Huu ndio ukomavu wa kisiasa si chuki kwa mtu binafsi

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,890
6,898

Katika hatua nyingine inayoashiria kuzidi kuungwa mkono kwa CHADEMA na viongozi wake, jana Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe alikuwa kivutio katika sherehe ya Siku ya Sheria nchini iliyofanyika katika viwanja vya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ambayo rais Jakaya Kikwete alikuwa mgeni rasmi.
Mbowe alikuwa kivutio wakati akiinuka kwenye kiti alichokaa kuelekea kwenye ngazi za Mahakama Kuu kupiga picha na viongozi mbalimbali wa serikali na mahakama ambao ni watumishi wa mahakama, mawakili na wananchi mbalimbali waliohudhuria sherehe hiyo. Watumishi wa mahakama pamoja na wananchi hao walisikika wakimshangilia kwa sauti ya juu “Mbowe Mbowe, Mbowe” na kiongozi huyo kulazimika kuwapungia mkono na kutabasamu.

Source, Tanzania daima newspapers
 
Tanzania tunahitaji viongozi wakomavu kisiasa na wala si chuki kwa mtu binafsi. Tofauti za itikadi za kisiasa isiwe ndio mwenendo wa kuchukia mtu binafsi.
Mheshimiwa mbowe nampongeza kwa dhamira nzuri aliyofanya kuhudhuria tukio lile la mhimili mmojawapo wa taifa letu, na hakuishia hapo akajitosa kusalimiana na viongozi mbalimbali waliopo akiwemo Rais Kikwete kama picha inavyoonyesha. Huu ni mfano mzuri wa kuigwa na wanasiasa na inaleta picha nzuri ya mahusiano ya viongozi kwa kuonyesha utanzania. Tukiwa katika uringo wa siasa ni hoja za siasa, na tunapokuwa katika matukio ya kitaifa siasa tunaweka kando na kushiriki mambo muhimu ya taifa letu.
 
Mambo yaleyale lakini angalia kichwa cha habari kinasemaje ndo maudhui ya habari. Nimejifunza jambo zuri sana hapa ambalo ni mfano zuri wa viongozi wenye upeo katika mambo ya umma kutokuwa wabinafsi bali kujali utaifa
 
Mkuu sikatai wala si kwamba ni mbaya isipokuwa nimeshauri tu kwakuwa picha hii hii imeletwa kama thread asububi hii na maudhui ni kama haya so ndo maana nikaomba ziunganishwe. Otherwise ni nzuri!
 
Yaliyotokea Pemba miaka ile viongozi wa CUF na CCM na serikali walikuwa wanakwepana na kupeana mikono ilikuwa hadharani haikuonekana, lakini Chadema wameanza onyesha hali tofauti na matarajio ya wengi yalivyokuwa.
Chadema wametangaza kwamba sasa ni wakati wa kuwawakilisha wananchi na kusaidia kujenga taifa ndo tunayotaka
 
Katika hatua nyingine inayoashiria kuzidi kuungwa mkono kwa CHADEMA na viongozi wake, jana Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe alikuwa kivutio katika sherehe ya Siku ya Sheria nchini iliyofanyika katika viwanja vya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ambayo rais Jakaya Kikwete alikuwa mgeni rasmi.
Mbowe alikuwa kivutio wakati akiinuka kwenye kiti alichokaa kuelekea kwenye ngazi za Mahakama Kuu kupiga picha na viongozi mbalimbali wa serikali na mahakama ambao ni watumishi wa mahakama, mawakili na wananchi mbalimbali waliohudhuria sherehe hiyo. Watumishi wa mahakama pamoja na wananchi hao walisikika wakimshangilia kwa sauti ya juu “Mbowe Mbowe, Mbowe” na kiongozi huyo kulazimika kuwapungia mkono na kutabasamu.

Source, Tanzania daima newspapers

Sipati picha kama Zitto ama Shibuda angechukua nafasi ya Mbowe ktk picha hiyo.
 
Hivo JK afya yake vipi? Naona kama kachoka vile. Au umri nn?
 
Ukipenda chongo huita kengeza. Kama ni zito huyo aliepeana mkono na kikwete angetukanwa na wanachadema lkn ni mchaga mwenzao haya. Langu jicho.
 
Ukimwangalia vizuri kikwete alivyosimama na anavyomwangalia Mr. Mbowe, ni kama haamini kama amekutana na Mwenyekiti wa Chadema kweli.
Kikwete anaweza kuwa na fikra mpya kuhusu Chadema
 
Wanamapinduzi si visasi, tujifunze aliyofanyiwa mzee Madiba Nerson Mandela. Ustahimilivu ndio ukomavu upendo hushinda kama isemavyo upendo una nguvu kama mauti
 
Mwaka 2005 wakati wa kutangaza matokeo ya rais - diamond jubilee.
Angalieni kina nani hawakuhudhuria kisha mlinganishe na wanachokisema leo
 
Attachments

  • Kikwete_nec_2005.jpg
    Kikwete_nec_2005.jpg
    82.5 KB · Views: 36

Katika hatua nyingine inayoashiria kuzidi kuungwa mkono kwa CHADEMA na viongozi wake, jana Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe alikuwa kivutio katika sherehe ya Siku ya Sheria nchini iliyofanyika katika viwanja vya Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ambayo rais Jakaya Kikwete alikuwa mgeni rasmi.
Mbowe alikuwa kivutio wakati akiinuka kwenye kiti alichokaa kuelekea kwenye ngazi za Mahakama Kuu kupiga picha na viongozi mbalimbali wa serikali na mahakama ambao ni watumishi wa mahakama, mawakili na wananchi mbalimbali waliohudhuria sherehe hiyo. Watumishi wa mahakama pamoja na wananchi hao walisikika wakimshangilia kwa sauti ya juu “Mbowe Mbowe, Mbowe” na kiongozi huyo kulazimika kuwapungia mkono na kutabasamu.

Source, Tanzania daima newspapers

Chamelionism and hypocricy.
 
Mwaka 2005 wakati wa kutangaza matokeo ya rais - diamond jubilee.
Angalieni kina nani hawakuhudhuria kisha mlinganishe na wanachokisema leo
kafu ni wanafiki na wana very short memories, kama mende
 
Napinga kwamba huu ni ukomavu wa kisiasa... UKOMAVU WA KISIASA SIYO KUCHEKACHEKA, BALI NI KUTEKELEZA AHADI KWA RAIA WAKO NA KUKUBALI KUSHAURIKA, NA KUJIREKEBISHA... BILA KUSAHAU KUKOSOLEWA
 
Ukomavu wa kisiasa si chuki kwa mtu ila hoja za msingi katika haki na ukweli.
Bill Clinton na George Bush walienda kucheza mpira pamoja siku za mapumziko ya weekend baada ya bush kushika madara ya nchi ya Marekani. Huo ndio mfano wa kuigwa kwani jukwaa la siasa halitufanyi tuwe maadui wenyewe kwa wenyewe bali tunatofautiana katika itikadi.
Mume na mke ndani ya nyumba wanaweza wakatofautiana kiitikadi lakini hawachukiani.
 
Napinga kwamba huu ni ukomavu wa kisiasa... UKOMAVU WA KISIASA SIYO KUCHEKACHEKA, BALI NI KUTEKELEZA AHADI KWA RAIA WAKO NA KUKUBALI KUSHAURIKA, NA KUJIREKEBISHA... BILA KUSAHAU KUKOSOLEWA

Kwamba ukomavu wa kisisa siyo kuchekacheka maana yake ni kukasirikiana? Hapo sikubaliani na hoja yako kwa maana kwamba nisipokubaliana na hoja yako basi nikukasirikie?
Tunapinga utaratibu mbaya, sera mbaya, sheria mbaya, lakini hatuwachukii watu.
 
Back
Top Bottom