Well Nyani Ngabu, let me highlight some of the queries which you have raised in your comment as follows;
quoting the words of the late Mwalimu Julius Kambarage Nyerere with the title words "RUKSA ARDHI KUUZWA KAMA KANZU!!", alisema,
"Katika nchi kama yetu, ambamo waafrika ni masikini na wageni ni matajiri, kuna uwezekano mkubwa kwamba Mwafrika akiruhusiwa kuiuza ardhi, katika miaka themanini ijayo, ardhi yote ya Tanganyika itamilikiwa na matajiri wageni na wenyeji watakuwa watwana. Lakini hata kama wageni wasingekuwa matajari litaibuka tabaka la watanganyika matajiri na wajanja. Tukiruhusu ardhi iuzwe kama kanzu, katika muda mchache, kutakuwa na kundi dogo la waafrika wakiwa na ardhi na walio wengi watakuwa watwana" Mwl. Julius K.Nyerere, 1958
Hayo yalikuwa mawazo na muono wa Mwalimu mwaka 1958, mwaka 1999 Watanzania tukapata sheria zetu za ardhi ambazo kimuundo zilitungwa kufanana kwa kiasi kikubwa na ile ya Uingereza. Sasa hebu tuangalie mapungufu yaliyopo katika Land Act 1999 ambayo yanatoa nafasi kwa wageni kumiliki ardhi, kifungu cha ishirini kifungu kidogo cha kwanza kinaeleza ni marufuku iliyowekwa kwa wageni kumiliki ardhi isipokuwa kwa ajili ya uwekezaji au makazi ya wafanyakazi wa mradi wa uwekezaji , naomba nikinukuu, "For avoidance of doubt, a non-citizen shall not be allocated or granted land unless it is for investment purposes under the Tanzania Investment Act"
Lakini sheria hiyo hiyo imetoa nafasi kwa wageni kupewa Hatimiliki (Right of Occupancy) badala ya Hatimiliki hafifu(Derivative right) kama ilivyoelezwa katika sheria, vifungu vinavyotoa nafasi kwa wageni kupewa hiyo Hatimiliki( Right of Occupancy) ni kama vifuatavyo, naomba kunukuu
Section 19(2) "A person or a group of persons, whether formed into a corporate body under the Companies Act *(21) or otherwise who is or are non-citizens, including a corporate body the majority of whose shareholders or owners are non-citizens, may only obtain a
right of
occupancy or derivative right for purposes of investment prescribed under the Tanzania Investment Act
Section 25 Procedure for application for right of occupancy
(1) An application for a right of occupancy shall be–
(h)if made by a non-citizen or foreign company, accompanied by a Certificate of Approval granted by the Tanzania Investment Centre under the Tanzania Investment Act *(26) and any other documentation which may be prescribed by that Act or any other law
MWISHO WA KUNUKUU
Sasa wanaotakiwa wafanye marekebisho haya ya sheria sio kwamba hawajui kama yapo ila wameyaacha na wanatumia upungufu huu wa sheria kugawa ardhi kwa wageni wanaokujua kwa kigezo cha uwekezaji. Ardhi ni moja ya rasilimali muhimu sana ambazo tusipokuwa makini Watanzania tutashindwa kuwa na ardhi yetu maana itaishia mikononi mwa wageni wenye fedha,swali la kujiuliza je, ni ruksa ardhi kuuzwa kama kanzu?