Huu msalaba wa Maamuzi mabovu unabebwa na nani? - Zitto Kabwe

ACT Wazalendo

Verified Member
May 5, 2014
429
1,000
Kilimo. Maamuzi. Msalaba.

Kilimo - Sekta ambayo inaajiri watu wengi ( takribani 70% ya Watanzania ) na ambayo inasisimua sana uchumi sasa inachechemea.

Waziri wa Fedha ametuambia juzi kwamba, Kilimo kimeshuka kasi ya ukuaji wake kutoka 2.5% hadi 0.6% mwaka 2016. Hii ni kasi ndogo zaidi kupata kutokea ya ukuaji wa sekta ya kilimo tangu nchi yetu ipate uhuru.

Kilimo kinatakiwa kikue kwa kasi ya asilimia 6 - 8 kwa mwaka ili kuondoa umasikini kwa kasi. Hata hivyo kiwango cha juu zaidi kufikiwa ni 4.4% katika kipindi cha kuanzia mwaka 2000 mpaka mwaka 2015. Hii ndio sababu ukuaji wa uchumi Tanzania hauondoi umasikini kwani sekta zinazoendesha ukuaji huo sio sekta za wanyonge.

Kushuka kwa kasi ya ukuaji wa sekta ya kilimo ni kiashiria kikubwa sana cha 1) kuongezeka kwa umasikini, 2) kupanuka kwa wigo wa wenye nacho na wasio nacho na 3) kuongezeka kwa ukosefu wa ajira. Hivi Ndio viashiria vya MAENDELEO na sio idadi ya ndege ambazo nchi inamiliki.

Kilimo kinaathiri usalama wa chakula na kadiri bei za vyakula zikiyumba, masikini wa mijini (urban poor) hali yao huwa mbaya zaidi. Kukauka kwa ghala la chakula ni matokeo ya uendeshaji mbovu wa uchumi usiozingatia hali za wanyonge na kukumbatia maonyesho ya vitu.

Unaposema kila mtu abebe msalaba wake mwenyewe, nani anabeba msalaba Wa makosa ya kimaamuzi na kisera yaliyofanywa na serikali na kusababisha njaa nchini?

Bajeti ya pembejeo za kilimo imeshuka kutoka shilingi 78 bilioni mwaka 2015/16 mpaka shilingi 10 bilioni mwaka 2016/17. Pembejeo hazikufika kwa wakulima kwa Wakati na zilizofika zilikuwa ghali Sana. Wakulima wengi wanyonge hawakuweza kulima kwa mbolea na ilibidi kutumia mbegu ambazo hazina ubora. Huu msalaba wa maamuzi kuhusu pembejeo anaubeba Nani? Wananchi?
 
Wamunzengo

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
810
250
mbona ndege zinawauma sana kila mara lazima mchombeze ndege. kwani huwezi tuu ukawasilisha hoja yako bila kutaja ndege.?

kwa hiyo ndege ndio zimemaliza pesa zote za serikali.? inawezekana una hoja ya msingi, ila kuingiza ndege kwenye hoja yako umeniharibia mood.

kilimo kiwe kilimo na ndege ziwe ndege. acheni ushamba wa kuwaza ndege kwennye kila mnalowaza.
 
Dumbuya

JF-Expert Member
Jan 23, 2014
532
1,000
Kwa ukuaji huo wa sekta ya kilimo hakika Tanzania ya Viwanda itangoja mno...labda wawekezaji waje na mashamba yao au malighafi zao ila itakuwa ajabu sana kwa wawekezaji kuja na malighafi zao kisha kuzalisha humu humu Tz.
 
Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
18,643
2,000
mbona ndege zinawauma sana kila mara lazima mchombeze ndege. kwani huwezi tuu ukawasilisha hoja yako bila kutaja ndege.?

kwa hiyo ndege ndio zimemaliza pesa zote za serikali.? inawezekana una hoja ya msingi, ila kuingiza ndege kwenye hoja yako umeniharibia mood.

kilimo kiwe kilimo na ndege ziwe ndege. acheni ushamba wa kuwaza ndege kwennye kila mnalowaza.
Kuwa na ndege siyo mbaya, bali anapotaja ndege anaonyesha priorities zetu zilivyo za hovyo.
 
Wamunzengo

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
810
250
Kuwa na ndege siyo mbaya, bali anapotaja ndege anaonyesha priorities zetu zilivyo za hovyo.
Mkuu, hakuna priority ya hovyo hapo. kwanza hilo lilishaisha, ndege zilishanunuliwa. nadhani tungeendelea na mengine. lakini kukaa tuna reffer ndege kila tukilala tukiamka ndege, hii inaonyesha tulivyo washamba. siku sekta ya utalii ikiinuka kutokana na ndege tunazonunua mkumbuke kuja hapa mkiri aibu zenu.

ndege...ndege...ndege..............basi zichukueni mzirudishe huko canada ili mfurahi.

nani aliwaambia ndege ndio zimezuia kilimo.? huu ni ushamba na ufinyu wa kufikiria.
 
