Hukumu ya Lissu - Jisomee mwenyewe | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hukumu ya Lissu - Jisomee mwenyewe

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Isango, Apr 27, 2012.

 1. I

  Isango R I P

  #1
  Apr 27, 2012
  Joined: Jul 23, 2008
  Messages: 295
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Leo ni siku ya hukumu, ni kesi ya uchaguzi, inatokana na uchaguzi uliofanyika tarehe 31/10/2010, waombaji ni Shabani selema, na Paskali Halu. Walileta mashahidi 24, na vielelezo saba, wanawakilishwa na Wasonga. Kimsingi wanapinga uteuzi wa Lissu kuwa mbunge wa Jimbo la Singida mashariki, wakidai kuwa kulikuwa na ukiukwaji wa sheria za uchaguzi. Wakidai kuwa kulikuwa na dosari zilizofanya uchaguzi usiwe huru na haki, hivyo kumfanya Mgombea wao wa CCM asishinde.

  Walalamikiwa, mlalamikiwa wa kwanza walisema kuwa yeye hakuwemo, au hakuwa mshirika wa tuhuma zilizofanywa. Walalamikiwa wote pamoja wanasema hakuna kitu cha msingi kinachoweza kuifanya mahakama itengue matokeo.

  Haibishaniwi kuwa mgombea alishinda kupitia CHADEMA, kupitia jimbo la singida mashariki, na kumshinda mgombea wa CCM Bw. Njau ambaye alipata nafasi ya pili. Tofauti ya Kura kati ya Lissu na Njau ilikuwa kura 1626.

  Mlalamikiwa wa pili, anaunganishwa katika kesi kama necessary paty, kwa kuwa mlalamikiwa wa pili ni Msimamizi wa uchaguzi.

  Hoja katika kesi zilikuwa 11.

  Hoja ya kwanza, Lissu anadaiwa kuandaa barua zilizotolewa na vyama vingine vikidai kupeleka majina ya mawakala,

  Hoja ya pili, ilidaiwa kuwa Lissu alikuwa na Mawakala 1240,

  Ni kama Lissu alikuwa na mawakala 620, ndani na nje ya vituo

  Kama Lissu alitoa rushwa kwa mawakala nje ya Chama cha CCM, Kwa kuwapa chakula, usafiri katika vituo vyote? Na kama jibu ni ndiyo, je hayo yalifanyika yeye akijua, au

  Ni kama Wakala alichukua kitabu na kuhakiki majina ya wapiga kura badala ya afisa mhusika, hivyo kucchukua mamlaka ya msimamizi.

  Ni kama Maaskari polisi katika baadhi ya vituo, waliacha kazi zao na kuanza kukampeni kwa ajili ya Lissu.

  Ni Kama Lissu alitoa usafiri kwa baadhi ya wapiga kura kwa gari yake, toka Taru kwenda Mang'onyi

  Ni kama Msimamizi wa uchaguzi alibadilisha matokeo ya uchaguzi katika kituo cha Ikungi na kupeleka taarifa tofauti

  Ni kama Mgombea wa CCM alikataaa kusaini matokeo ya uchaguzi wa jimbo la singida mashariki kwa kuwa uchaguzi haukuwa huru na wa haki

  Ni kama vitendo vilivyotajwa viliathiri matokeo ya cuahguzi katika JImbo la Singida mashariki.

  Ni wahusika wana haki gani mbele ya mahakama.

  Kimsingi, Hoja ya kwanza nay a pili zinafanana, zinahusu mawakala.

  Hoja ya kwanza, inadaiwa kuwa Lissu aliandaa barua, kwa ajili ya vyama vingine na kuzipeleka kwa msimamizi. Mashahidi walioitwa kuitwa kuthibitisha hoja hii, walikuwa wengi, shahidi wa kwanza na wa pili, hawakuongelea juu ya barua hizo, wote walikana na kusema kuwa Lissu hakuandika barua hizo isipokuwa ziliandikwa na makatibu wa vyama husika. Shahidi wa kumi alizungumzia juu ya ufanano wa barua hizo, yaani zinatoka katika chanzo kimoja. Walisema Lissu aliandaa, lakini alipohojiwa walisema zimeandikwa na makatibu. John Madidilo, shahidi wa 19, anasema barua ya TLP iliandikwa na katibu wa Chama chao, alikiri kuwa barua ilikuwa na mhuri na wa Chama. Shahidi wa 22, alipohojiwa, Bw. Huseim Mwangia, alisema barua hizo ni tofauti. Haibishaniwi kuwa barua hizo zinafanana, juu ya suala la anwani japo zilisainis

  Chadema walipeleka 24/10/2010, CUF 24/10/2010, CCM 18/10/2010 kwa ajili ya kupeleka majina ya mawakala. Haya yote yaliyozungumzwa yalilinganishwa na barua ya Chadema. Waliosaini barua hizo ni makatibu wa Vyama husika, na haibishaniwi kuwa Vyama vyao vilishiriki katika Uchaguzi, na vilikuwa na wagombea.

