Donyongijape
JF-Expert Member
- May 28, 2010
- 1,497
- 811
Nimekuwa nikifuatilia kwa makini taarifa za habari zinazotolewa na vyombo vyetu vya habari has kipindi hiki cha kampeni,televisheni,radio na magazeti.Pia Nimekuwa msomaji mzuri wa magazeti ya kila siku na yale yanayotoa habari kwa mtindo wa makala ( i mean kila wiki).
Kwa mawazo yangu,naona waadishi wa habari ndio wenye uwezo mkubwa wa kuweza kupotosha au kujenga jamii yetu kutokana na umuhimu wao katika kuhabarisha jamii.
Tatizo kubwa ninaloliona kwa waandishi wa habari na hata waahariri wao ni kutofanya Upembuzi yakinifu juu ya habari wanazozitoa,kwa lugha nyingine kutoa habari kwa USHABIKI. Kimsingi hili ndilo tatizo ni kubwa sana hasa kwa magazeti yetu haya ya kila siku.
Wanachofanya ni kutoa HABARI KAMA ILIVYOSEMWA BILA KUFANYA CRITICAL ANALYSIS NA KULETA KITU KILICHOKAMILIKA at the very first delivery kwa wananchi na MATATIZO yake wanakuja kuleta critics at a time habari ikiwa imeshaumiza jamii.
Nitatoa mifano michache ya karibuni:
> Tamko la majeshi:baada ya jeshi kutoa tamko lao,vyombo vingi vya habari vilitoa raw information kutoka kwa vyombo hivyo bila kuwa na chembe ya critical analsyis juu ya uhalali wa jeshi kufanya hivyo..kwa mawazo yangu waandishi wa habari zile walipaswa kufuata maoni ya wadau mbali mbali kisheria na katiba inasemaje,tume ya uchaguzi na wananchi kwa ujumla n.k kuona wao wanasemaje kabla ya kutoa habari zao. Wengi ambao hawaingii JF au hawakusoma na kusikia habari juu ya majeshi tangu siku ya Ijumaa watakuwa bado wana maswali mengi (ninaamini wapo wengi) na wengine bado wanaogopa hayo matamko.
> Tamko la Masheikh: Sijui kama hawa waliulizwa maswali na waandishi au walipotoa tamko waandishi wakaenda kuandika moja kwa moja bila kuhoji..Kimsingi Sheikh aliposema kwamba kuna viongozi wa dini wanataka watu wachague viongozi wa dini zao na ilkhali waandishi wote walikuwa informed kwamba hakukuwa na kiongozi wa dini aliyewahi kusema mchagueni fulani kwa sababu ni dini yetu,nilitegemea waandishi,ambao wao ndio wapata habari ya mwanzo kuhoji juu ya uhalali wa tamko hilo wakati hakuna kitu kama hicho..Kilichotokea kesho yake na jioni ile..WAISLAMU WAKEMEA VIONGOZI WA DINI WANAOLETA UDINI...Hakuna hata critical analysis hata moja,eti mpaka baadaye muanze kuandika kwenye makala juu ya mapungufu ya habari ile..Why not the very first day?.
> Kuhusu REDET: Although habari haijatoka kwenye TV na magazeti kesho,lakini kubwa linalotarajiwa,REDET wasema JK kapata hizi,fulani kapata hizi...Magazeti mengi yataandika juu ya namna REDET walivyosema..Hakuna hata moja (Labda km litakuwepo) litakalotoa kutoa analysis ya ripoti ya REDET hata kama inaonekana ina upotoshaji ndani yake..Kimsingi kuna maswali mengi ndani ya ripot hiyo kama Je Peter Mziray wa APPT kwa nini hakujumuishwa,au kwa nini CCJ ijumuishwe wakati walishafutwa kabla hata ya Uchaguzi..na mengineyo mengi tu amabayo yatawafanya wananchi kupata picha halisi ya ripot yenyewe..!
Mwisho: Mimi nadhani Muda huu hasa reporting ya matukio makubwa kitaifa kama haya ya uchaguzi, waandishi (Hasa wale makini ambao hawajanunuliwa) hawapaswi kuandika habari kama walivyoipata..Ni muhimu kabla ya kuitoa waulize maswali ya msingi juu ya habari husika kwa mhusika lakini pia watafute maoni ya wananchi..Kwa Mfano, waweza andika kichwa cha Habari; REDET WATOA MATOKEO YAO; Lakini ukafanya utafiti wewe binafsi kabla ya kuchapicha habari hiyo na kusema,WANANCHI WAIKUBALI/WAIPINGA kutokana na sababu A,BA,CHE etc.Lakini kutoa tu habari alafu usubirie kesho yake ndio uandike critics kwa mtindo wa makala ambao wengi hawasomi..Umekwisha,unakuwa mwandishi uchwara..Jifunzeni CNN,Raisi/Mkuu wa jeshi etc anatoa tamko au habari inatoka hapo hapo wanaleta matukio yanayoendana na hilo au wanahoji wananchi na kupata pia maoni yao mapema kabisa. Kinachofuata ni habari kamili iliyojaa