Huu nao ni udhaifu kwa wanawake wengi

Mshinga

JF-Expert Member
Feb 5, 2013
3,532
1,124
Wanawake wengi wanaweza kuwa na msimamo wa kumkataa mtu ama msimamo wa kutunza penzi la mpezi wake ama msimamo wa kutunza ndoa yake na kutofanya udanganyifu wowote.

Lakini wengi wanapopata matatizo hasa ya kifedha hugeuka na kuwa walaini na kuifutilia mbali misimamo yote waliyoiamini na kuishikilia huu ni udhaifu mkubwa.

Kwani wanawake hawawezi kuvumilia shida mpaka kuvunja misimamo yao ili wapate unafuu wa fedha kwa mtu ambaye waliapa kutojaribu hata kuwa naye ama kwa kuamua kusaliti penzi ama ndoa? Wanawake hawastahili kupata shida na kuvumilia?
 
Sio wote labda wenye tamaa na hizo hela
Siyo wanatamaa,mwenye tamaa huwa hatosheki na anajulikana.

nawaongelea wasio na tamaa ila wanapopatwa na shida ambazo kimsingi si kwa ajili ya mambo ya starehe wanalazimika kutumia miili yao ili wapate chochote kusolve matatizo yanayowakabiri.

mfano mimi naweza kuwa na mke ama mpenzi halafu nikiyumba kidogo kifedha japo si tajiri na wakati ambapo mpenzi/mke
wangu anapaswa kuvumilia mpaka mambo yakae sawa yeye anaweza kusaliti penzi ama ndoa kwa kuwa atasaidiwa hata shida kidogo na mchepuko.

huo ndo udhaifu ninaouona
 
Wanasema binadamu ambaye mawazo yake yameganda huyo ni kichaa. Hivyo mawazo ya mwanadamu yanabadilika kila wakati. Ndio maana si ajabu kuona mtu ametengua kiapo chake
 
Mkuu naona kama unawaonea sana wanawake.. wote wanaume na wanawake wana tamaa na udhaifu.. Na kila jinsia hapa mwisho wa siku inatumia karata iliyonayo katika kutatua shida au tamaa..

Wanaume wanaweka rehani mali zao, wengine wanaenda kuiba, wengine wanadhulumu na mengi mengineyo.. Wanawake wanatumia miili yao kutatua shida au tamaa zao..

Sasa useme kama ni sahihi au sio dhambi kwa mwanaume kwenda kuiba au kudhulumu ili aitosheleze shida au tamaa yake lakini sio sahihi na ni dhambi kwa mwanamke kuutumia mwili wake kuitosheleza shida au tamaa yake hiyo hiyo..!
 
wanawake wengi wanaweza kuwa na msimamo wa kumkataa mtu ama msimamo wa kutunza penzi la mpezi wake ama msimamo wa kutunza ndoa yake na kutofanya udanganyifu wowote.

lakini wengi wanapopata matatizo hasa ya kifedha hugeuka na kuwa walaini na kuifutilia mbali misimamo yote waliyoiamini na kuishikilia.

huu ni udhaifu mkubwa. kwani wanawake hawawezi kuvumilia shida mpaka kuvunja misimamo yao ili wapate unafuu wa fedha kwa mtu ambaye waliapa kutojaribu hata kuwa naye ama kwa kuamua kusaliti penzi ama ndoa?

ma wanawake hawastahili kupata shida na kuvumilia?

Mwanamke anahitaji Mtu anayeweza kuumimina Moyo wake.. Usinihoji zaidi.. Nawakilisha Na kuweka nukta. Wanawake mafukara Na wanafunzi ndio wanaopaparikia vijisent..
 
Mwanamme akianza kuonesha udhaifu kwenye mapenzi, basi na mwanamke ndio huzidi. anapohitaji hela mwanamke,huwezi kumwambia moja kwa moja bali unahitajika kumueleza atleast mipango yako ya kupata hela ili umpe
 
Mwanamke hakuumbwa ili apate shida . hata ukisoma vitabu vitakatifu utaona adamu ndiye aliyeambiwa utakula kwa jasho na si eva. Ukiona mwanamke anapata shida ujue amepeleka asset yake kwenye sehemu isiyo stahili.
 
mwanamme akianza kuonesha udhaifu kwenye mapenzi, basi na mwanamke ndio huzidi. anapohitaji hela mwanamke,huwezi kumwambia moja kwa moja bali unahitajika kumueleza atleast mipango yako ya kupata hela ili umpe

Umenena vyema.

Na sometimes mwanamke hafanyi kwa starehe, may be ana watoto ambao ni lazima wapate chakula, let alone kwenda shule. Sasa wewe mwanaume ukishasema huna hela, hata watoto huwawazi, kinyume na wanawake.
 
mfano mimi naweza kuwa na mke ama mpenzi halafu nikiyumba kidogo kifedha japo si tajiri na wakati ambapo mpenzi/mke
wangu anapaswa kuvumilia mpaka mambo yakae sawa yeye anaweza kusaliti penzi ama ndoa kwa kuwa atasaidiwa hata shida kidogo na mchepuko.

huo ndo udhaifu ninaouona
Yamekukuta???
 
Mshinga

Nikweli hususani hawa wa kizazi kipya wanajifanya hawawezi kuwa na uvumilivu hata kidogo hususani akimuona mwenzie yupotofauti na yeye kidogo lazima nae afosi maisha mazuri,
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom