Huu ndio uongozi wa Mh. Freeman Mbowe CHADEMA

Huu ndio uongozi wa Mh. Freeman Mbowe CHADEMA

God'sBeliever

JF-Expert Member
Joined
Sep 1, 2015
Posts
5,788
Reaction score
3,062
Watu wengi wamezungumzia sana swala la ukabila na ufisadi ndani ya chadema.
Walioelimika wameelewa na wale watu wazima wanajua historia ya chadema hadi hapa ilipo.

Tatizo linatokea kwa vijana na vibaraka wasiopenda taifa letu. Hawajali wanawapa malkana watu waaina gani bali wao wanafata upepo tuu bila kutafakari.
Pia watu wazima wenye chuki wamekua wakiponda vilivyo CCM ili chadema iingie madarakani lakini Mungu atawalinda watanzania tuu.

Ni kweli nchi ilikiua katika kipindi kigumu mno katika uongozi wa Mh Kikwete ila kuna mazuri yake aliyafanya jamani pamoja na upinzani wote stil Mh Rais aliongozana nao kwenye mambo mengi ya kitaifa ikiwemo michakato ya maendeleo, demokrasia kuwafariji walio kwenye msiba hata misiba ya wapinzani pia aliweza kuleta umoja na ndilo ninalomsifu huyu mkuu na alirudisha JKT ili watu wajifunze uzalendo.
Alikua kakomaa kisiasa pamoja na hali ya nchi haikua nzuri ila bado alipigana kuwaridhisha watanzania.

Mimi nilikua upande waupinzani ila baada ya kuona chokochoko na ubabe wa mbowe nikakimbia na kwa mtizamo wangu ni bora CCM wabaki madarakani maiaka 1000 kuliko hawa wakabila ambao watakuja kuigawa nchi kidini na kikabila na hatimaye tuanze kuuana kama nchi jirani za rwanda na burundi.

Kiongozi kama huyu (Mbowe) keshaonyesha tabia chafu kiasi hiki akikabidhiwa nchi sindo tutaangamia kabisa?

Watanzania nawaomba muwe na busara na msiwe watu wa kukurupuka hata kama mna hasira na mtambue kwamba mimi natokea kaskazini na nimeshaona kabisa huyu Mbowe ni jipu ataigawa nchi akiendelea na ukabila wake.

Kama kaanza kuwamaliza wenzake ndani ya chadema wewe unadhani atajali raia?

Leo hii wako wapi wakina slaa, zitto kabwe na mkumbo? Mimi naona hawa walitengenezewa mazingira tuu ya uongo ili waonekane wachafu kumbe sio.

Na katika uchunguzi wangu huu nimeona chanzo cha haya machafuko ndani ya chama ni kuhusu nafasi ya mwenyekiti wa chadema! ikumbukwe chacha wange na zitto kabwe waliwahi ongelea sana hili jambo na watanzania wengi waliwaelewa ila wale wajinga wakaona eti wanataka madaraka ya juu japokua kuna waliowakuta humo?

Sasa ni demokrasia gani hiyo ya ulafi? kama mwenyekiti umeshindwa kuonyesha mfano wewe ni mtu kweli?

Naomba watanzania wenye nia njema na taifa letu mtoe elimu tujue hawa watu wanaodai madaraka kabla ya kuwapigia kura. Waheshimiwa huku tupeni busara zenu hapa maana mimi kama kijana niliefumbuliwa macho ni sharti langu kuwafumbua na wengine waliopotea.

Wale watakao tukana hapa na kukejeli hatutajali sisi nia yetu ni kupeana elimu juu ya mfumo mzima wa kisiasa ili tuwe aware na political issues na watu wenyewe wanaohusika.


Leo hii yule fisadi mkubwa waliekuwa wanamsema sasa hivi ni malaika eti??
Ila tuaweza kuona wabunge wengi wa chadema wanakubali tuu sababu ya ubabe wa mbowe wanajua akipinga kitakachowakuta ni umauti.

Pitieni hii video hapa ili mjifunze kitu kuhusu huyu mlafi wa madaraka toka 1995 hadi leo anapigana tuu muone alivyo na uchu. Mungu amlaze mahala pema peponi Baba wa taifa hili hayati J K Nyerere kwa busara zake na maono yake ya mbali.

Leo hii toka 1995 alichobashiri ndicho kinachowakumba watanzania ila Kwa neema zake Mwenyezi-Mungu watanzania walio wengi walikuelewa na hawajampigia kura huyu mtu na Mzee huko mbinguni tambua alisha hama CCM saivi yupo chadema na alishindwa uchaguzi na ufisadi aliuendeleza hadi alipojiuzulu uwaziri mkuu 2007.



Leo hii mshirika wako wa karibu (Slaa) umemtema wewe ni mtu kweli?

Naomba moderators wasittoe huu uzi jamani wala ku merge kwenye mada nyingine hata kama hili jambo lishazungumzwa sio ubaya kulitafakari tena.
Natanguliza shukrani kwenu.

MUNGU IBARIKI TANZANIA, MUNGU WABARIKI WANANCHI WAKE DAIMA TUPENDANE NA TUDUMISHE UMOJA WETU NA WALE WENYE NIA MBAYA NA TAIFA LETU WASHINDWE WALEGEE KWA JINA LAKO.

NAWASILISHA.
 
Mkuu,Mbona Kikwete alimtema mshirika wake Lowasa lkn husemi hilo isipokuwa Mbowe kumtema Slaa unaona haaminiki?!!...so unataka kutuambia kuwa hata JK haaminiki kwa sababu alimtema EL?
 
Hawa Chadema tangu walipomteua mgombea wao wa urais na kuaanza kumsafisha na tuhuma za ufisadi ambazo mwanzo walimtuhumu nazo sina hamu nao tena na ingetokea wangeshinda urais nchi ingeingia katika ufisadi na rushwa ya hatari.
 
Wapiga Ramli naona mahirizi yanabana mnaweweseka..mtu mwenye akili timamu hawezi uliza Zito,Mkumbo,Slaa wapo wapi kisiasa hata aliyetolewa macho na mtu anayemtuhumu kuwa ni Scorpion atakwambia walipo hao Mayuda ambao hawakusubiri mpaka Jogoo awike bali mnuso wa hela,uchu,tamaa,na kujiona kuwa wao ndo ma alwatani uliwatoa kwenye Chama Chao pendwa.
  1. Ni kiwete pekee wa ubongo ndo ana uwezo wa kurudi CCM lakini nafsi ikiwa inamsuta kuwa huku nimefata madaraka na ulaji bali si kuwatumikia wananchi na kuwaelimisha yaliyo mema.
  2. Vijana wengi wamerithi mikoba bado wakiwa wadogo kwa kuitumikia ccm sababu inawafunza kuwa wakatili,wasiwe na huruma,wawe na uchu wa madaraka,wawe wezi/wapokea rushwa,wasiwe wazalendo na wasithamini kabisa nembo yao ya Jembe na nyundo,ila wauenzi wimbo usemao"ccm ni ile ile.."
  3. Mwalimu nyerere hakuwafunza ccm wawe wezi na wasitumie jina lake kujisafisha na kukisafisha Chama cha Mapinduzi.
  4. Hata JPM mnayemnadi ni mrithi wa Nyerere kama atafufuka hata kesho atamkana kabla Jogoo halijawika..
 
Hapa tulipofika nikwasababu ya Mbowe na Chadema? Ukiona mpaka leo watu bado wanawaza Mbowe na Chadema fahamu kuna mambo huko waliko hayako sawa sasa wanajaribu kujilinganisha na wengine ili kujitetea au kuona wako sawa.
 
Daah RIP CHACHA WANGWE
Mkuu damu ya mtu haipotei hivi hivi malipo ni hapa duniai tuu.
Unafiki utazidi kujidhihirisha tuu, et wanasema wanapinga rushwa wakati mkuu wao ni jizi la kufa mtu na linawakandamiza vibaya mno.