  Mashahidi wa waombaji wanakiri kimsingi, kuwa kila chama kilikuwa na haki ya kuweka mawakala.

  Suala la Msingi hapa ilikuwa kama Lissu aliandaa barua hizo. Barua hizo ziliandaliwa kwa mujibu wa sheria ya uchaguzi inayokitaka kila chama kinachoshiriki uchaguzi, kupeleka majina ya mawakala sio zaidi ya siku saba kabala ya uchguzi kuwajulisha kwa maandishi, majina mawakala na vituo vyao. Hoja inakuja kwamba, kifungu hiki, hakisemi wale wanaogombea wapeleke majina ya wagombea wa Vyama vingine. Kufuatana na ushashidi uliotolewa na Lissu, barua ya CDM iliandikwa na kwa ushauri wake, lakini alikana kujua uandishi wa Vyama vingine kwani havikuandikwa kwa ushauri wake. Lissu alisema kuwa barua hizo zinafanana na akasema yawezekana kuwa zilitoka ndani ya Printa Moja, na shahidi wa tatu alikiri suala hilo.

  Wasonga alisema, hizi ni njia zilizotumika kusaidia kosa. Shahidi wa kumi wa waleta maombi alisema kuwa Shahidi alisema kamati ya maadili haikukaa kutatua mgogoro huo. Na kusema ingawa barua ziliandaliwa na Lissu japo hakuzisaini. Shahidi wa 19, toka TLP, alionyesha kilichomfanya awe na hofu kwa kuwa barua ya TLP, aligundua zinafanana na ya CDM. Na shahidi wa 23, alisema zinafnana kwa kuziangalia kwa macho, ingawa alisema kuwa hazijui nani aliziandaa.

  Lissu katika utetezi wa barua, alikiri kuandaa barua ya CDM na kuwa alishirikiana na Vyama vya Upinzani, na kuwa alimshauri shahidi wa 3, namna ya kuandika barua. Walalamikaji walijiuliza kwanini barua hizo ziliandikwa katika stationary moja, na Wakili wa walalamikaji anauliza, Lissu alijuaje hayo kama hakuandaaa barua hizo zikiwemo za vyama vingine? Na kwanini barua zingine ziwe na tarehe inayofanana? Walalamikaji wanatilia shaka kuwa barua hizo ziliandikwa na Mlalamikiwa wa Kwanza, Lissu.

  Mlalamikiwa wa kwanza, Lissu, na Mlalamikiwa wa Pili, Msimimamizi wa uchaguzi, wamesema kimsingi wameshindwa kuthibitisha madai yaliyoletwa. Vielelezo vya maandishi vilivyoletwa na walalamikaji havionyeshi kuandaliwa na Lissu bali na makatibu wa vyama vya husika. Shahidi wa kwanza, hakugusia kabisa kuhusu barua hizo, na shahidi wa walalamikaji alisema kuwa vyama vyote vilifuata utaratibu. Hata shashidi wa Pili wa walalamikaje, marcel halu naye hakuzungumzia, na wala hakuona wakati barua hizo zikiwa zinaandikwa wala kuzikabidhi kwa msimamizi. Shahdi wa 10, katibu wa CCM naye alisema hajui na hawezi kuthibitisha kama barua hizo ziliandikwa na Lissu. Japo alisema box 261, ni la CHADEMA, shahidi mwingine aliyekuja yaaani postermaster alisema kuwa CDM hawatumii box hilo. Shahidi wa 19, alikiri barua kuwa ni ya kiongozi wa ofisi yao na ilikuwa na saini ya katibu wao, na kwamba aliyefanya uteuzi wa mawakala ni Mwenyekiti wa wilaya. Hivyo hoja ya kwanza ilikosa maana.

