Huu hapa ndio ukweli kuhusu kinachoendelea sasa Zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huu hapa ndio ukweli kuhusu kinachoendelea sasa Zanzibar

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by GHIBUU, Oct 27, 2012.

 1. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #1
  Oct 27, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,188
  Likes Received: 705
  Trophy Points: 280
  Ukweli ni kwamba kuna viongozi wa juu kwenye serikali ya Zanzibar ambao kwa kushirikiana na Idara ya Usalama wa Taifa ya Tanzania wanahusika moja kwa mja kwenye machafuko ya Zanzibar kuanzia yale ya kwenye uchaguzi mdogo wa Bububu hadi haya sasa.


  Lengo kubwa ni kuhakikisha kwamba ajenda ya Wazanzibari kudai mamlaka kamili kupitia mchakato wa Katiba Mpya inashindwa kwa kuiua kabisa serikali ya Umoja wa Kitaifa na Maridhiano.


  Makubaliano ya pamoja kati ya Dodoma, kundi la vibaraka wao kwenye GNU na CCM Zanzibar na Idara ya Usalama wa Taifa, ni kwamba Maridhiano yaliyozaa GNU ndio adui nambari moja wa mfumo wa Muungano uliopo. Sasa ili kuulinda mfumo huu wa Muungano, ni lazima kumuangamiza adui huyo. Na ndicho kinachofanyika sasa.


  Tukio la kutekwa kwa Ustaadh Farid lilikuwa la kweli na lilikuwa ni sehemu ya programu hiyo kubwa ambayo inagharimu mamilioni ya fedha za walipa kodi wa Tanzania nzima na si wa Zanzibar peke yake. Kiasi cha mwezi mzima kabla ya Ustaadh Farid kutekwa, kijana mmoja wa Idara ya Usalama wa Taifa anayefanya kazi Zanzibar, alijenga mahusiano makubwa na viongozi wa juu wa Uamsho, hasa Sheikh Farid.


  Kijana huyu, ambaye hakujificha kwamba ni mtu wa Usalama wa Taifa, alijitokeza kama sehemu ya kundi la watu waliomo kwenye taasisi za dola na ambao wanaunga mkono Ajenda ya Zanzibar. Kwa maslahi ya ajenda hiyo, na kwa maslahi ya Zanzibar, bahati mbaya viongozi wa Uamsho walimuamini. Ni yeye ndiye aliyekuwa mtu wa mwanzo kabisa kumpigia simu Sheikh Msellem saa 2:00 usiku wa siku ya kutekwa kwa Imamu Farid, kumjuulisha kwamba Usalama wa Taifa wamemkamata Sheikh Farid.


  Ndani ya siku tatu za suintofahamu hiyo, ni yeye aliyekuwa akiwashinikiza viongozi wa Uamsho na vijana kwamba ni lazima shinikizo kubwa lifanyike kama kweli wanataka kiongozi wao aachiwe akiwa salama.


  Kwa hakika, siku ya pili yake aliwasiliana na kukutana na Sheikh Msellem, na kumuambia kwamba alikuwa tayari kumpeleka aliko Sheikh Farid. Baada ya kuingia kwenye gari, hakumpeleka kwa Sheikh Farid, bali alimwambia kwamba wazungumze naye kwa simu kwanza, akiwa tayari ameshaipiga simu hiyo, kwa alivyosema.


  Kwenye simu, ni kweli Sheikh Msellem alisikia sauti ya Sheikh Farid ikimuambia kwamba ametekwa na wanamtesa, na kwamba kama hawakujikaza basi wanaweza hata kumuua. Alipotaka kuuliza mengi zaidi, Sheikh Msellem hakuweza maana ile simu ilikatwa.


