Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 34,071
- 79,437
Hamjambo!
Kwanza nimpongeze kwa hatua kubwa, ya kijasiri, yenye kuaibisha, kudharau, kudogodesha mambo yote yanayoendana na kinyume cha HAKI na KWELI.
Jambo kubwa ambalo Humphrey amelifanya katika barua yake ni kumkabili moja kwa Moja mwajiri wake, yaani Rais.
Kwamba, matendo ya Rais ndio yamemfanya Humphrey ajiuzulu. Hasa kupitishwa kiholela, kimazabe pasipo kufuata kanuni na Sheria za chama na kuwanyima wanaccm wengine fursa ya kugombea nafasi ya urais kwa Mwaka huu.
Historia itamkumbuka Humphrey Polepole kwa kukataa ulaji, uheshimiwa, na kumkaanga Boss wake bila kumuangalia usoni.
Angekuwa mtu mwingine, wala asingejishughulisha.
Maana rais aliyeko madarakani ndiye kampa ajira ya ubalozi, hivyo kuitisha uchaguzi CCM ingeweza kuhatarisha maslahi ya balozi.
Watibeli tunampongeza Humphrey kwa ujasiri huo.
Tunahitaji watu ambao wataitetea HAKI hata kama ni haki za mahasimu wao.
Haki katika taifa letu ni usalama kwa nchi.
Uadilifu, maadili.
Bado hatujasahau waliotekwa, waliouawa, na waliopotea kwa mazingira ya matendo ya ukosoaji wa serikali.
Tunahitaji viongozi wanaothamini maisha ya wengine. Maisha ya watoto wa wengine.
Wanaoheshimu utu.
Wanaoheshimu sheria lakini Sheria za Haki.
Hatupo kwaajili ya kikundi au mtu Fulani.
Hatupo kwaajili ya chama Fulani.
Tupo kwaajili ya watu wote na makundi yote ya watanzania.
Tupo kwaajili ya vyama vyote.
Wanachadema wasiwaonee wanaccm
Na wanaccm wasiwaonee wanachadema.
Wote tuwe chini ya sheria.
Tupo kwaajili ya Nchi.
Tupo kwaajili ya urithi wa watoto wa nchi hii watakaokuja baada yetu.
Hongera Sana Humphrey!