Huu mrengo wa kiuanaharakati uko twitter hauna mwisho mzuri, mbaya wao ni mbuzi aliyejivisha ngozi ya kondoo

Naanto Mushi

JF-Expert Member
Oct 16, 2015
6,236
15,602
Kuna huu mrengo wa kiuwanaharakati huko twitter ambao kwa siku za karibuni umejidhihirisha kuwa upo sambamba na sehemu muhimu ya chama cha ACT Wazalendo. Mrengo huu kwa siku za karibuni umekuwa ukifanya mashambulizi ya wazi wazi kwa chama cha CHADEMA pasipo haswa kuwa na hoja zenye mashiko zaidi ya matusi kwa viongozi wakubwa wa CHADEMA.

Pamoja na mrengo huu wa kiuanaharakati kuonesha kila mara kuikosoa serikali ya Rais Magufuli ila ajenda yao ya kuishambulia CHADEMA imekuwa fikirishi kwa wajuzi wa mambo kwamba yawezekana Grand Architects wa harakati hizi za Twitter wana nia ya kuiporomosha CHADEMA kutoka chama kikuu cha upinzani ili kuisaidia CCM kuendelea kubaki madarakani.

Wanachoshindwa kuelewa wana harakati hawa uchwara ni kwamba, hawajajua haswa ajenda kuu ya Grand Architects wa harakati hizi. Wamejisahau wanakula na nani, wapo gizani, na matokeo ndo haya tunayaona wanapotezwa taratibu taratibu na dola.

Hili ndo tatizo la kufanya harakati za kupelekwa na upepo kama bendera, pasipo kujua ajenda za anaye kutumikisha ni zipi. Ukweli ndo wanaupata sasa hivi kwamba hizo #harshtag na hao maaskari nyuma ya keyboard hawana msaada wowote.



Heri ya Christmas na Mwaka Mpya
Nipo Kibosho – Moshi
N.Mushi
 
Lengo lao ni kuuthibitishia ulimwengu kwamba Meko ni full Dikteta.

Naye bila kujitambua amekuwa akiwatuma polisi wawakamate kisha kuwafungulia kesi za kuzusha za uhujumu uchumi.

Mabeberu wanachofanya kwa sasa ni kurekodi matukio haya ya kihayawani ili baadae waje kumburuza the Hague huku wakiwa na ushahidi wa kutosha.

Angalizo: Meko ajiangalie sana. Hawa watu wanamwingiza mtegoni bila yeye kujijua. Hii inatokana na intelijensia mbovu aliyonayo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukiwa Msukule wa mtu/chama/kitu chochote unakosa akili kabisa.

Hivi kwanini watu weusi mkikosolewa mnaugua kabisa ?
Sijui una refer kitu gani haswa ila nachotaka kusema ni kwamba hao wanaojiita wana harakati wana ajenda za kutetea maslahi ya watu fulani na sio taifa.
 
Ben Bella,
Nakubaliana kabisa na wewe, kwamba haya yanayotokea yanatengeneza footprint ili yaje kuwa ushahidi hapo baadae. Ila shaka yangu kubwa ni kwanini wana harakati hawa hawa wanaishambulia pia CHADEMA ilihali wote ni wakosoaji wa serikali hiyo hiyo moja? Huoni kwamba kuna ajenda imejificha kwenye hizi harakati?
 
Wafuasi wa CHADEMA hapa ndio mnakera watu hamtaki kuambiwa madudu yenu mnataka mpigiwe makofi tu mda wote, hapa juzi mmenda mwanza kuomba ndoa ya mkeka, watanganyika wakastuka wanaanza wakalia kooni kuwahoji masuala mawili

Moja kwanini mnataka ndoa ya mkeka, ili hali uchaguzi serikali za mitaa imekuwa ndivyo sivyo, pili kwanini wanaotaka mchallenge mwenye chama cha CDM mnawachukia mjadala ukawa mkubwa kipi kilichotokea mkiwa bado mpo kwenye vikao vya uchaguzi ili kututoa kwenye mijadala na hao watu wenu akakamatwa kijana wawatu magoti lengo mtutoe kwenye hoja za msingi tuanze mjadili magoti na hilo mmefanikiwa hongereni sana

CHADEMA ni chama cha siasa
 
Watanzania tujifunze kutii sheria, kukosoa inaruhusiwa ila sasa huo uhuru mliopewa mnautumia vibaya...

Haiwezekani, mkosoe kwa lugha ya maneno makali, hapo sheria lazma ifuate mkondo wake...

Hata kwa Kabendera ilikuwa hivi mwisho wa siku yeye na familia yake wanateseka zile free erick kabendera zimepotea, hata kwa tito itakuwa hivi hivi hiki kikombe atakinywa yeye na familia yake...

Mungu ibariki Tanzania...

Mungu mubariki Mh. Dkt John Pombe Magufuli...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakika hauko Moshi. Wenye akili ndio watangamua lengo la hii hoja si kwa manufaa. Very cheap propaganda, try again
Wewe umengámua nini kwenye hoja yangu hii? Kiweke ulichongámua ili nione kama kina mashiko. Mimi napinga waziwazi hii ajenda ya wanaharakati kukishambulia chama cha CHADEMA angali wote ni wakosoaji wa serikali. Haijalishi, sote tunajua CHADEMA kina mapungufu yake ya kiuongozi ndani ya chama ila walichofanya wanaharakati kuiweka hiyo kama ajenda ya kuishambulia CHADEMA ni makosa makubwa sana.
 
Watanzania tujifunze kutii sheria, kukosoa inaruhusiwa ila sasa huo uhuru mliopewa mnautumia vibaya...

Haiwezekani, mkosoe kwa lugha ya maneno makali, hapo sheria lazma ifuate mkondo wake...

Hata kwa Kabendera ilikuwa hivi mwisho wa siku yeye na familia yake wanateseka zile free erick kabendera zimepotea, hata kwa tito itakuwa hivi hivi hiki kikombe atakinywa yeye na familia yake...

Mungu ibariki Tanzania...

Mungu mubariki Mh. Dkt John Pombe Magufuli...

Sent using Jamii Forums mobile app
Hahahahhaaaaa naona mmehamia huku.
 
REJESHO HURU,
Hoja yako ni dhaifu, bado haswa hujaniambia ni kitu gani kinasababisha wanaojiita wanaharakati hawahawa kuishambulia CDM. Na ndo mana nikasema, hao ma Grand Architect wa harakati wana ajenda kubwa ya kuiua CDM kwa maslahi ya CCM. Ila watu kama wewe kwa kuwa hamuwezi ku connect dots mtabaki vibaraka na wahanga.
 
Back
Top Bottom