  Nani aliandaa, na kwamba kuna shaka kama Lissu kweli aliziandaa, au kama walipewa ushauri na viongozi wa CHADEMA. Mlalamikaji alilalamikia kusema kuhusu maandalizi, lakini sisi wasomi wa sheria tunafafanua kuwa maandalizi sio kitendo, kitendo na kudhamiria kutenda ni vitu tofauti. Wakili wa walalamikaji katika hili alipotoka. Tunachukua neno kutoka Oxford Dictionary, kuangalia neno "prepare" which means to make something ready or to do something. Yaani kufanya kitu Fulani kiwe tayari kutumika. Hii ndio ilikuwa maana iliyokusudiwa na waleta malalamiko. Maana waliyochukua ilikuwa na kasoro. Vitendo vinavyodaiwa kuandaliwa vinaenda beyond preparation. Je walithibitisha kuwa Lissu ndo alifanya hayo? Na Kama alifanya hivyo je iliathiri matokeo? Nimekazia maneno hayo kwa kuwa walalamikaji walikuwa wanadisprove barua zao, badala ya kuprove kesi yao. Hakuna hata barua moja iliyokuwa na saini ya Lissu. Na maswali yote waliyoleta barua ya CDM ilisainiwa na Shaban Limu, na Masuala yote waliyoleta yapo katika suspicion ambayo wao walipaswa kuthibitisha. Hakuna shahidi hata moja aliyethibitisha kusema kumwona Lissu akishiriki kufanya hayo. Waliosaini hizo barua walikuwa ni mashahidi muhimu, na kisheria walalamikaji walipaswa kuwaleta wale walioandika, na sio kumrushia Lissu Mzigo huo. Kuna shahidi wa 7, na wa 19, aliongelea hisia, lakini kwenye barua yao ya TLP anasema, ´mheshimiwa katibu Mkuu ukweli atautoa aliyepanga mawakala hao, yaani Mwenyekiti wa TLP wa Singida. Kwa kuangalia barua hiyo shahidi muhimu alikuwa Mwenyekiti wa TLP wa wilaya Singida, na mahakama haijaambiwa kwanini huyo hakuitwa. Mahakama inasema kuwa pengine walalamikaji kwa kumruka shahidi muhimu pengine angeharibu kesi yao. Walalamikaji walipaswa kuprove case yao beyond reasonable doubt.

  Uthibitishwaji wa kesi, ni jukumu la aliyeleta uchaguzi. Lazima uthibitishe bila kuacha shaka. Shaka ni vigumu kuifafanua katika hali ya kawaida ya utendaji wa kazi, lakini uthibitishaji huo unategemea naukubwa wa tuhuma hizo. Kifungu cha 112, cha sheria ya ushahidi, inasema, anayelalamikia jambo lazima athibitishe yeye. Uthibitishaji wa kesi ya uchaguzi, lazima uiridhishe mahakama kuu, ili Yule aliyechaguliwa kuwa mbunge. Hakuna kesi za madai zilizowahi kupatikana kwa sababu ya kufafana kwa barua. Waombaji hawakuleta uthibitisho kusema kuwa barua hizo zimechapwa na Computer ya Lissu. Hakuna ushahidi unaomhusisha Lissu moja kwa moja katika hili. Kufanana peke yake kwa barua za Vyama, haitoshi kuifanya mahakama iamini kuwa Lissu aliandaa. Hata kama wanaunganisha na ushauri aliotoa, kasoro hiyo kulingana na kifungu cha 48, ikisomwa pamoja na 57 haiwezi kuwa sababu ya kuifanya mahakama itengue uchaguzi. Kwa sababu nilizozitaja hapo, issue namba moja haikuthibitishwa kiasi cha kuiridhisha mahakama.

  Hoja ya Pili, inafanana nay a kwanza. Inayozungumzia idadi ya mawakala. Kwa kuwa hoja ya kwanza haikuthibitishwa, nayo ya pili inayozungumzia idadi ya mawakala, hiyo nao haina mashiko.

  Hoja ya tatu; kwamba kulikuwa na vituo 124, Lissu anadaiwa kuwa na mawakala wawili wawili kila kituo. Mashahidi walioitwa kusemea hayo, baadhi yao walikana. Semina ambazo Lisu baadhi ya washiriki walitoka vyama vingine kikiwemo CCM. Wale waliokuwa CHADEMA waliosimamia uchaguzi kwa vyama vingine tofauti na CCM, ni shahidi wa 9 na 12. Wengine walikuwa mashahidi na mawakala wa CCM, NA wanachama wa CCM, lakini walitoa ushahidi kwa kutumia maneno waliyosikia kwenye sherehe wakati Lissu anawashukuru wapiga kura. Shahidi wa 3 alikana kuwa hakukuwa na idadi hiyo ya mawakala.

