Hukumu ya Babu Seya, Papii, Mapya tena yaibuka

Hukumu ya Babu Seya, Papii, Mapya tena yaibuka


View attachment 501822
Tumaini jipya! Mtoto wa kiume wa mfungwa anayetumikia kifungo cha maisha jela, Nguza Viking ‘Babu Seya’, Mbangu Nguza ameibuka na kusema kuwa, mwaka 2017 ndiyo wa mwisho kwa baba yake na mdogo wake, Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ kuendelea kutumikia kifungo chao cha maisha jela.

Akizungumza katika mahojiano maalum na Gazeti Amani mwanzoni mwa wiki hii, Mbangu alisema kuwa, turufu ya mwisho ya hukumu ya ndugu hao ipo kwenye mikono ya Mahakama ya Haki za Binadamu Afrika (AfCPHR) yenye makazi yake jijini Arusha ambayo kimsingi vikao vitatu vya awali vimeshakaa na kubaini kuwa, hukumu ya Babu Seya na Papii ilikuwa na kasoro.

“Unajua watu hawafahamu, kule ambako hukumu ya mzee na bwana mdogo (Papii), ilipelekwa kuna hatua. Kwanza kabisa, wale majaji wanatoka nchi mbalimbali, kwa hiyo siyo kwamba wanakwenda tu Arusha na kupitia hukumu, hapana.

“Kilichofanyika ni kwamba, kuna watu walikaa mara tatu kupitia hukumu ili wajiridhishe kama kuna makosa ambayo majaji wakikaa watayaona?
“Kwa hiyo vile vikao vimeshakaa mara tatu zote na kubaini kuwa, kweli hukumu ya baba na bwana mdogo ilikuwa ina kasoro.

“Sasa ndiyo majaji wameitwa ili kupitia na kutoa hukumu yao ya haki. Hii kazi ingekuwa imeshafanyika muda mrefu ila sasa, kilichotokea ni kwamba, kuanzia Novemba mwaka jana kama sikosei, watu wa mahakamani walikuwa likizo ndefu mpaka kwenye Februari mwaka huu, ndiyo wamerudi.

“Kingine kimechelewesha ni mwaka jana kustaafu kwa rais wa ile mahakama, Jaji Augustino Ramadhani (kutoka Tanzania), kukawa na kitambo cha kusubiri kumpata rais mpya, tayari yupo (Sylvain Ore kutoka Cote d’Ivoire).
“Kwa hiyo bwana, baada ya sasa, wakati wowote ule, majaji watatua Arusha na kukaa kupitia, naamini, tena narudia kusema, naamini, baba na bwana mdogo wangu mwaka huu watakuwa huru.

“Hili suala la wao kuwa huru liko pia kiroho, hata kama mahakama hiyo isingekaa, bado wale ndugu wangetoka tu, lazima. Kwani Mungu ninayemtegemea mimi ameshaniambia watatoka,” alisema Mbangu ambaye kwa sasa ni Mwinjilisti wa Neno la Mungu.

TUMEFIKAJE HAPA?

Nguza na wanawe watatu walikamatwa Oktoba 12, mwaka 2003 na kufikishwa Kituo cha Polisi Magomeni, Dar, walipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Oktoba 16, mwaka 2003 wakituhumiwa kubaka na kunajisi watoto 10.

Baada ya kusikilizwa kesi hiyo Juni 25, 2004, Hakimu Mkuu Mkazi wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar, Addy Lyamuya aliwatia hatiani Babu Seya na wanaye kwenda jela maisha kwenye Gereza la Ukonga, Dar es Salaam.

Januari 27, mwaka, 2005, Jaji wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, Thomas Mihayo alitupilia mbali rufaa yao iliyokuwa ikipinga hukumu.

Awali mwaka 2004, baada ya kukutwa na hatia katika kesi hiyo, Babu Seya, Papii Kocha na wakili wao, Mabere Nyaucho Marando walikata rufaa ya pili ambayo ilitupiliwa mbali.

Mwaka 2010 waliomba tena rufaa ambayo marejeo yake yalisikilizwa na kutolewa hukumu Februari, 2010. Mahakama iliridhia hukumu ya kifungo cha maisha kwa Babu Seya na Papii Kocha, ikawaachia huru watoto wake, Mbangu na Francis Nguza.

Chanzo: Global Publishers
Hivi Una Uelewa wa Mahusiano kati ya mahakama za kikanda za haki za binadamu (REGIONAL HUMAN RIGHTS COURTS) na Mahakama za Nchi?????? HAKUNA MAHAKAMA YOYOTE YA KIMATAIFA AU YA KIKANDA YENYE UWEZO WA KISHERIA KUTENGUA HUKUMU ZA NDANI ZA NCHI (Domestic Court Judgments).... