Huu ndo urafiki feki?

Bin Shaib

JF-Expert Member
Aug 1, 2019
1,315
1,186
Ndugu wana jukwaa ningependa kuwashiirikisha hili na ninahitaji ushauri wenu nahisi itanisaidia sana .
Nina rafiki yangu natamani kumuepuka kimya kimya kutokana na tabia zake ambazo naona ni rafiki ambaye si rafiki anayeweza kuniongoza hata kunako mafanikio.

KISA CHA KULETA UZI HAPA
Nina jamaa yangu ambae tumekuwa marafiki sasa yapata kama miaka 2 hapa jijini Mwanza ambaye tumekuwa tukisaidiana ishu za hapa na pale kama marafiki.

Amekuwa akiniomba ushauri kuhusu mahusiano nami bila kinyongo huwa namshauri nakupata suruhu, japo nami nimepitia kuimizwa kunako mahusiano kipitia kuumizwa nimeshapata ujuzi kidogo ambao unaweza kumjenga mtu.

Nikiwa kwenye kumshauri kuhusu mapenzi atatega sikio kwa makini lakini kuhusu mambo yangu huwa haweki umakini kabisa.

Nikimwambia nataka kufanya hiki atanipinga na kuniambia huwezi, nikisema mimi ni fundi wa hiki anasema huwezi, tukiwa tunapiga story nikaleta maada ambayo yeye hajawahi kuisikia au jambo lolote atabisha sana na kuniita muongo mbele ya wadau.

Nikisema nataka ninunue hiki anaonesha kama kutofurahia halafu cha kushangaza yeye ndo anaenda kununua kile kitu yaani anatumia mawazo yangu kufanya mambo yake,

Lakini yeye huwezi kusikia hata siku moja anakushauri jambo lolote la msingi, ni mbishi sana na hapendi kukosolewa, ukimukosoa anakasirika munakwaruzana, anapenda akukosoe yeye halafu ukitaniwa hata na demu atacheka na wewe unaamua kukausha tu.


Na hapo ni kiufupi tu ni mambo mengi sana,

Je, ni rafiki wa kweli?
Au nimuepuke?
Au njia zipi nitumie kutengana nae?

Japo sahizi nimeshapunguza mawasiliano nae kama zamani.

©Bin Shaib Classic 2020

Kuwa makini Corona bado ipo.
 
MWANAUME HATAKIWI KUMLALAMIKIA MWANAUME MWENZIE ETI "RAFIKI"...
Sema ni mshikaji au Mwana tu...

Hujafungwa wala kulazimishwa kumshirikisha mambo yako... Hukutakiwi hata kulajamika... It seems bado mtoto wewe. .. Hujakua bado...

Kwani ni lazima kumshirikisha. .. Wapi imeandikwa kuwa ni LAZIMA?

ACHA HUO UTOTO... Hayo mambo wanafanyaga wanawake kwa Mashoga zao. ..

Fanya mambo yako KIUME. .. ACHA KULALAMIKIA WANAUME WENZIO KWENYE PLATFORM ZA WATU WAZIMA KAMA HIZI...
 
MWANAUME HATAKIWI KUMLALAMIKIA MWANAUME MWENZIE ETI "RAFIKI"...
Sema ni mshikaji au Mwana tu...

Hujafungwa wala kulazimishwa kumshirikisha mambo yako... Hukutakiwi hata kulajamika... It seems bado mtoto wewe. .. Hujakua bado...

Kwani ni lazima kumshirikisha. .. Wapi imeandikwa kuwa ni LAZIMA?

ACHA HUO UTOTO... Hayo mambo wanafanyaga wanawake kwa Mashoga zao. ..

Fanya mambo yako KIUME. .. ACHA KULALAMIKIA WANAUME WENZIO KWENYE PLATFORM ZA WATU WAZIMA KAMA HIZI...

Powa mkuu sahizi sitoweza kumushirikisha lolote
 
Mkuu, unatakiwa ujue maana ya urafiki ndiposa utajua kama na yeye ni mmojawapo ama vinginevyo.
 
Sio lazima yeye akusaidie.

Yeye kaona wewe una akili au mawazo kuliko yeye. Sasa ukimwomba wewe akujibu nini

Anasema tu hiiiiiiii
😂😂😂
 
Back
Top Bottom