Natafakari hii huruma inayopigiwa chapuo sasa na wana CCM kuhusu umoja na mshikamano.Hali hii imezidi kipindi hiki cha matukio hasa tukio la kutaka kumuwa Lisu kushindikana.
Kuna dhana kuu mbili hapa tunalazimka kuzitazama kidogo.
1. Dhana ya kujikosha baada ya kuumbuka
Dhana hii inajengeka kuhusu huruma ya ghafla kwa wapinzani wakati ni miaka karibu 2 sasa wapinzani wamepatwa na masaibu makubwa yaliyotishia mustakbali wa nchi. Hakuna mwana CCM aliyethubutu walau kukemea mwenendo ulivyo hadi sasa.
WAPINZANI WAMENYANYASWA BUNGENI, WAMENYANYASWA NA POLISI na kusumbuliwa sana. Bungeni ni mfano hai kwa sababu wabunge wote walistahiki kutendewa sawa na kama ni kanuni zilipaswa kuwa sawa kwa wote lakini hali haikuwa hivyo. Makosa yale yale waliyohukumiwa wapinzani yamefanywa na wabunge wa CCM na hawakuchukuliwa hatua yoyote.
Hali ya manyanyaso imekwenda na wapinzani wamekuwa wakipiga kelele na hata kutahadharisha kuwa HAKUNA ATAKAYEKUWA SALAMA mpaka sasa imefika mahala Tundu Lissu huyu huyu kwa mfano alie mkosoaji mkubwa wa serikali kupigwa risasi eti ndio huruma inakuja na tayari kukiwa na mpasuko wa kiitikadi katika nchi.
Dhana hii ya kujikosha inaonesha CCM kuwa wanafanya unafiki wa wazi baada ya kuona malalamiko kupitia taasisi za kiraia na kisheria zinalaani tukio la Lissu na wao kuamuwa kufanya unafiki. Tumeshangazwa na CCM eti kulaani leo na hata kutoa matamko ya kutaka wahalifu washikwe .
2. Dhana ya uwoga na kumsaliti mwenyekiti wao
Dhana hii nayo inaonesha wana CCM wengi ni waoga na pengine hawaridhiki na kile kinachoendelea katika nchi lakini hawana uwezo wa kukabiliana na mwenyekiti wao.
Rais JPM akiwa mwenyekiti wa CCM alishatoa msimamo wa kutoshirikiana na wapinzani na kuwaita watakaofanya hivyo kuwa WASALITI. Hili lilikuja wakati wabunge wa CCM walipokwenda kumtembelea Mh Lema Gerezani waliitwa wasaliti.
Sasa leo CCm na wanachama wake wakiwemo UVCCM, Katibu wa Uenezi na hata wanachama mmoja mmoja wamepatwa na nini kutoa kauli zinazoonesha kuguswa na wapinzani (Lissu) wakati walishaambiwa ni usaliti ? Hapa ni dhahiri kuna uoga ulioambatana na unafiki. Itakuwa wamemsaliti mwenyekiti wao.
Mimi nauliza tu nini kimewapata wana CCM hadi kuwa na huruma na wapinzani leo?
Kishada.