  Shahidi 11, na 18 walisema kuwa wao walikuwa ni mawakala wa CUF na APPT maendeleo,walisema kuwa walisimama kwa vyama hivyo japo walikuwa ni wanachama wa CHADEMA.Shahidi wa 9, anasema wakati wa Semina, waliambiwa juu ya umuhimu wa fomu namba 14, na kwamba hakukuwa na wizi wa kura na vitu kama hivyo. Hata katika mafunzo hayo walikuwepo wa CCM. Hakuna hata shahidi mmoja kati ya hao aliyejaza fomu ya malalamiko inayotakiwa kisheria. Wakili wa walalamikaji alisema, kulikuwa na uwezekano wa kuwepo kwa mawakala 5 ndani na nje ya kila kituo.

  Lissu alisema, kwa vile, hoja ya tatu inategemea hoja ya kwanza nay a pili, ithibitike kuwa hata hoja hii haikuwa na mashiko. Lakini hata yeye anasema, kati ya vituo 124, vya kupigia kura, ni vituo 7 tu ndio walileta ushahidi. Hivyo hakukuwa na ushahidi uliothibitisha kuwa kulikuwa na mawakala 620, nje na ndani. Ilikuwa kazi ya waleta maombi kuthibitisha hayo. Mwisho kabisa Lissu ameshauri kuwa kitu pekee kinachoweza kuthibitisha nani alikuwa wakala ni hati ya kiapo cha kutunza siri. Hicho ndo kinaonyesha nani alipaswa kuwepo. Hivyo hoja ya tatu haikuthibitishwa. Waombaji wameleta vitu vya kufikirika tu. Hivyo vielelezo hivyo haviwezi kuthibitisha kujibu hoja ya tatu.

  Hata hivyo Shahidi 10, aliyeandika kulalamika kusema kuwa Lissu alikuwa ana mpango wa kuweka mawakala 2 ndani ya kituo, na 3 nje ya kituo. Lakini hakuna hata mpiga kura hata mmoja aliyeleta lalamiko kwa suala hili. Majaji wenzangu wamewahi kusema kuwa tuhuma ambazo hazijathibitishwa zinachukuliwa kwa wepesi. Kesi husika ni Silvesta masinde na Pius Msekwa, inasema "labda kama Yule aliyeshindwa kuandika zile fomu katika kituo aeleze sababu, vinginevyo tutapima ukweli anousema ni kiasi gani. Tukienda kwa mfano, shahidi wa 1, alisema Chadema walikuwa na mawakala wengi, na kwamba walikuwa na mawakala 5, nje na 5 ndani, pia shahidi 20 na 21. Ukiangalia kwa ujumla wake ushahidi huuu ulikuwa unachanganya. Kielelezo namba 5 cha barua ya CCM inazungumzia 2 ndani na 3 nje, au shahidi wa 1, 20 na 21 waliosema 5 ndani na 5 nje. Nakubaliana na walalamikaji kuwa haikuwa busara kuleta mashahidi toka vituo vyote. Pili kushindwa kujaza fomu ya malalamiko hakumfanyi ashindwe kuleta ushahidi. Lakini hayo yanaleta uzito mdogo. Hata hivyo shahidi wa 8, aliyejaza fomu ya malalamiko na kuichana baada ya kugundua kuwa CCM walishinda katika kituo chake. Pia shahidi namba 5, alisema hati yake ya malalamiko ilichukuliwa na msimamizi, hata hivyo walalamikaji walishindwa kuileta hata copy baada ya kukosa origina.. Ushahidi wa 10 ni katibu wa CCM alijikita mno katika hisia za kisiasa, alikuwa na ushabiki wa kisiasa. Alisahau hata barua yake aliyoandika. Alichoandika na alichosema vilikuwa tofauti, na vilitawaliwa zaidi na hisia, ushahidi wake ulikuwa wa hisia za CCM zaidi.