Matendo husema.
 
Kwani Slaa aliondolewa Chadema na Mbowe au alijondoa mwenyewe Chadema kwa kujiuzuru Ilatibu Mkuu (Same as Lipumba?) Acha siasa za kijinga jinga we Dada!

Tena kibaya zaidi Slaa aliacha Jeshi likiwa kwenye mapambano karibu kabisa na kumshinda adui. Ila kwa tamaa zake za Mali na ulafi akaamua kukimbia jeshi lake na kuwa msaliti kwa kulishambulia jeshi lake lililomfikisha hapo alipokuwa..... Na akitegemea lianguke.

Mungu ni mwema na Chadema itendelea kuwepo hata wajukuu wako wataikuta ikiwa Imara zaidi.

Muache Slaa apumzike kwa amani mahali pema uko alipo!

Nonsense.
 
Kwani Slaa aliondolewa Chadema na Mbowe au alijondoa mwenyewe Chadema kwa kujiuzuru Ilatibu Mkuu (Same as Lipumba?) Acha siasa za kijinga jinga we Dada!

Tena kibaya zaidi Slaa aliacha Jeshi likiwa kwenye mapambano karibu kabisa na kumshinda adui. Ila kwa tamaa zake za Mali na ulafi akaamua kukimbia jeshi lake na kuwa msaliti kwa kulishambulia jeshi lake lililomfikisha hapo alipokuwa..... Na akitegemea lianguke.

Mungu ni mwema na Chadema itendelea kuwepo hata wajukuu wako wataikuta ikiwa Imara zaidi.

Muache Slaa apumzike kwa amani mahali pema uko alipo!

Nonsense.
Yeye ndio shujaa wa kweli huwezi kumdharau mtu na kumuita mwizi leo hii uje umpokee na umpe mamlaka kwenye himaya yako huo ni ujinga uliotukuka.
 
Mbowe hafai kabisa, ona nchi uchumi umesinyaa kama ng'ombe aliyeugua sotoka. Maelfu ya watoto wa masikini watashindwa kusoma elimu ya juu kwa kukosa mikopo kwa sababu ya huyu Mbowe wa Chadema. Kiongozi gani huyu hatufai.
Watoto wanakosa chanjo za kinga kwa Mara ya kwanza toka Uhuru sababu ya Mbowe hampendi Slaa, Zitto na Kitila, hata dawa za watu wazima nazo hakuna ngoja mvua zije na kipindupindu kichukue nafasi watu watakufa utadhani vita kuu ya pili ya dunia maana Mbowe anaweza kusema kwani Chadema ndio inaambukiza kipindupindu? Mbowe kwa nini lakini hutaki kujiuzulu pamoja na kusababisha yote haya?
Vijana hawana ajira wala chama chako hakiwaambii mpango wa kujiajiri ukoje. Sisi kule katika chama chetu tunaaminishwa kuwa wewe Mbowe ukiondoka katika hicho cheo chako nchi itaendelea kwa kasi ya ajabu sana.
Jee baba utaondoka lini ili tununue ndege zingine kwa cash maana fedha tunazo
 
Kweli nimeamini vijana wa Lumumba hawana hoja kwanini kila siku kuhangaika na Mbowe na Lowasa? Hivi hatuwezi kujadili namna yakuiendeleza nchi Mbowe na Lowasa wana-effect gani kwa ccm hawako madarakani Why mbowe always time?
 
Mkuu damu ya mtu haipotei hivi hivi malipo ni hapa duniai tuu.
Unafiki utazidi kujidhihirisha tuu, et wanasema wanapinga rushwa wakati mkuu wao ni jizi la kufa mtu na linawakandamiza vibaya mno.

Matendo husema.

Mwizi (jizi) mahali pake ni wapi eti?

Au wewe ndiye Jizi mkubwa sasa unajihami kuita wenzio majizi with no subsatantial evidences??

Acha kujihami bwana kwa kutumia watu wengine kama cover ya "ujizi" wako huko kwenye Chama Cha Majipu a.k.a CCM!!
 