  Kumbe kilichokuwa kimefanyika, ni kuwa Sheikh Msellem alisikilizishwa sauti ya kurikodi ya Sheikh Farid na hakuwa anazungumza naye moja kwa moja. Ilikuwa ni baadaye sana, viongozi wa Uamsho walipokuja kung’amua hayo.
  Ndani ya kipindi hicho cha kupotea kwa Ustaadh Farid, viongozi wa serikali ya Zanzibar wanaohusika na programu yao, waliyatoa makundi ya vijana wao kuchoma maskani za Kisonge, kuharibu mali, kuiba, kupiga, kujeruhi, na hata kuua.


  Katika purukushani hizo, vijana hao walikuwa wakipigana na kuumizana wenyewe kwa wenyewe. Miongoni mwao ni askari aliyepigwa risasi na kuuawa na wenzake, lakini huyo hatajwi kabisa na vyombo vya habari, badala yake anatajwa askari aliyeuawa Bububu kwa kukatwa mapanga, na ambaye huenda kabisa asiwe na uhusiano na matukio haya.
  Miongoni mwa vijana walioumizwa wako waliojeruhiwa vibaya na ambao hadi sasa wamelazwa kwenye hospitali ya jeshi ya Bububu, lakini taarifa zao zimewekwa siri sana. Kilichotokea, ikiwa ni sehemu ya programu hiyo kubwa, ni kwa Idara ya Habari Maelezo ya SMZ kutoa agizo kwa vyombo vyote vya ndani vya habari kutokutangaza kabisa matukio ya sasa, tangu kukamatwa kwa Sheikh Farid.


  Kwa hakika, hata katika kamatakamata ya polisi, nao pia wamewakamata vijana kadhaa wa makundi hayo lakini huwa wanawaachia kwa amri ya Kamishna Mussa Ali Mussa, Mkuu wa Jeshi la Polisi la Zanzibar, ambaye ni sehemu ya programu hiyo ya kuivunja GNU.


  Sheikh Farid aliachiliwa baada ya uingiliaji kati viongozi wawili wa juu GNU, kwa kuanzia na Makamo wa Kwanza wa Rais Seif Sharif ambaye baada ya kufahamishwa undani wa mkasa mzima alimwendea Rais Ali Shein, na kumuambia maneno yafuatayo: “Mhe. Rais ninasikitika sana kwamba sisi wenyewe ndio tunaohusika na haya yanayotokezea hivi sasa.

  Watu wetu wanajua wapi alipo Sheikh Farid. Wanafanya hivi kukuharibia wewe uonekane kwamba huna uwezo wa kuongoza na kwamba unaiwachia nchi iingie kwenye machafuko. Lakini zaidi wanafanya hivi ili kuivunja GNU, maana watatufanya sisi tujihisi kwamba ni sehemu ya uozo huo nasi hatutakubali. Sasa waambie watu wako ambao wako chini ya ofisi yako (akamtaja kwa jina yule kijana wa Idara ya Usalama wa Taifa) wakuoneshe walipomueka Farid.” Usiku wake, saa 2:00 Sheikh Farid akaachiliwa.


  Lakini hadi kuachiliwa kwa Sheikh Farid, tayari sehemu ya lengo moja kwenye mkakati wao ilishafanikiwa: nayo ni kutengeneza mazingira ya fujo na kuhalalisha matumizi ya nguvu, ghasia na uvunjwaji wa haki za binaadamu kama yanayoendelea sasa.


  Pia kwa sababu ya kuficha uovu na asili ya mkasa mzima, wamemkamata Sheikh Farid na viongozi wa Uamsho ambao wanaujua ukweli wote wa mkasa huu, na sasa wamewaweka ndani na kuwafungulia mashitaka kadhaa, ili wasiwe nje wakaweza kuueleza umma kile hasa kilichotokea.


  Kwa upande mwengine, wanavilisha vyombo vya habari vya Tanzania Bara na vile vya Zanzibar vinavyopinga Maridhiano na Umoja wa Kitaifa, taarifa za uongo kuhusu viongozi hao wa Uamsho na wafuasi wao. Picha inayojengwa ni kwamba Uamsho ni magaidi na hivyo wapate kuhalalisha kuongeza wanajeshi na matumizi ya nguvu ya vyombo vya dola dhidi ya raia wanaodai mfumo wa Muungano wa Mkataba.