  Shahidi mwingine aliyesema kuwa alijaza fomu ya malalamiko, eti hakukuwa na fomu ya kiapo isipokuwa CCM, lakini hati ya kiapo hakiwa ushahidi pekee wa kuthibitisha kuwa Fulani alikuwa wakala au la. Walalamikaji hawakuongelea sana ushahidi wa shahidi namba 4. Huyu Ally Mkhandi, alisema kuwa aliona mawakala wa CCM, CHADEMA TLP, APPT MAENDELEO Na CUF, ushahidi wake ulitupitia mbali malalamiko kuwa wote walikuwa mawakala wa Lissu. Shahidi wa 9, alikataa kuwa walikuwa na wamakala 5 ndani na nje ya kituo, japo walikuwa ni mashahidi wao.

  Wakili wa walalamikaji, aliomba shahidi ambaye yeye alisema ni Golden Witness, aliyesema walikuwa na mawakala 5 ndani na 5 nje, na kwamba alimsaidia mtu mmoja ambaye alikuwa hajui kusoma na kuandika. Shahidi hakutaja jina la mtu aliyemsaidia, japo walitoka katika kijiji kimoja. Hoja nyingi ambazo wakili wa walalamikaji alisema, zingine zilishatupiliwa mbali tangu mwanzo wa kesi.

  Shahidi wa 11, alisema kuwa kulikuwa na wizi wa kura. Wale mashahidi ambao walibadili uhalisia. Mashahidi walionekana kuwa ni wa CDM, na walikuwa wapenzi wa Lissu, lakini baadaye walimgeuka. Hawa ni turn court witness, ni kama kiti kinachozunguka, hakina msimamo. Haikujulikana ni kwa nini hawa waliokuwa wafuasi waaminifu wa Lissu waliamua kuanza kumgeuka.

  Tunashindwa kuelewa jinsi gani kunapotokea hasa watu wanapohama katika vyama, na hasa inapojitokeza katika kesi za uchaguzi. Mahakama isibariki vitu kama hivyo. Vina scandalize mahakama, na kuwafanya majaji waonekane hawatendi haki. Mtu aliyekuwa Kampeni meneja, anabadilisha utii wake wakati wa uchaguzi, na kutaka kutengua ushindi wa Yule ambaye yeye mwenyewe alishiriki katika kuupata. Tunashindwa kutengua ushindi kwa kutegemea ushahidi wa aina hii. Kama shahidi wa 18, alikuwa ni shahidi wa kuaminika, lakini alikataa kuwa hakuiba kura hata moja, na kile alichosema vilitokana na hisia tu. Yeye hakuiba kura, hata moja ila alitoa ushahidi wa hisia.

  Shahidi namba 11, kulingana na sheria za uchaguzi, hairuhusiwi kuchagua mtu asiyejua kusoma na kuandika kumchagua kuwa wakala. Kile alichosema huyu shahidi, ilikuwa ni vitu vya kubuni. Hivyo mahakama hii haiwezi kuamimi.

  Hisia za shahidi 10, hazitoshi, kulihitajika ushahidi zaidi. Tarehe ambayo CCM walileta, 30/10/2010. Barua hiyo haikugongwa mhuri wa kupokelewa na tarehe yenyewe ilikuwa ni siku moja kabla ya uchaguzi ambapo wengi walikuwa wameshaenda kwenye shughuli zingine za uchaguzi. Ilikuwa ngumu kuita kamati ya maadili siku hiyo. Kwa kuwa barua hiyo haikuwa na mhuri wa kupokelewa, na imeletwa na katibu wa CCM ilikuwa na hisia za kisiasa. Hii pia naitupilia mbali.

  Hoja ya Nne, ya kuwa mawakala wa Vyama vingine kupewa, maji, soda na biskuti. Mimi jaji nimejiuliza, hivi kwa sheria zetu kuna uwezekano wa kuwahonga mawakala?. Lissu alitaja kuwa sheria za uchaguzi zinazungumzia kuhonga wapiga kura, sio kuhonga mawakala.

  Haibishaniwi kuwa mawakala walikuwepo pale kulinda maslahi ya wagombea wao. Na kama walipewa Chakula, uwakilishi wa usawa utakuwa haupo, isitoshe hata waliotunga sheria hizo walisema kuwa mawakala wanaweza kuwa wapiga kura. Lakini sheria haisemi, lazima usimamie kwa maslahi ya Chama chako ambacho wewe unakisimamia.

