi sana. Lakini hawa ni sehemu yao. Malisa GJ Josephat Keraryo Nyambeya, Frey Cosseny, Kwinyara Kwintara Kwinyara, Tz Classic, Justin Gitano Nyirabu, Manoah William, Celina Donald Chacha, Upendo Moses etc.
15) Tanzania Students Networking Program (TSNP) kwa pamoja tumeshirikiana sana katika kila hatua.
16) Athuman Hamis Juma
Huyu ndiye kijana aliyekuwa anaenda na Agnes kila mahali alipoitwa kwajili ya msaada. Hii ilikuwa ni kuhakikisha kunakuwepo na usalama lakini pia kusaidai kupunguza vishawishi. Mchango wake ni mkubwa sana.
Mwisho
Agnes ni kielelezo cha tatizo kubwa linalowakumba wanafunzi wengi kiasi cha kuamua kukatisha masomo yao. Wapo vijana wengi sana wanaoshindwa kutimiza ndoto zao. TSNP peke yake tuna jumala ya wanafunzi 19 ambao wanahitaji msaada. Tunatoa wito kwa taasisi mbali mbali kujitokeza kuwasaidia wanafunzi hao na wengine ambao hawana uwezo. Hata wale ambao mlionesha nia ya kumsadia kama Joketi Mogelo, bado misaada yenu inahitajika sana. Kuhusu serikali, tayari TSNP tumeandika waraka kuishauri wizara husika namna bora ya kupunguza au kundokana kabisa na tatizo hili ambalo ni kinyume kabisa na ahadi ya Rais John Magufuli kwa wanafunzi wa vyuo vikuu.
Bob Chacha Wangwe
TSNP