Huruma za wazungu sometimes ni kituko... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Huruma za wazungu sometimes ni kituko...

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by Leornado, Jul 23, 2011.

 1. L

  Leornado JF-Expert Member

  #1
  Jul 23, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,534
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Hii nimeikuta kwenye wall page ya mholanzi aishiye Arusha, akielezea furaha ya kuokoa maisha ya mbwa.

  "I think it is safe to tell now, we have a new puppy her name is Suffy and she survived the streets of Arusha, she improves, karibu nyumbani"


  Huruma hii angefanya kwa mtoto wa mtaani ningemwelewa, yeye kaona bora aokote kambwa street na kuishi nako.

  Kweli Africa na european tumetofautiana kwenye vipaumbele.
   
 2. Mshume Kiyate

  Mshume Kiyate JF-Expert Member

  #2
  Jul 23, 2011
  Joined: Feb 27, 2011
  Messages: 6,774
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 135
  Duuuuuu!!!
   
 3. MAMMAMIA

  MAMMAMIA JF-Expert Member

  #3
  Jul 23, 2011
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 3,822
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Ni rahisi kumwokoa mbwa wa mitaani kuliko mtoto wa mitaani.
  Hakuna atakayekwenda kudai kuwa mbwa huyo ni wake, lakini kwa mtoto wa mitaani mara watatokea akinababa kumi kudai kuwa ni mtoto wao. Tena sikwambii serikali, watamwanda wamkamue kwa rushwa hadi akome. Atakiwa awe na kibali/ruhusa ya kubaki na mtoto huyo. Diwani atadai mtoto huyo yuko katika manispaa yake kwa hivyo apatiwe mchango wa kuendeleza manispaa. Mkuu wa Wilaya atadai ofisi za vizazi na vifo liko katika hali mbaya, wanahitaji msaada wa kulijenga ili litoe huduma za kisasa. Wanaharakati watadai anataka kumuuza kama mtumwa. Watu wa dini watadai huyo ni gay au pedophile. Haya yote hayatomfika kwa kuokoa maisha ya mbwa.
   
 4. L

  Leornado JF-Expert Member

  #4
  Jul 23, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,534
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Nimekupata ndugu, lakini mie naona kama ni kufuru flani kwani Binadamu kwanza halafu mmbwa baadae. Can u imaginine hicho kijimbwa kimepelekwa clinic na kinapewa maangalizi maalumu?
   
Loading...