chuwaalbert
JF-Expert Member
- Sep 17, 2010
- 3,598
- 2,115
Hussein Mwinyi, raia mwenye bahati ya kupata kuwa mbunge kupitia majimbo ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar na Pemba, alisema Bungeni kuwa kuondolewa kwa kero za Muungano ni kwa Zanzibar kuruhusiwa kujiunga na OIC, na kupata fursa SAWA katika ajira za Muungano, ili kupata amani na ustawi wa jamii. Alisema: Kero ya mgawo wa ajira za Muungano uwekewe utaratibu utakao hakikisha uwepo (kuwepo?) kwa uwiano mzuri wa ajira za Muungano kati ya Zanzibar na Bara(tamka Tanganyika).
My take: Misimamo hii ya Wazanzibari ya SIKAKI NATAKA ndo inakwamisha kuimarika kwa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar. Tanganyika itoke katika mbeleko ya Tanzania na ije nje, wazi ili kila Nchi iwe na Hazina yake yenyewe na mambo madogo kama ya usawa wa ajira yatajitatua kwa kuangalia uwiano wa mchango wa kila Nchi katika Mfuko wa pamoja.