inategemea na situation yenyewe, na huko kwenu unapeleka kivipi, unapeleka kimshitaka|? au kutaka ushauri..
wakati mwingine kama una mzazi mfn mama msiri waweza kumwambia akupe ushauri, lkn asimwambie baba na watu wengine..yaani aweke moyoni..kama unaelewana na mama yako mbona huyo ndo rafiki yako wa kwanza..ila pia uangalie na ishu yenyewe maana unaweza kumwambia mama yako kitu akaumia kuliko hata wewe mwenye tatizo mwishowe mkaanza kuuguza presha na kisukari..
mimi binafsi sina wazazi wote walishafariki, nina ndugu lkn huwa siwashirikishi matatizo ya home kwangu, lkn napata tabu sana kwani wakati mwingine huwa natamani mama yangu angekuwa hai, nimueleze kitu fulani anishauri au anipe moyo....basi naishiaga tu kuliaa na kubaki na matatizo yangu moyoni...kuna wakati hasa kwa msichana, binti aliyeolewa atahitaji ushauri wa mama..
huu ni kwa mtizamo wangu lkn