foxolox
Member
- Nov 24, 2015
- 14
- 3
Kutokana na kuwepo baadhi ya nyumba ambazo zimejengwa kwenye maeneo hatarishi yakiwemo ya kwenye kingo za mito pamoja na bahari hususani kwenye eneo la mto msimbazi nyumba ambazo zipo pembezoni mwa mto msimbazi kwa umbali wa Mita 60; Kwa muda mrefu serikali ikitoa fidia na hifadhi kwa watu wa mabondeni kutokana kusombwa na mafuriko.
Na hali hiyo ilisababisha serikali kutoa viwanja katika eneo la Mabwepande kwa wakazi waliokuwa mabondeni. Na baadhi yao walihama lakini wengine waliendelea kusalia kwenye maeneo hayo ambapo wiki mbili zilizopita serikali ilianza zoezi la bomoa-bomoa katika maeneo hayo ambayo watu wanaishi Mita 60 ndani ya mto msimbazi.
Na bomoa-bomoa hiyo ilianzia kwenye eneo la Mkwajuni na baada ya siku kadhaa Waziri wa ardhi nyumba na maendeleo ya makazi William Lukuvi akawa amesitisha zoezi hilo mpaka Janauri 5 ambayo ni leo.
Lakini kabla ya kufika kwa siku ya Januari 5, wakazi wa Kinondoni wakiongozwa na Mbunge wa Jimbo hilo walikwenda kufungua kesi kwenye mahakama ya ardhi wakipinga kufanyika kwa hilo zoezi la bomoa-bomoa. Na kesi yao jana kwa mara ya kwanza imekuja kusikilizwa hapa kwenye mahakama kuu ya ardhi ambapo Jaji wa Mahakama hiyo Kuu ya Ardhi, Mh. Panterine Kente alisikiliza pande zote kwa maana ya waleta maombi pamoja na upande wa watetezi kwa upande wa serikali na mjadala ulikwenda kwa muda kidogo ikawa wamezungumza kila mtu akitoa hoja zake kutetea upande aliopo.
Lakini baada ya majadiliano ya muda mrefu ya kisheria Jaji Pente akawa ameamua kwamba leo majira ya saa tano angeweza kutoa maamuzi kwamba nini kitafuata kama ni kusitisha hiyo bomoa bomoa au kuendelea na taratibu zipi.
Sasa kilichotokea leo katika eneo la mahakama ambayo ipo katikati ya Jiji hapa kwenye mtaa wa Samora, nimefika majira ya asubuhi kshuhudia kesi hiyo ifanyiwe hukumu kwa maana ya kutolewa uamuzi majira ya saa tano lakini hilo halikuweza kufanyika.
Taarifa imetolewa mahakamani kwamba hukumu ya kesi hiyo itatolewa majira ya saa nane mchana. Wakazi zaidi ya mia sita wa kinondoni wako nje pembezoni mwa barabara ya Samora wakisubiri maamuzi ya kesi yao. Jeshi la Polisi linaonekana kuimarisha ulinzi katika eneo hili kuna magari ya doria ya polisi ambapo tayari wameshatoa tangazo kwa wananchi hao kwamba waondoke katika eneo hili.
Kwahiyo maamuzi ya bomoa inaendelea au inasitishwa ni saa nane leo mchana.