  Hivi sasa operesheni ya kijeshi imeimarishwa kisiwani Unguja, hasa kwenye mkoa wa Mjini Magharibi, ambako Tume ya Kukusanya Maoni ya Katiba Mpya inakuja hivi karibuni. Wananchi wanatishwa na wanatiwa hofu na mazingira yanajengwa ya kuzuia maoni ya wananchi hao mbele ya Tume, maana hadi sasa wengi waliokwishatoa maoni yao, wameshasema wazi wanataka mabadiliko ya msingi kwenye Muungano.


  Matokeo wanayoyatarajia ni aidha kwa wananchi wanaopigwa na makundi waliyoyatayarisha na vikosi vya SMZ kujibu mapigo na hivyo kuiingiza nchi moja kwa moja kwenye fujo za kudumu, au kwa wajumbe wa CUF kwenye GNU kuja juu na kujitoa kwa kupinga dhuluma hii. Lolote kati ya mawili hayo, mwisho wake ni kuyavunja maridhiano na umoja wa kitaifa na hivyo kuiua na kuizika kabisa Ajenda ya Zanzibar.


  Kwa upande wa wananchi, programu hiyo inalenga kuwavunja moyo wao kwa serikali ya GNU, hasa kwa wafuasi wa CUF mbele ya Makamo wa Kwanza Seif Sharif, ambaye wanajengewa picha ya kwamba amewasaliti na haguswi na mateso wanayoyapata.


  Mwenyewe Maalim Seif analijua na analifuatilia kwa karibu kila linalotokea na anamshauri Rais Shein kama ulivyo wajibu wake kama makamo wa kwanza wa Rais. Amechukua na anaendelea kuchukua kila jitihada za kumsaidia Rais Shein na kuilinda GNU isianguke, maana ikianguka ndio hatima ya Zanzibar imekwenda pamoja nayo.


  Katika ghasia zinazoendelea sasa kwenye jimbo la Bububu, amemfahamisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais anayehusika na vikosi vya SMZ, Dkt. Mwinyihaji Makame, na amemueleza wazi kwamba kinachofanyika ni uvunjaji wa haki za binaadamu, mateso na udhalilishaji, ambao mwisho wake ni kwa wananchi kuamua kujilinda na machafuko yakisambaa, hakuna hata mmoja atakayenusurika, si Dkt. Mwinyihaji wala si yeye Maalim Seif.


  Laiti Rais Ali Mohammed Shein ana dhamira, nia na uwezo wa kuinusuru ndiye mwenye nafasi ya juu kufanya hivyo. Wapinzani wa Maridhiano na Umoja wa Kitaifa walikuwapo pia wakati wa muasisi wake, Rais Amani Karume, lakini alikuwa na uthubutu wa kuwadhibiti.


  Rais Shein kwa upande ake anaonekana kuelemewa vibaya na kundi la wapinzani wa Maridhiano na Umoja wa Kitaifa waliomo kwenye serikali yake, chama chake na vyombo vyake vya usalama. Kundi hilo ambalo linatumikia ajenda ya Tanganyika dhidi ya Zanzibar, kama ilivyoonekana wazi, liko tayari hata kukanyaga maiti za Wazanzibari alimradi tu lifikie kwenye lengo lake.


  Kwa hivyo, inabakia kuwa juu ya Wazanzibari ambao sasa wanateseka chini ya mikono ya kundi hilo aidha kulipa nafasi ya kumaliza kazi liliyoianza ya kuisimamisha ajenda ya Tanganyika, au kuyapa nafasi Maridhiano na Umoja wa Kitaifa nayo kumaliza kazi yaliyoianza ya Ajenda ya Zanzibar.


  Zanzibar imeanza tena kuzama. Inahitaji kuokolewa hivi sasa.
   
 2. Iselamagazi

  Iselamagazi JF-Expert Member

  #2
  Oct 27, 2012
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 2,221
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Imekaakaa kama ile ya Ulimboka! Bora hata ile ya Ulimboka, ni true fact.
  Can you believe the source?

