Humphrey Polepole: Bandari ya Bagamoyo sio muhimu kuliko Bandari ya Dar na Tanga

troiker

JF-Expert Member
Aug 18, 2019
1,429
2,262
Akihojiwa katika kipindi cha ajenda na Mtangazaji Mtozi Nyanda amesema bandari ya Bagamoyo si muhimu kuliko bandari ya Dar na Tanga.

Kazungumzia katiba mpya na kasema haipingi usipokuwa kuna maangalizo matatu kayatoa yazingatiwe kabla ya kuiandika katiba mpya.

Pia ametumia tahadhali sana katika uwasilishaji wa maoni yake kuhusu bwawa la umeme la JNHP, amesema ni lazima likamilike.

Kagusia kuhusu kukosekana kwa crane ya kubeba milango ili bwawa lijazwe maji ni kwamba kwa mradi huo crane ni Minor things,pesa iliyowekezwa ni nyingi sana crane sio issue kabisa.

Kasema japo si moja kwa moja, yakwamba kuna wahuni wanashirikiana na mabeneru kuhujumu mradi huo,kwani mradi huo ulipingwa kwa nguvu nyingi sana mwanzoni mwa mchakato wake
 
03 December 2021

THE BIG AGENDA : EXCLUSIVE INTERVIEW NA HUMPHREY HERSON POLEPOLE


Humphrey Polepole is a Tanzanian politician, a former Chama Cha Mapinduzi's Ideology and Publicity Secretary and currently serving as nominated Member of Parliament
  • Orodha ya wahuni walioshughulikiwa
  • Udhaifu, Awamu ya 5 imeshindwa kumaliza wahuni
  • Katazo la mikutano ya shughuli za siasa kwa wapinzani, awamu ya 5 hadi sasa awamu 6 ya uongozi
  • Desturi, amri, kanuni, tamko, miongozo kukataza shughuli za siasa ni sheria au katiba
  • Ushindi wa kishindo wa CCM ktk uchaguzi mkuu mwezi October 2020
  • Ilani ya CCM kuhusu bandari mbalimbali
  • Mpango Mkuu / Grand Plan
  • Reli ya SGR na matawi yake
  • Reli toka bandari ya Tanga, Moshi mpaka bandari ya Musoma
  • Ujenzi wa Bwawa la Umeme JNHPP Stiegler's gorge Rufiji
  • Mabeberu ni kina nani
  • Communication psychology ya Humphrey Polepole
  • Nitasema kweli daima fitna kwangu mwiko - Humphrey Polepole
  • Umuhimu wa Wakulima ktk ilani ya CCM, je upo kivitendo mfano ukulima na mbolea ghali sana
  • N.k n.k
Source : Star TV Habari
 
Akihojiwa katika kipindi cha ajenda na Mtangazaji Mtozi Nyanda amesema bandari ya Bagamoyo si muhimu kuliko bandari ya Dar na Tanga.
Pia kazungumzia katiba mpya na kasema haipingi usipokuwa kuna maangalizo matatu kayatoa yazingatiwe kabla ya kuiandika katiba mpya
Ametumia tahadhali sana katika uwasilishaji wa maoni yake
Jamaa Leo ndio nmegundua ana kitu ambacho kinaweza nufaisha Taifa, kama atapewa Nafasi.

Nimependa anavyojiamin, kutetea anachokiamini.
 
Akihojiwa katika kipindi cha ajenda na Mtangazaji Mtozi Nyanda amesema bandari ya Bagamoyo si muhimu kuliko bandari ya Dar na Tanga.
Pia kazungumzia katiba mpya na kasema haipingi usipokuwa kuna maangalizo matatu kayatoa yazingatiwe kabla ya kuiandika katiba mpya
Ametumia tahadhali sana katika uwasilishaji wa maoni yake
Swala la Bandari amaliweka vizuri sana.

Ile Bandari bana, tunakuwa kama watoto. Kwanini tujenge bandari nyingine pua na mdomo na bandari ya DSM? Kwanini hizo nguvu zisitumike kuendeleza bandari za Tanga na Mtwara?
 
Cha kubanga bhana..

wakat wake ulisha pita.... hapo mama achague moja.. ama kumpoteza kabisa kisiasa.

ama kumpa cheo kikubwa zaidi.
Akili mbovu hushambulia mtu zaidi kuliko kushindanisha hoja.
Ili kauli ya Polepole ikose tija, njooni na kauli nyingine inayoonyesha ni namna gani bandari ya Bagamoyo itakuwa na tija kwa taifa ili tuwaelewe..
 
Swala la Bandari amaliweka vizuri sana. Ile Bandari bana, tunakuwa kama watoto. Kwanini tujenge bandari nyingine pua na mdomo na bandari ya DSM? Kwanini hizo nguvu zisitumike kuendeleza bandari za Tanga na Mtwara?
Labda kama Bandari ya Dar es Salaam ina potential ya kujengwa kwa kiwango cha megaport otherwise hamjui mkisemacho. Strategic location ya Dar au Bagamoyo huwezi ilinganisha na Tanga au Mtwara.
 
Naungana na Magu kuweka pembeni mradi wa Bagamoyo. Wabunge hawajui in/out wapowapo tu wala hawauchambui. Pamoja na mapungufu ya Pole2 hakika mradi wa Bagamoyo tutaingia mkenge wa maisha kwa bunge hili lisilohoji mikataba.
Mbaya zaidi spika Ndugai nae alikwisha ramba zake kibindoni,unategemea nini hapo?
 
Back
Top Bottom