Ileje

JF-Expert Member
Dec 20, 2011
5,890

Bado kuna ndege zingine zinakuja na zimelipiwa cash! Cash ambayo ingesaidia kununua pembejeo, mikopo kwa wanafunzi, kulipa madeni ya watumishi nk!

Sasa pasuka kabisa!
 
isotaaaa

JF-Expert Member
Sep 16, 2016
1,925
2,000
Kilimo. Maamuzi. Msalaba.

Kilimo - Sekta ambayo inaajiri watu wengi ( takribani 70% ya Watanzania ) na ambayo inasisimua sana uchumi sasa inachechemea.

Waziri wa Fedha ametuambia juzi kwamba, Kilimo kimeshuka kasi ya ukuaji wake kutoka 2.5% hadi 0.6% mwaka 2016. Hii ni kasi ndogo zaidi kupata kutokea ya ukuaji wa sekta ya kilimo tangu nchi yetu ipate uhuru.

Kilimo kinatakiwa kikue kwa kasi ya asilimia 6 - 8 kwa mwaka ili kuondoa umasikini kwa kasi. Hata hivyo kiwango cha juu zaidi kufikiwa ni 4.4% katika kipindi cha kuanzia mwaka 2000 mpaka mwaka 2015. Hii ndio sababu ukuaji wa uchumi Tanzania hauondoi umasikini kwani sekta zinazoendesha ukuaji huo sio sekta za wanyonge.

Kushuka kwa kasi ya ukuaji wa sekta ya kilimo ni kiashiria kikubwa sana cha 1) kuongezeka kwa umasikini, 2) kupanuka kwa wigo wa wenye nacho na wasio nacho na 3) kuongezeka kwa ukosefu wa ajira. Hivi Ndio viashiria vya MAENDELEO na sio idadi ya ndege ambazo nchi inamiliki.

Kilimo kinaathiri usalama wa chakula na kadiri bei za vyakula zikiyumba, masikini wa mijini (urban poor) hali yao huwa mbaya zaidi. Kukauka kwa ghala la chakula ni matokeo ya uendeshaji mbovu wa uchumi usiozingatia hali za wanyonge na kukumbatia maonyesho ya vitu.

Unaposema kila mtu abebe msalaba wake mwenyewe, nani anabeba msalaba Wa makosa ya kimaamuzi na kisera yaliyofanywa na serikali na kusababisha njaa nchini?

Bajeti ya pembejeo za kilimo imeshuka kutoka shilingi 78 bilioni mwaka 2015/16 mpaka shilingi 10 bilioni mwaka 2016/17. Pembejeo hazikufika kwa wakulima kwa Wakati na zilizofika zilikuwa ghali Sana. Wakulima wengi wanyonge hawakuweza kulima kwa mbolea na ilibidi kutumia mbegu ambazo hazina ubora. Huu msalaba wa maamuzi kuhusu pembejeo anaubeba Nani? Wananchi?
Unanswered cries........everyone come with complainments but no solutions on those complaints.

Unanswered Cries
 
Wamunzengo

JF-Expert Member
Aug 2, 2012
810
250
Bado kuna ndege zingine zinakuja na zimelipiwa cash! Cash ambayo ingesaidia kununua pembejeo, mikopo kwa wanafunzi, kulipa madeni ya watumishi nk!

Sasa pasuka kabisa!

wewe ndio utapasuka. mi ninachojua serikali ina pesa mpaka sasa hivi. pembejeo zitanunuliwa kwa wakati muafaka.
mikopo ya wanafunzi waliostahili wameshapata.
madeni ya watumishi yanalipwa kadri yanavyohakikiwa.

Mkuu, unapokuwa na sakata kama hili la watumishi hewa huwezi lipa lipa tuu bila kuhakiki.
 
Ranks

JF-Expert Member
Oct 21, 2012
2,592
2,000
images-1443.jpeg

Inakuhusu ewe mwananzengo.Kuijenga Tanzania mpya kutoka iliyofifia na kudhoofika ndani ya miaka 50 ya uhuru ilikuwa ni lazima kuanza na 1)kilimo.(2)reli~train za uhakika.,viwanda,ndege na kuendelea bila kusahau "elimu na afya " mwanzo mwisho speed 260.
Pia kumbuka compony za private zilisha~take cover kwenye usafiri wa anga kuokoa jahazi lililokwisha zama.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom