mwankuga
JF-Expert Member
- Aug 30, 2010
- 334
- 120
HAMPHREY POLEPOLE: IBILISI WA MTU NI MTU MWENYEWE
Historia ni mwalimu mzuri sana. Kuna mambo mengi sana tumejifunza kutokana na historia. Nikisoma historia ya harakati za uhuru wa Tanganyika na Afrika huwa napata msisimko usioelezeka. Lakini kwa upande mwingine roho inauma hasa katika kipindi hiki cha soko holela.
Wakati wa harakati za kutafuta uhuru wa kisasa vijana wengi walikuwa mstari wa mbele katika harakati hizo. Kulikuwa na akina Julius Nyerere, Oscar Kambona, Zuberi Mtemvu Mwinshehe n.k. Katika umri wao mdogo, walijitwisha majukumu magumu ambayo yaliwaletea matatizo.
Wajilitolea kwa kiwango cha juu sana, kiasi kwamba wakaacha kazi serikalini na kuamua kufanya siasa ambazo hazikuwa na masilahi kama leo hii. Huu ni uzalendo uliotukuka sana.
Jambo la kufurahisha sana nimeliona kwa Dr. Salim Ahmed Salim. Katika umri wa miaka 22 tu, Dr. Salim akapewa majukumu ya ubalozi. Kwa hali tuliyonayo sasa, inawezekana isiwe rahisi sana kupata dhamana kama hiyo. Tukumbuke kwamba Dr. Salim ndiye Katibu Mkuu wa OAU kukaa muda mrefu (1989 – 2001).
Aidha Dr. Salim alikaribia kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa mwaka 1981 kama isingekuwa fitina za mataifa makubwa yenye ushawishi kwenye umoja huo. Dr. Salim ana sifa zilizotukuka sana, hasa nje ya Tanzania. Kwa maoni yangu, naona kama Dr. Salim ni rais ambaye hajawahi kuwa rais wa nchi hii.
Mtakumbuka wakati wa uchaguzi mkuu mwaka 2005, kama isingekuwa figisu za wana mtandao, inawezekana leo hii tungekuwa tunamzungumzia Dr. Salim kama rais Mstaafu.
Lengo la Makala hii fupi ni kuzungumzia nafasi ya vijana katika kuleta maendeleo katika nchi yetu na pengine Afrika nzima. Viongozi niliowataja walitoa mchango wao katika nchi wakiwa na umri mdogo (vijana). Natambua kwamba wapo vijana wengi wanaotoa mchango mkubwa katika nchi hii katika nyanja mbalimbali.
Kwa leo napenda kumulika jinsi vijana walioko kwenye siasa na nini wanakifanya kuinufaisha nchi. Tuna vijana wengi kutoka kwenye chama tawala na vyama vya upinzani. Kuna akina Zitto Kabwe, John Mnyika, Godbless Lema, Halima Mdee, Joshua Nasari, Mwigulu Nchemba, January Makamba, Nape Nnauye, n.k. Kama tutatumia nadharia ya ulinganifu, tutaona kuna tatizo kwa sasa tofauti na zamani. Sababu zipo nyingi sana (ambayo inaweza kuwa mada tofauti).
Kwa kuzingatia hayo juu, ningependa kumzungumzia ndugu yangu Hamphrey Polepole, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM akichukua nafasi ya Nape Nnauye. Nimekuwa nikimfuatilia Polepole kwa muda mrefu sana. Kuna wakati nilikuwa nafarijika sana kuona kijana kama Polepole anazungumza mambo yenye masilahi kwa Taifa kwa umahiri mkubwa sana.
Vuguvugu la pili la mabadiliko ya katiba ndilo lililomuibua Polepole kiasi kwamba akajulikana Tanzania nzima. Nimepata kuhudhuria mihadhara ambayo Polepole alikuwa miongoni mwa wasemaji wakuu. Polepole alivutia sana vijana. Alikuwa anazungumza mambo kwa ufasaha sana na kujenga hoja kwa umahiri mkubwa. Alikuwa mjumbe wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba. Hata baada Tume kukabidhi rasimu ya katiba , aliendelea kusimama kidete na kutetea maoni ya wananchi.
