huu ndio Usta wa Ma Rap wa Kibongo? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

huu ndio Usta wa Ma Rap wa Kibongo?

Discussion in 'Jamii Photos' started by MziziMkavu, Dec 24, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Dec 24, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,605
  Trophy Points: 280
  Undumilakuwili wa Afande Sele waanikwa

  Undumilakuwili wa Afande Sele waanikwa
  Msanii Suleiman Msindi ‘Afande Sele’, ameanikwa kwa tabia yake ya undumilakuwili.
  [​IMG]

  Picha za video, zinazomuonesha Afande akiwatukana Clouds FM, zimeanikwa mtandaoni kuthibitisha jinsi msanii huyo alivyo ndumilakuwili.
  Hivi karibuni, Afande alisaliti harakati za wasanii wanaopambana katika mradi wa Anti Virus na kwenda kuimba kwenye tamasha la Clouds, jambo ambalo limewaudhi wadau wengi.
  Katika video hiyo, Afande anatoa matusi makali kuwa Clouds wanataka kumuua kimuziki, akasema kwamba badala ya kusikiliza Clouds watu wasikilize Magic FM.
  Katika mashambulizi hayo, Afande aliponda pia kuwa watangazaji wengine wa Clouds walikuwa watoto wakati yeye anakuwa Mfalme wa Rhymes mwaka 2004, hivyo akasisitiza hawambabaishi.
  Hata hivyo, juzikati Afande alitosa tamasha la Vinega, Ustawi wa Jamii na kwenda kwenye shoo ya Clouds aliokuwa anawatukana kwamba wanamuua kimuziki.
  Mbali na kwenda kwenye shoo, Afande aliponda tamasha la Vinega lakini mwisho wa mchezo, Vinega waliibuka kidedea kwa kukusanya nyomi la hatari.


  Hii ndio Bangi kwa wingi ? au ndio show ya muzik ya kibongo?
   
 2. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #2
  Dec 24, 2011
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,401
  Trophy Points: 280
  Mgambo sele bangi tu hizo zinamzingua,muulizeni ncha butu kawakimbia vinega
   
Loading...