  Hoja ya msingi, ili kuthibitisha hoja hii, ni shahidi 1,18,20,21. Mlalamikiwa Lissu aliwahonga na kuwashahishi kwa kuwapa usafiri katika vituo 124, siku ya uchaguzi, na chakula kilitolewa na pikipiki, na kuwa katika baadhi ya maeneo walitumia magari. Niseme katika hoja hii, mashahidi walipaswa wajikite katika hoja. Na wote walipaswa kujaza fomu za malalamiko kuhusiana na hili.

  Niseme kuwa , kwa mfano, inawezekanaje, mtu aache kitu ambacho ni cha msingi wakati wa kuandika malalamiko, lakini waje waseme baadaye wakti wa kusikiliza kesi. Mlalamikiwa Lissu na Cleti Kidamwina, kulingana na shahdii 14, 15, 4. 6,7, na 8 walimtaja Gineton Bulali na Bw. Toto wa CUF;

  Ninajibu hoja hii nikijua kuwa mawakala hawa hawakuwa wa CDM, kwa kuwa alisema kwanza walikuwa wa CHADEMA, baadaye walalamikaji wakasema kuwa alihonga mawakala wa vyama vingine. Hapa walalamikaji walikuwa Kinyonga, wanabadilika badilia. Kama mawakala wote walikuwa wa Lissu, hoja ya kuwa aliwahonga vyakula ingejitokeza? Jibu ni hapana. Kwa kuangalia, hoja hii ilikosewa. Kuna mashahidi waliosema kuwa Lissu alisema kuwa hana pesa, na kuwa wangepewa juice, maji na biskuti, na wengine walisema walimwona Lissu akigawa vyakula.

  1,na 5 wanasema walimwona, Mungaa kituo namba 3, lakini alipoulizawa maswali alisema alikuwa Makiungu namba2. Ushahidi huuu ulikuwa hauna unyoofu, alisema Lissu alikuwa na gari yake Land Rover, Discovery, lakini alisema kuwa wangekuja. Baadaye alisema alimwona akigawa chakula, baadaye akasema alimwona akiwa anapita, na baadaye alisema aliambiwa na mawakala. Ushahidi huu hauna unyoofu. Shahid 5, Sophia Mhoji, anasema alimwona Lissu akigawa chakula, makiungu, na alikuwa na Mateo. Lakini ushahidi wake pia unatilia shaka. Shahdi wa 10 katibu wa CCM alisema kuwa waliwapa kila wakala sh. 5000, lakini huyu wakala alisema hajui lolote juu ya hayo. Je alikuwa shahidi au alikuwa anaremba remba. Hata alipokuja hapa hakunyanyua kichwa hivyo sikuvutiwa na ushahidi wake mahakamani. Shahidi wa 9, alisema kuwa Lissu aliwaambia kuwa kwenye semina waliambiwa ni mawakala wa CHADEMA ndo wangepewa Juice, Maji na Juice.

  Dereva: Alitajwa na mgombea wa CCM Ikungi, alisema kuwa hakumwona Lissu, hivyo hakukuwa na na Muunganiko na suala kuwa Lissu aligawa juice.

  Suala la kugawa chakula, linaonekana halikuwa ni suala lililomhusu Lissu.

  Shahidi 7, alisema yeye ni Mwanachama wa CDM, hata hivyo hakujua nani aligawa na nani alinunua. Hivyo hakukuwa na muunganiko na malalamiko kumhusu Lissu

  Shahidi 8, hakumuunganisha Lissu na tuhuma yeyote.

  Kuhusu hoja ya Cleti Kidamwina.

  Ushahidi wa Kidamwina, alikataa kabisa kuwa hakuwa na pikipiki, na hajamiliki. Hivyo dai la kuwa alikuwa anamiliki pikipiki,

  Suala la rangi ya pikipiki na umiliki, mimi sioni kuwa ni muhimu. Alionekana akigawa hayo, ila haionekani kuwa alifanya hayo kwa Baraka za Lissu. Shahidi wa 13, alisema alimwona Kidamwina na hakumwona Lissu, Hivyo hivyo kwa shahidi wa 14, na 15. Huyu hakuwa na uongozi wowote ndani ya Chama, ni mfuasi tu ambaye hakuwa na ruhusa yeyote.

  Hata Mgombea wa CUF aliyegawa chakula naye hakuwa na Muunganiko wowote na Lissu. Japo aligawa chakula kinachofanana na kile cha kile cha CHADEMA. Binafsi sioni hoja kuhusu kufanana vyakula kwani sijui chakula gani kilikuwa kinapatina kwa urahisi katika mazingira hayo.