Kuiamini Chadema kwa sasa haihitaji kutumia akili wala MAARIFA bali kichwa kikubwa, PUA, masikio na mdomo wewe tayari unakuwa Chadema fuluu.

Said by M2020.

Utatetea ujinga na upumbavu. By Ben Mkapa.

Chadema ni Chama dhaifu ambacho kikipewa nchi kitavuruga msingi ya UMOJA wa taifa letu. Bila ccm imara nchi yetu itayumba. Naendelea kuaminiwa ccm it aendelee kutawala miaka 100 zaidi. By Mwl NYERERE
.
 
Ukweli uliopo wazi ni kuwa CCM kimechoka na hakina tena uwezo wa kuivusha nchi yetu kutoka hapa ilipo kwani ni miaka mingi ilikuwa nafasi ya kufanya hivyo lakini badala yake wakaturudisha nyuma baada ya kusonga mbele........

Haiwezekani nchii hii kwenye miaka zaidi ya 50 ya uhuru tushindwe kutatua tatizo la maji kwa wananchi tena wengine wapo kama kilometer tano tu kutoka vyanzo vya maji.....

Haiwezekani mpaka sasa tuwe tunahangaikia madawati ya wanafunzi na nyumba za walimu wakati wenzetu wanaangalia uwezekano wa kuwapatia laptop wanafunzi kama nyenzo ya kujisomea......

Yapo mengi yanayoonyesha kuwa CCM kimeshindwa kukidhi haja na kiu za Watanzania......

Lakini pamoja na yote hayo bado watawaliwa tuna mashaka na aina ya upinzani tulionao....ambao tungependa kuwa mbadala wa CCM......

Kwa kweli wapinzani wanatakiwa wabadilike ili sisi wapiga kura tuelewe na tuone kuwa ndio mbadala wa CCM kwa matendo na mifano.......
 
Ukweli uliopo wazi ni kuwa CCM kimechoka na hakina tena uwezo wa kuivusha nchi yetu kutoka hapa ilipo kwani ni miaka mingi ilikuwa nafasi ya kufanya hivyo lakini badala yake wakaturudisha nyuma baada ya kusonga mbele........

Haiwezekani nchii hii kwenye miaka zaidi ya 50 ya uhuru tushindwe kutatua tatizo la maji kwa wananchi tena wengine wapo kama kilometer tano tu kutoka vyanzo vya maji.....

Haiwezekani mpaka sasa tuwe tunahangaikia madawati ya wanafunzi na nyumba za walimu wakati wenzetu wanaangalia uwezekano wa kuwapatia laptop wanafunzi kama nyenzo ya kujisomea......

Yapo mengi yanayoonyesha kuwa CCM kimeshindwa kukidhi haja na kiu za Watanzania......

Lakini pamoja na yote hayo bado watawaliwa tuna mashaka na aina ya upinzani tulionao....ambao tungependa kuwa mbadala wa CCM......

Kwa kweli wapinzani wanatakiwa wabadilike ili sisi wapiga kura tuelewe na tuone kuwa ndio mbadala wa CCM kwa matendo na mifano.......
Shukrani mkuu natumai kwa busara zako wanao, nduku zako na marafiki zako wa karibu wanafaidika kwa hekima zako.
Mungu akubariki zaidi.
 
Magamba utawajua tu, mpunga hawana wanatafuta pa kutokea mara wanakuja kwa staili ya kuhakiki kila kitu alafu sasa walivyo kuwa kama mashetani wanataka watokee kwenye fedha za misaada ya tetemeko,
Vipi huyu shetani wenu anaeleta ukabila? tumuache aje aigawe nchi na kusababisha ukabila???
Wote washenzi tuu pamoja na Jipumba kwa kueneza udini utao kuja kugawa taifa letu.

Umeshindwa kuwa kiongozi mzuri wa familia yako, chama chako je taifa utaweza??
Shindwa na mlegee kwa jina la Yesu.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom