Huu ndio muda maalum wa kutoa risiti za EFD!

Freyzem

JF-Expert Member
Jun 29, 2013
8,540
2,000
Wanajamvi, hivi wafanyabiashara wana muda maalum wa kutoa risiti za efd?
Wenye biashara na wazoefu, pia hata mamlaka husika inaweza kutusaidia kwenye hili!
Jambo lililonifanya nihoji hili ni kwamba nimekwenda dukani karikoo, mida ya saa 12:40 hivi jioni na kutaka kununua bidhaa flani!
Baada ya kuikagua hiyo bidhaa na kuridhika nayo nilianza mchakato wa kuilipia lakini nikamuhoji muuzaji pia kama anaweza kunipa risiti ya efd!
Ghafla yule muuzaji akanijibu kwa hasira kuwa ameshafunga mahesabu na kamwe hawezi kutoa mashine kwa ajili ya mtu mmoja tu na kwamba bidhaa niliyotaka kununua basi nisiinunue tena niiache!
Sasa je ni kwamba kweli kuna muda maalum wa kutoa hizo risiti?
Hii ishu imekaaje...
 
Inna

JF-Expert Member
Jan 13, 2017
11,073
2,000
Atakua hana huyo alitumia defence mechanism kukwambia uache bidhaa
 
Mtetezi.com

JF-Expert Member
Oct 6, 2016
3,006
2,000
Ww unahitaji bidhaa au unahitaji receipt?
Fata kilichokupeleka hujui unavyong'ang'ania hivyo unazidi kukaza vyuma vya watu.?
 
Kumekucha2012

Member
Dec 2, 2017
97
125
Wanajamvi, hivi wafanyabiashara wana muda maalum wa kutoa risiti za efd?
Wenye biashara na wazoefu, pia hata mamlaka husika inaweza kutusaidia kwenye hili!
Jambo lililonifanya nihoji hili ni kwamba nimekwenda dukani karikoo, mida ya saa 12:40 hivi jioni na kutaka kununua bidhaa flani!
Baada ya kuikagua hiyo bidhaa na kuridhika nayo nilianza mchakato wa kuilipia lakini nikamuhoji muuzaji pia kama anaweza kunipa risiti ya efd!
Ghafla yule muuzaji akanijibu kwa hasira kuwa ameshafunga mahesabu na kamwe hawezi kutoa mashine kwa ajili ya mtu mmoja tu na kwamba bidhaa niliyotaka kununua basi nisiinunue tena niiache!
Sasa je ni kwamba kweli kuna muda maalum wa kutoa hizo risiti?
Hii ishu imekaaje...
Kuwa mzalendo na uwariport watu kama hao. ndio wanao rudisha maendeleo ya nchi nyuma na kama sikosei huyo atakuwa ni muhindi.
 
ankol

JF-Expert Member
Aug 21, 2012
1,332
2,000
Ni kweli akishatoa daily report hatakiwi ku punch tena kwa siku hiyo paka kesho yake. Yupo sahihi tu mdau. Ila sio kesi si ulienda ukanunua kwingine?
 
RRONDO

JF-Expert Member
Jan 3, 2010
41,619
2,000
Ni kweli akishatoa daily report hatakiwi ku punch tena kwa siku hiyo paka kesho yake. Yupo sahihi tu mdau. Ila sio kesi si ulienda ukanunua kwingine?
Hakutakiwa auze basi. Anatakiwa atume hio ripoti akiwa anafunga.
 
Freyzem

JF-Expert Member
Jun 29, 2013
8,540
2,000
Ni kweli akishatoa daily report hatakiwi ku punch tena kwa siku hiyo paka kesho yake. Yupo sahihi tu mdau. Ila sio kesi si ulienda ukanunua kwingine?
Basi angenielekeza taratibu au angeniambia ameshafunga muda wa kuuza umeisha...
Na siyo kufura na kunikasirikia kwa frastuesheni zake...
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom