dustless
JF-Expert Member
- Oct 21, 2016
- 796
- 714
Habari wakuu
Kwa mujibu wa pita pita yangu ya hapa na pale, nimejiridhisha pasina shaka yoyote kuwa zaidi ya robo tatu ya wanaume walioko kwenye ndoa wamewachoka wake zao.
Hivyo basi, wanaume hao wanatamani kabisa kabisa ndoa zao zivunjike hata leo wabaki huru ama wakaishi na wanawake wengine.
Tatizo linalowakwamisha kuvunja hizo ndoa zao ni uoga wa sheria. Kwa maana wanawake wengi kama si wote hutishia kwenda kwenye vyombo vya sheria ili kulinda ndoa zao.
Hivyo basi ndoa nyingi zimeshikiliwa na sheria na wala sio mapenzi ya moyoni na zingine ni huruma za watoto kwa waliofanikiwa kupata watoto.
Iko hivi, kwa kawaida wanaume wengi hutumia nguvu nyingi za ushawishi kumpata mwanamke ambaye hajadate nae tu na nguvu hizo hizo na pengine zaidi huhamia kwa mwanamke kumlinda na kumdhibiti mwanaume asimwache pindi wawapo kwenye ndoa.
Hii yote ni kwa sababu mwanaume hakuumbiwa kuwa na mwanamke mmoja, siku ni mtu wa kutamani bidhaa mpya zaidi na kuiacha ya zamani ikiendelea kubaki kabatini mpaka siku ya siku kuu.
Kibaya zaidi sheria hizi hizi za ndoa ambazo mwanaume anaziogopa zimetungwa na wanaume wenyewe ili kuwafeva wanawake na mwisho wa siku zinawagharimu tena wanaume hao hao watunzi.
Pamoja na hayo, wenye maamuzi magumu tu ndo hawafungwi na kitanzi hicho cha sheria. Huishi kwa kufarahisha zaidi mioyo yao kuliko kuridhisha watu wanaowazunguka. Wahenga wanasema, raha jipe mwenyewe.
Na hitimisha kwa kusema mapenzi ya mwanaume yana expire kwa muda mfupi sana wakati wanawake wana penzi endelevu, pengine ndio maana baadhi yao huchukuwa muda mrefu sana kabla ya kumruhusu mwanaume kuuperuzi mwili wake maana anajua akimweka moyoni ndo mazima until sun set.
Wanawake msikimbilie ndoa kwa wanaume ambao hawana utayari, mara hoo ukitaka kunipata twende nyumbani, shauri zenu. Kuna wanaume hawaogopi gharama, atafanya utakacho mwisho wa siku umekolea kwenye ndoa mwenzio anaendelea kusearch mitandao mengine kufurahia vifurushi vipya.
Sent using Jamii Forums mobile app