Lakini wakati sio rafiki yetu. Mambo yanaenda haraka sana. Leo hii tuna akina Polepole wawili. Polepole wa vuguvugu la uandikwaji wa katiba mpya na Polepole msemaji wa Chama cha Mapinduzi. Ukimwangalia Polepole wa zamani, utaona kwamba alikuwa na sura ang’avu, kichwa kilichotulia na sauti ya polepole yenye kushawishi.
Kila neno lililomtoka likawa na matumaini kwa kesho ya vijana na Taifa kwa ujumla. Kwa kuwa ukweli unajieleza wenyewe, kila neno alilokuwa anatoa lilikuwa linasimama lenyewe. Hakukuhitaji maelezo ya ufafanuzi au utetezi. Ukweli hujisimamia wenyewe. Polepole aling’ara hasa. Alivutia kumtazama. Vyombo vya habari vikaweka makazi kwake.
Polepole wa pili, amepauka na kunyauka. Polepole huyu anatumia nguvu sana kujenga hoja, badala ya nguvu ya hoja kujisimamia yenyewe. Kila akizungumza, maneno yake hayapenyi kwa urahisi kwenye masikio ya msikilizaji. Ili kumwelewa ni lazima ulazimishe kuelewa. Sauti yake ni dhaifu. Sura yake haiendani na kile anachokizungumza. Ni kama amevamiwa na “pepo” ambalo limeny’anganya au kukamata ubongo wake. Linamwekea maneno. Ni kama vile ametekwa na watu wasiojulikana.
Polepole anaonekana amechoka na ana haraka sana. Sijui kimempata kitu gani huyu rafiki yangu. Kila nikimtazama naumia moyoni. Kuna mwanazuoni mmoja anasema, “Kifo sio tatizo, tatizo pekee ni pale tunapoacha mambo tuliyonayo kwenye mioyo yetu kufa”. Namwona Polepole kama mtu aliyekataa tamaa, mwenye msongo wa mawazo na mtu mwenye haraka sana.
Polepole wa sasa anaonekana ni mtu mwenye mzaha na aliyeamua kuwa “mchekeshaji”. Ni kama viatu alivyovaa havimuenei, na analazimisha vienee. Sielewi kwa usahihi kama cheo alichonacho kwenye chama, kinahitaji useme mambo ya ubeuzi.
Nimemzungumzia Polepole kwa sababu nampenda. Ni kijana mwenzangu. Akifanikiwa yeye, tumefanikiwa vijana wengi. Akiaminiwa yeye, basi vijana tutaaminiwa. Katika vitu ninavyompongeza Rais wangu JPM ni kuwapa nafasi za maamuzi vijana wengi.
Ni jukumu la vijana hao kutumia vizuri nafasi walizopewa kwa manufaa ya vijana na watanzania wote. Sina ubaya na Polepole. Aidha natambua kwamba ile nafasi aliyonayo ni kazi ya mshahara. Na vijana lazima tufanye kazi kwa masilahi ya familia zetu na Taifa kwa ujumla.
Lazima tuwe makini katika harakati zetu, maana kuna maisha yanaendelea. Tunayoyasema na kuyatenda leo yana hukumu kesho. Kwa kuwa umri unaruhusu, lolote linaweza kutokea mbeleni. Siku ukisimama mbele za watanzania ukihitaji chochote kutoka kwao, watachukua na kupekua faili lako. Bahati nzuri sana tuko kwenye ulimwengu wa teknolojia. Kila ulichokisema kitawekwa wazi. Kuna mtu amewahi kusema katika maisha mwogope sana Mungu na Teknolojia.
Polepole ni kijana, ana muda mrefu wa kufanya siasa. Atathimini mwenendo wake na maneno anayoyasema kama inaweza ikawa dhamana kwa maisha yake na faida kwa Taifa. Kuwa msemaji wa taasisi kama chama cha siasa haina maana kwamba useme chochote kinachokujia kichwani.
Tutofautishe usemaji wa Masau Bwire na Ruvu Shooting yake, na usemaji wa taasisi ambayo inagusa masilahi mapana ya Taifa. Ujana una mwisho wake. Lakini pia tutambua kwamba ujana pekee bila kuwa na mawazo ya kiujana ni bure. Tutumie ujana wetu kwa kusaidia maendeleo ya Taifa letu. Ibilisi wa mtu ni mtu mwenyewe.