  Ushahidi mwingine mfano shahidi 21, ulionekana ulitengenezwa baada ya kesi kufunguliwa mahakamani. Huyu hakuwa na shahidi wa kuaminika, wakati yeye hakuwa amealikwa na akawa amaeamua kuchukua DVD, Huyu alikuwa na nia ovu.

  Shahidi 21, ni mkereketwa wa CCM alisema kuwa alimsikia Lissu akisema niliwapa. Binafsi naona kuwa haya hayakuwa na uzito.

  Shahidi wa 1 wa utetezi,Shaban Lyimu alitoa mchanganuo kuwa alipata chakula toka makao makuu, na mgawanyo. Walimwita katibu wa CUF ambaye alisema kuwa waliwaambia mashahidi wake wale chakula kisichozidi 2000/- Wakili wa walalamikaji alijitahidi kupunguza nguvu ya ushahidi wake, kwa hiyo hakutembelea vituo, lakini hata hivyo hata shahdi wa CCM ambaye alikuwa mgombea naye hakutoa ushahidi wa kweli.

  Sasa, naenda kwenye suala la rushwa. Vitendo vya rushwa vinavyodaiwa, mtuhumiwa anayedaiwa hakuwepo katika eneo hilo. Mahakama ilifafanua kuwa with knowledge, and approval. (Rejea kesi ya Mbowe na Eliofoo), kwamba, neno uthibitishe mpaka uiridhishe mahakama, kwamba uzito wa kuthibitisha hilo linamlalia mlalamikaji. Sio mlalamikiwa. Anayeomba uchaguzi utenguliwe ndiye anayethibitisha. Walalamikiwa hawakuleta ushahidi wa kutosha. Hoja hii pia naitupilia mbali. Sijazungumzia suala la usafirishaji kwa kuwa kwenye ushahidi mawakala walitoka vijiji vile vile. Wakili wa walalamikaji hakujipanga wakati wa kuandika shitaka

  Hoja ya TANO; Kwamba Ikungi Kituo namba 2, Mlalamikiwa alichukua kitabu cha kuhakiki wapiga kura, badala ya msimamisi wa uchaguzi. Shahidi alikuwa ni wakala wa CHADEMA, aliyekaa na wasaidizi. Hakukaa kwenye benchi, ambalo mawakala wenzake walikaa. Shahidi wa 4 alisema kwamba ilikuwa ni kinyume na sheria, na kwamba msimamizi wa pale aliitwa akaonywa. Suala liliisha. Shahidi 22, alipokuja hapa hakugusia tuhuma hizi, na alionekana alikuwa kituo cha Ikungi namba 4, kupingana kuwa 2, au 4, kuliongelewa sana na walalamikiwa. Wakasema kuwa aliyepaswa kuja kuthibitisha ni yeye, na kwa kuwa walimwita, na hakuthibitisha hivyo hata wao hawakuthibitisha kesi. Hata baada ya kuona orodha iliyoletwa, Husein alikuwa kituo namba 4, na hati yake ya kiapo ilikuwa ikionyesha vile.walalamikaji hawakuleta uthibitisho. Hivyo ni kesi ya kupika. Wakili wa serikali alisema yale yale kuwa Husein mwangia aliitwa lakini hawakumuuliza kwanini kulikuwepo na tofauti. Je kwenye mkanganyiko huo, je kunatoa ukweli kuwa huyu hakuwa wakala? Binafsi nimeona kuwa kasoro hizo ni ndogo. Ukiangalia kesi zingine zinasema kama contradiction ni ndogo tuna ignore. Anayetuhumiwa aliitwa mahakamani hakutoa maelezo. Jambo linalowapa manufaa walalamikiwa. Na bado suala hili halikuathiri uchaguzi. Maswali yanayohusu suala hili walipaswa kujibu wao, na sio kurushia kwa walalamikiwa. Shahidi wao alisema kuwa hakuna hata mmoja aliyekatazwa kupiga kura. Soma kesi ya Martha Michael Weja, agains AG, pg 61. Hakuna ushahidi unaoonesha kuwa kasoro hizo zaweza kuathiri matokeo. Hakuna ushaidi unaooonesha kuwa wakala wa CDM alikuwa anahakiki yeye peke yake bila msimamizi. Alitumia madaraka yake.

  Hivyo hoja ya tano naitulipia mbali.