   
 3. s

  swrc JF-Expert Member

  #3
  Oct 27, 2012
  Joined: Jun 17, 2012
  Messages: 442
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  habari ndeeeefu haina mvuto wala mashiko na bado in maswali mengi
   
 4. Indian

  Indian JF-Expert Member

  #4
  Oct 27, 2012
  Joined: Oct 27, 2012
  Messages: 749
  Likes Received: 542
  Trophy Points: 180
  Zanzibar ni ndogo tu watu wanajuana na dawa yake ni ndogo pia.
   
 5. m

  mantegi Member

  #5
  Oct 27, 2012
  Joined: Oct 16, 2012
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  maswali ni mengi sana mfano, ilikuaje amtume dereva wake huku akienda peke yake kukutana na watu asiowajua??
   
 6. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #6
  Oct 27, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,347
  Trophy Points: 280
  Huyu Shekh Farid twasikia anafadhiliwa uarabuni, kwanini huyu GHIBUU hasemi connection hiyo?
   
 7. MWEEN

  MWEEN JF-Expert Member

  #7
  Oct 27, 2012
  Joined: Feb 6, 2010
  Messages: 472
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 45
  Kichwa cha uzi kingekuwa "TAMKO LA CUF KUHUSU VURUGU ZA ZANZIBAR". Inaonekana imehaririwa na Jussa.
   
 8. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #8
  Oct 27, 2012
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,752
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  ngoja ntaisoma....then ntachangia kitu hapa
   
 9. J

  JokaKuu Platinum Member

  #9
  Oct 27, 2012
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,778
  Likes Received: 5,000
  Trophy Points: 280
  GHIBUU,

  ..ndiyo maana sisi wengine tumekuwa tukisema hakuna haja ya kuendesha kampeni na mihadhara ya CHUKI dhidi ya wa-Tanganyika na Mwalimu Nyerere.

  ..njia rahisi ya kuuvunja muungano ni wawakilishi kupitisha azimio la kutangaza mgogoro wa muungano, na wabunge wa ZNZ kujitoa ktk bunge la muungano.

  ..kama mliweza kupitisha azimio la kuunda serikali ya umoja wa kitaifa, basi hata hayo niliyoyaeleza yako ndani ya uwezo wenu WAZANZIBARI.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 10. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #10
  Oct 27, 2012
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  Mwandishi ana hoja kwenye andiko lake, lisomeni kwa mapana yake kuna kitu mtatambua hapo
   
 11. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #11
  Oct 27, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,227
  Trophy Points: 280

  hakuna mwenye jeuri wala dhamira ya kuvunja muungano....

  Viongizi wao wamezoea kuwatumia kama ngazi ya madaraka, wanatumia chuki zao kama mtaji, wakiwa nao wanawachochea wakigeuka wanapooza....

  Zooote blah blah tu
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 12. Che Guevara

  Che Guevara JF-Expert Member

  #12
  Oct 27, 2012
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 1,178
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 145
  Kumbe, kwa mujibu wa mleta mada, viongozi wa serikali ya umoja wa kitaifa ya Zanzibar wanahusika na vurugu ambazo pia zimehusisha kuharibu baa, kuiba bia kwenye makreti, kuchoma makanisa na kuharibu maskani za CCM?

  Ila ni kama imetoa vitu fulani kwenye sakata la Ulimboka na kutengeneza movie nyingine...
   
