Huu mwaka bora uishe tu, maana......

Kitoabu

JF-Expert Member
Jul 7, 2011
7,917
2,000
Nasemaje, huuu mwaka ni bora uishe, tena uishe kabisaaaah.
Yani katika uhai wangu, mwaka 2020 na mwaka 2017 ni miaka pekee ambayo sinta kaa nikaisahau, haki ya mama.

Huu mwaka (2020) nimezika zaidi ya marafiki 6 wa faida.

Nime zika kaka mkubwa Likoroma, huyu ndio wakwanza kufungua dimba.
Sikumbuki tarehe, lakini ilikua ni mwezi wa pili, kamkubwa alikufa kwa kupigwa na ng'ema (kufukiwa na shimo ) lawama ziwaendee waliokuwa wakifanya nao kazi, maana walikimbia kipindi jamaa (Likoroma) akiwa kafukiwa na kifusi, laiti wange kaza roho, Likoroma asinge kufa.

Wapili dogo Pita.
Dogo pita alikufa kwa ugonjwa wa Mareta (ugonjwa huu unatokakana na kubanduana na mwanamke alie toka kuzaa mda mchache ) kilicho mponza ni kuficha maradhi.

Tulimuuliza sana kama ametembea na dem mwenyewe tatizo hilo, ila alikataa kata kata, nahisi aliona haibu.

Mwisho wa picha pita tumbo lilijaa kama ana ujauzito na huo ndio ukawa mwisho wa maisha yake.

Watatu ni mchizi boti wangu Sura ya kazi.
Sura ya kazi alikufa kwa kufukiwa na gola (shimo) tulijitahidi kumfukua lakini tulishindwa, maana kila tukifukua ndio shimo lilizidi kukatika na kutishia maisha ya wengine.
Mwisho wa picha lile shimo (gola) ndio lilikua kabuli lake, tulimuacha hapo hapo, na mpaka leo eneo hilo limekua kama Maka au Islaer.

Mwingine ni Wamboka, na yeye alifia shimoni.
Huyu alifukiwa kama utani, yani mzungu (mwenye pori) katuulia mchimbaji mwenzetu.

Wamboka alikua ni mpole kupita kiasi, hata haya maisha ya uchimbaji Haku fanana nayo kabisa.

Mwengine ni prospa.
Prospa boss wangu umekufa kwa tamaa zako.
Kwa maisha haya magumu tunayo ishi wachimbaji usingekua na roho ya dhulma.

Kumbuka wengi wetu hatuja fika home Tanzania yapata miaka 7 sasa, kwa hiyo unapo dhulumu haki ya mtu tegemea kifo, nilikupenda ila mungu kakulipa ulicho stahili.

Mwengine ni Njaa (Fome fome) kama mwenyewe alivyo penda kujiita.
Njaa wewe ni zaidi ya jasiri nilie wahi kuwaona katika maisha yangu.
Japo nime zaliwa Daressalam, lakini kwa mtoto wewe wa Mbeya napiga saruti.

Njaa ndie shujaa wangu wa maisha yangu yote.
Ulisababisha tufanye kazi maning nice, kwa ajili yako nisha piga pesa nyingi, nakushukuru maboy.

Bila Risasi za tumbo ulizo pigwa wenda sasa hivi tuko New York kama ndoto zako zilivyo kua zikikutuma.
Tangu ufe, mgodini kumekua na njaa kama jina lako.

Wamwisho ni Abdul (Chikago) huyu ndio sina la kusema.
Nimekupeleka mwenyewe hospital.

TB ndio imekutupa.
Umeniachia ujumbe kua Pombe (kupitiliza) sigara, bange, ngono zembe hazina mpango katika maisha yetu ya utafutaji.

Sinto kusahau mpaka nakufa, kwani bado kidogo unifie mkononi kama sio kwenda kukununulia chakula.

Mungu aziweke mahali pema roho za marehem amin.
 

Grim Langdon

Member
Dec 21, 2020
85
125
Life goes on...
ob_04226a_oyyi-12.jpg
 

machiaveli

JF-Expert Member
Jun 4, 2016
1,082
2,000
We unasema huu mwaka uishe Tena mkuu nawakati ndio umeshaanza!

Au ulikua unamaanisha mwaka Jana Kama vipi mods wa ufute huu uzi?

Hauna maana
 

Ollachuga Oc

JF-Expert Member
Jul 4, 2016
14,212
2,000
Toka uko machimboni wewe halafu achana kushabikia litimu la hovyo kama manure cjui man u ..hizo ela ulizopata uko rudi nyumbani uwekeze..fungua hata banda la mpira mkuu

Unang'ang'ana na madini na bado unashabikia litimu la hovyo utakufa mdogo wangu rudi nyumbani kumenoga.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

Top Bottom