Huu hapa mchezo mchafu waliofanyiwa chadema korogwe vijijini

DAMAS DAMIAN

Senior Member
Apr 8, 2011
115
54
Chama cha demokrasia na maendeleo wilayani Korogwe kimejikuta katika wakati mgumu kufuatia maamuzi ya kamati ya rufaa yaliyopelekea kuenguliwa kwa wagombea wa chama hicho kwa vijiji Zaidi ya 98 vya jimbo la Korogwe vijijini.

Uamuzi uliotolewa na kamati ya rufaa siku ya jumatatu tarehe 01/12/2014 saa nane mchana umewanyima sifa za kugombea wateule wa chadema kwa kutumia mihuri isiyo sahihi na wengine wakidaiwa ya kwamba sio wanachama wa chadema bali ni wanachama wa chama cha mapinduzi.
Baada ya kupokea maamuzi kablasha lenye maamuzi hayo ya kamati ya rufaa, viongozi wa chadema wakiongozwa na Thomas Luoga(Katibu wilaya)na Aminata Sagutiwalikwenda kumuona msimamizi wa uchaguzi wa wilaya kwa ajili ya kupata ufafanuzi juu ya mambo hayo yaliyoamuliwa na kamati ya rufaa, Mkurugunzi wa halmashauri Bwn Mweri alisema hana cha kufanya hasa ukizingatia kwamba uamuzi wa kamati ya rufaa ndio ya mwisho. Walikwenda katika mamlaka mbali mbali za mkoa na taifa kwa ajili ya kupinga uonevu huo, mpaka sasa juhudi zinaendelea kuhakikisha haki inapatikana kwa wagombea walioenguliwa kwa hujuma.


MAMBO YANAYOZUA UTATA KATIKA UAMUZI WA KAMATI YA RUFAA
Ifahamike ya kwamba kamati ya rufaa ya wilaya inaongozwa na katibu tawala wa wilaya, pia kamati hiyo inashughulika na rufaa zilizowekwa na wagombea baada ya kutoridhishwa na uamuzi wa wasimamizi wasaidizi wa ngazi ya kijiji na kata. Na kwa mujibu wa muongozo wa uchaguzi, kamati ya rufaa ilipaswa kufanya kazi ya kusikiliza rufaa ndani ya siku nne kuanzia tarehe 26/11/2014 mpaka tarehe 29/11/2014. Kamati ya rufaa imefanya kinyume kama ifuatavyo:-


1Kamati ya rufaa imefanya kazi nje ya muda uliopangwa, uamuzi wa kuwaengua wagombea wa chadema ulifanyika siku ya tarehe 01/12/2014 wakati rufaa zote zilipaswa kuishia tarehe 29/11/2014


Wagombea wa chadema wameenguliwa huku kukiwa hakuna mapingamizi yaliyowahi kuwekwa kwa wasimamizi wasaidizi na wala hakuna uamuzi uliowahi kutolewa na wasimamizi wasaidizi uliopelekea kwenda kukata rufaa, kinyume chake kamati ya rufaa haijafanya kazi ya kusikiliza rufaa bali imeamua kushiriki hujuma dhidi ya chadema.




3Wakati kamati hiyo ikiwaengua wagombea wa chadema kwa kosa la kutumia mhuri usiostahili tena wakiwa hawajawahi kuwekewa pingamizi, wakati huo huo kamati hiyo imewarudisha wagombea wa ccm ambao waliowekewa pingamizi la fomu zao kutokugongwa mhuri wa chama kabisa.


Mpaka sasa haifahamiki kamati hii ya rufaa imetumia vigezo gani kuwaengua wagombea ambao ni wanachama wa chadema na wamedhaminiwa na chadema kwa kosa la kwamba sio wanachama wa chadema bali ni wanachama wa CCM. Kwani uanachama wa mtu unakoma pale anapoamua kujiunga na chama kingine cha siasa.


Wasimamizi wa uchaguzi wamekabidhiwa nakala ya maamuzi yaliyofanyika, bila kuwepo kwa barua inayowaelekeza nini wanapaswa kufanya, badala yake wanapewa maelekezo kwa njia ya simu yanayosisitiza kuheshimiwa kwa maamuzi ya kamati ya rufaa lakini wakati huo huo kuheshimu ratiba za kampeni.

6 Mpaka sasa wagombea wengi wanaoambiwa kwamba wameenguliwa hawajapatiwa barua kutoka kwa msimamizi msaidizi za kuwataarifu ya kwamba wao sio wagombea halali, kinyume chake wamekuwa wakielekezwa kwa mdomo kwani watendaji walio wengi wamekiri kuhofia kuandika barua hizo ili kuepuka kuingia mtegoni kwa kuwa hata kamati ya rufaa haijawaandikia barua ya kuwaelekeza nini cha kufanya.


MSIMAMO WA CHADEMA KOROGWE
Uongozi wa Chadema wilaya ya Korogwe kupitia kwa katibu wa wilaya Thomas Luoga umewaagiza wagombea walionguliwa pamoja na viongozi wa maeneo husika kuendelea na kampeni kama kawaida kwani wao ni wagombea halali. Hii ni kwasababu mpaka muda wa mapingamizi unakwisha, wagombea walioenguliwa hawajawahi kupokea taarifa za kuwekewa mapingamizi waliowekewa kutoka kwa wasimamizi wasaidizi na badala yake wamepokea maamuzi ya kamati ya rufaa tu. Na mpaka sasa jambo hili limeshafikishwa kwenye ofisi ya katibu mkuu wa chama taifa.
Pia Chadema wilaya ya Korogwe kimeazimia kutumia mamlaka zote kupinga uonevu huu na hata ikibidi kufungua kesi mahakamani dhidi ya wote waliohusika.
Imeandikwa na,
Damas Damian Kawonga,
Korogwe Yetu
08/12/2014
 
Back
Top Bottom