 13. q

  querauk Member

  #13
  Oct 27, 2012
  Joined: Oct 13, 2012
  Messages: 54
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Acha uongo. Kinachofahamika hao waliokamatwa ndiyo wamekuwa vinara wa vurugu huko zanzibar. wao ndio wachoma makanisa na kuharibu mali nyingi nyinginezo, wanawatusi watu wa madhehebu mengine kwa sababu tu ya kuwa viongozi waliopo madarakani ni waimani yao. Haiwezekani kuachia hali hii iendelee Nchi hii ni ya kwetu wote na siyo ya watu fulani au imani fulani. Serikali ihakikishe inawafunga wote wanaohusika na sakata hili na ikipainika siyo raia wa nchi hii warudishwe kwao wakafanye fujo huko.
  Matukio haya yanaudhi na kutia kichefuchefu na yasiachiwe yaendelee
  Mungu ibariki Tanzania
   
 14. masopakyindi

  masopakyindi JF-Expert Member

  #14
  Oct 27, 2012
  Joined: Jul 5, 2011
  Messages: 13,918
  Likes Received: 2,347
  Trophy Points: 280
  Kweli mkuu JokaKuu, these people never learn.
  Kwa vurugu na kuleta fujo watadhibitiwa tu na waTnganyika , wapende wasipende.
  Watumie ustaarabu tu wa kupitisha maazimio ya kuunda nchi yao.
  Wakitaka kisago watakipata tu.
   
 15. Makala Jr

  Makala Jr JF-Expert Member

  #15
  Oct 27, 2012
  Joined: Aug 25, 2011
  Messages: 3,397
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Kuvunjwa kwa GNU ni kwa manufaa ya nani? | Kama watu wanaopanga wapo nyuma ya Dr.Shein,sasa inakuwaje hata ofisi za ccm zichomwe? | CUF wana jambo la kujibu kabla ya Dr.Shein wa CCM
   
 16. H

  Hydrobenga JF-Expert Member

  #16
  Oct 27, 2012
  Joined: Jun 24, 2012
  Messages: 1,124
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Habari ni nzuri tu kama utaisoma kwa makini....
  Lakini Kaa ukijua Hoja zote zinazoihusu zanzibar teyari watu wana majibu rahisi..kama
  Wavaa vipedo
  Wafuga ndevu
  Wavaa Kubazi
  Wacheza bao
  Wake wa waarabu
  Wala haluwa
  Wala tende
  Wafuga Majini
  Mashoga



  Halafu watu hawa wanajiita wasomi .....
  Bora Hoja kama hii uipeleke mzalendo.net utapata michango ya maana
   
 17. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #17
  Oct 27, 2012
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,437
  Likes Received: 19,791
  Trophy Points: 280
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. m

  mishalejuu Senior Member

  #18
  Oct 27, 2012
  Joined: Jun 27, 2012
  Messages: 196
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hiki ndicho kilichojili....wanaJF changieni sasa juu ya nini kifanyike sio muanze kutoa maswali. maada iko wazi kabisa inatakiwa mawazo kutoka kwa great thinkers kama mnavyojitambulisha! tuache ubaguzi!
   
 19. GHIBUU

  GHIBUU JF-Expert Member

  #19
  Oct 27, 2012
  Joined: Jan 13, 2011
  Messages: 3,188
  Likes Received: 705
  Trophy Points: 280
  Nakubaliana na wewe asilimia mia moja,tatizo lipo kwa rais wetu wa zanzibar,kama rais atakuwa tayari kwa hilo basi hakuna shaka kwa hilo linaweza kufanyika .lakini tatizo lipo kwa rais na ameapa kulinda muungano kwa nguvu zote kwani urais alio upata amepata kwa nguvu za kijeshi na viongozi wa tanganyika walio muweka.

  Rais kama angelikuwa anawasikiliza wananchi basi yasingelitoekea haya yote,wakati ilipoundwa serikali ya umoja wa kitaifa rais mwenyewe ndio alio isimamia ,japokuwa kulikuwa na changamoto ndogo ndogo za baadhi ya watu ambao walikuwa hawataki umoja wa wazanzibari kuwa kitu kimoja,lakini hawakuweza kufua dafu kwa vile rais ndio alie simamia suala la GNU.
   
 20. Bilionea Asigwa

  Bilionea Asigwa JF-Expert Member

  #20
  Oct 27, 2012
  Joined: Sep 21, 2011
  Messages: 12,627
  Likes Received: 9,840
  Trophy Points: 280
  ngumu kumeza hii kitu aisee.........
   
Loading...