Habari zenu wakuu! Happy new year to you all!
Suala lililonileta kwenu hapa ni kutaka kufahamu juu ya hili!
Nimeshuhudia baadhi ya wanawake wakiwa wembamba na wakiwa na miili yao mizuri tu ambayo si minene!
Sasa cha ajabu ni pale wanapokuwa wameshajifungua..! Wengi wao hufutuka na kunenepeana sana! Yani yale maumbo yao ya asili yanapotea kabisa na hata mivuto nayo inatoweka pia!
Hii pia hupelekea matiti kuwa makubwa kupitiliza..
Sasa wadau, najiuliza sana, tatizo hapa ni nini? Kwanini mwili uongezeke tuuu baada ya kujifungua?
Je, kuna mbinu gani mbadala ambazo zinatakiwa kuzingatiwa ili kurudisha mwili katika hali ya kawaida na uendelee kuwa romantic?
Msaada wenu wadau!
Wenu.... Excel!
Hicho kitu hakiepukiki, ni kama uzee hata ukiukwepa vipi utakukuta tu. Kwa ujumla Mwamamke anapojifungua antakiwa ale ashibe vizuri ili mtoto apate maziwa ya kutosha, hasa kama huna mpango wa kumpa mtoto maziwa ya kopo kwa umri mdogo.
Biologically mwanamke kujifungua anasababisha mabadiliko makubwa mwilini ambapo homoni aina aina huzaliwa ili kukabiliana na mabadiliko hayo...hii ni kanuni ya asili!
Njia za kukabiliana na ongezeko hilo ni pamoja na kuwa na displine ya vyakula baada ya kujifungua,mazoezi ya mwili,kubana tumbo kwa mkanda maalum...
Mkuu unaweza kukubaliana na mimi kwamba wanenepao ni wanawake wa mjini tuu?
hii nimeishuhudia maeneo mengi.. kwanini wanawake wa vijijini hawanenepi baada ya kujifungua?
kutokana na aina ya vyakula na muda wa mapumziko wanaoupata hawa kinamama..akina mama wengi wa vijijin huingia kwenye majukumu muda mfupi baada ya kujifungua ila mjini unawapata wana wasaidizi..mf. Housegirl n.k
hii kauli ina utata mkuu!
naomba tadhali unielezee zaidi kidogo!
Mzazi inatakiwa ale vya kutosha ili kupata maziwa kwa ajili ya mtoto,vyakula vizuri kwa mzazi ni mchemsho/mtori na makongoro hayo yanaleta maziwa sana kwahyo mtoto kwake ni burudani,vyakula hyvo in turn vinamnenepesha mzazi!!
ahsante mkuu kwa maelezo ya kina!
kwanini lakini wanawake wa mjini ndio huathirika zaidi na hili?
Acha nijinepee kwa raha zangu,vichwa vitatu si mchezo,hapa navaa size 16,wakati nipi binti ilikuwa size 8,ila inategemea na Genes,mbona wengine wana watoto lukuki ila ni vimbao mbao tu?
Mkuu kijijini hakuna tofauti na kambi za kijeshi, mwanamke kajifungua leo,kumpet pet ni siku ile tu atakapotoka zahanati ya kijiji alikoenda kujifungulia, na msaada pekee atakaopata ni kusaidiwa kichanga hadi nyumbani...ni mwendo wa ngondi!
Chakula ni uji wa ulezi na ndizi za kuchoma zilizonakshiwa kwa mafuta yaliyopatikana kutokana na maziwa ya ng'ombe! Huku shughuli kibao zikimwandama ataachaje kuwa unaoita 'romantic'!
Mjini ukute mke mwenyewe ni hawa walotoka kwenye familia bora,kisha kapata kaexposure ka kwenye kideo kupia hizi chereko,hajui hata kushika ufagio,maid wa kumfulia hadi gagulo,na happen kampata mume ATM aliyekuwa anasaka mtoto kwa udi na uvumba ataachage kuwa boflo wakati hata kuwasha luninga ni kazi ya 'dada wa kunyumba?'
Ngoja nianze uchunguzi.
mkuu umenena vyema haswaa!!
wanwake wa vijijini wana kazi kubwa sana.. kwa sababu wao hata mimba za miezi saba, bado wanaenda shamba na kufanya nyingine nzito za kifamilia..
sasa naomba unisaidie hili.. kwa jinsi hali ilivyo, ama kwa maoni yako.. je, hali ipi wewe unaiona ni njema kati ya hizi pande mbili, yaani tule wa kijijini na wa mjini!?
yani kiafya, je ni sahihi kumuacha mwanamke ajinenepee na kuwa kama mnyamapori? ama itafutwe njia mbadala ya kupunguza mafuta mwilini mwake pasi na kumdhuru mtoto??
ahsante.
mkuu umenena vyema haswaa!!
wanwake wa vijijini wana kazi kubwa sana.. kwa sababu wao hata mimba za miezi saba, bado wanaenda shamba na kufanya nyingine nzito za kifamilia..
sasa naomba unisaidie hili.. kwa jinsi hali ilivyo, ama kwa maoni yako.. je, hali ipi wewe unaiona ni njema kati ya hizi pande mbili, yaani tule wa kijijini na wa mjini!?
yani kiafya, je ni sahihi kumuacha mwanamke ajinenepee na kuwa kama mnyamapori? ama itafutwe njia mbadala ya kupunguza mafuta mwilini mwake pasi na kumdhuru mtoto??
ahsante.