   
 2. Ciphertext

  Ciphertext Senior Member

  #2
  Apr 27, 2012
  Joined: Apr 21, 2012
  Messages: 161
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kazi nzuri, ubarikiwe sana. Endelea tuko pamoja mpaka mwisho.
   
 3. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #3
  Apr 27, 2012
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Tupo pamoja lakini ungeitupia kule kule mkuu ulikoanzisha uzi wako wa hukumu.
   
 4. K

  Kagalala JF-Expert Member

  #4
  Apr 27, 2012
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 2,372
  Likes Received: 77
  Trophy Points: 145
  Asante mkuu kwa kutujuza. JF is more than ........
   
 5. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #5
  Apr 27, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 302
  Trophy Points: 160
  Sijui atapona, wakimwondoa basi wamejimaliza.
   
 6. m

  mgeni wenu JF-Expert Member

  #6
  Apr 27, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 3,669
  Likes Received: 614
  Trophy Points: 280
  Kapigwa chini lisu kama lema
   
 7. R

  Rev. Damasus Mkenda Member

  #7
  Apr 27, 2012
  Joined: Dec 22, 2011
  Messages: 67
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Good, give us the rest of the thing.
   
 8. mikatabafeki

  mikatabafeki JF-Expert Member

  #8
  Apr 27, 2012
  Joined: Dec 29, 2010
  Messages: 12,837
  Likes Received: 2,101
  Trophy Points: 280
  nimeshaanza kuingia mashaka hapa
   
 9. S

  Sarya Senior Member

  #9
  Apr 27, 2012
  Joined: Nov 6, 2009
  Messages: 144
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  mmmmmhhhh... Asante sana japo unanipa mashaka kuwa upo kwenye system. How possible is this! ukaandiaka vitu vyote hivi ukiwa mahakamani na kuriport.
   
 10. Bukanga

  Bukanga JF-Expert Member

  #10
  Apr 27, 2012
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 2,863
  Likes Received: 714
  Trophy Points: 280
  Asante mkuu!!
   
 11. j

  joeprince Member

  #11
  Apr 27, 2012
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 89
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13


  100% unatisha kwa reporting
   
 12. TIQO

  TIQO JF-Expert Member

  #12
  Apr 27, 2012
  Joined: Jan 8, 2011
  Messages: 13,832
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 0
  Jasho la mtu haliliwi hivi hivi
   
 13. Fredrick Sanga

  Fredrick Sanga JF-Expert Member

  #13
  Apr 27, 2012
  Joined: Jan 27, 2011
  Messages: 3,148
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Mahaka ikiwa na hakimu kichwa sio mchezo. Duhh, Naomba Mungu katika maisha yangu aniepushe kuingia mahakamani.
   
 14. andrewk

  andrewk JF-Expert Member

  #14
  Apr 27, 2012
  Joined: Apr 13, 2010
  Messages: 3,103
  Likes Received: 55
  Trophy Points: 145
  Huyu jaji alisoma wapi? na yule wa Kesi ya lema aliwama wapi ? mbona akili tofauti sana?
   
 15. PMNBuko

  PMNBuko JF-Expert Member

  #15
  Apr 27, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 971
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kazi imekamilika
   
 16. dubu

  dubu JF-Expert Member

  #16
  Apr 27, 2012
  Joined: Oct 18, 2011
  Messages: 3,072
  Likes Received: 422
  Trophy Points: 180
  hivi wewe mgeni jf? inakuaje ucopy maneno yote hayo halafu uandike maneno machache hivi? jiangalie sana.
   
 17. ludoking

  ludoking Senior Member

  #17
  Apr 27, 2012
  Joined: Oct 5, 2008
  Messages: 124
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Asante Mkuu
   
 18. Fabolous

  Fabolous JF-Expert Member

  #18
  Apr 27, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 1,302
  Likes Received: 436
  Trophy Points: 180
  Watoto wa Facebook hao hata mimi amenikera sana. !
   
 19. k

  kijereshi JF-Expert Member

  #19
  Apr 27, 2012
  Joined: Apr 2, 2012
  Messages: 257
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  mbna kma naona wakili msomi wasonga kapigwa chini na mh.lissu yan hawakujipanga na mashahidi wao wa kutengeneza magamba yanatapatapa sna aise
   
 20. C

  Curriculum Specialist JF-Expert Member

  #20
  Apr 27, 2012
  Joined: Oct 8, 2007
  Messages: 2,736
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Yule wa Lema alipewa shinikizo!
   
Loading...