HURAAA! BoT MMEONYESHA NJIA. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

HURAAA! BoT MMEONYESHA NJIA.

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Tikerra, Sep 21, 2008.

 1. T

  Tikerra JF-Expert Member

  #1
  Sep 21, 2008
  Joined: Sep 3, 2008
  Messages: 1,704
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Huraa,BoT,mmeonyesha njia.Nitakalo kusema hata hivyo ni kwamba, tatizo hili haliko BoT tu,limezagaa nchi nzima.Na ni kubwa kiasi cha kutisha.Sasa serikali kwa makusudi kubisa itoe vihiyo wote walioko ndani ya serikali yenyewe, mashirika ya umma na binafsi.Kila cheti kihakikiwe upya, ni rahisi.Naamini kwamba utendaji mbovu uliokithiri katika serikali yetu na mashirika ya umma na binafsi, unaletwa kwa kiasi fulani na vihiyo hawa.Ninaamini pia kwamba ni rahisi zaidi kumhonga kihiyo kuliko msomi aliye bobea.Ni swala la 'mindset'.Mtu mwenye akili nzuri,si rahisi kuwa fisadi.Fisadi ni mtu mwenye matatizo ya akili.Amefirisika kiakili.Kwa hiyo tukitoa vihiyo tutapunguza ufisadi kwa kiasi fulani.
   
 2. K

  Kifuna JF-Expert Member

  #2
  Sep 21, 2008
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 426
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Nakubari Mwenye akili ni vigumu kuwa Fisadi.

  Lakini napata wasiwasi kidogo hasa kwa mtoto wa Mungai, Kipindi kile mtoto huyu alipokuwa akiajiliwa 2001, kama sijakosea nafikiri babayake alikuwa Waziri wa Elimu, je ndio alitumia ubazazi huo kumpa mwanae cheti cha ajabu?
  Sasa kama WAZIRI WA ELIMU ANAMPA MWANAE CHETI FEKI VIPI KWA MTOTO WA MKULIMA?

  ipo haja ya mawaziri wote kupitiwa vyeti vyao, tuone vikoje.
   
Loading...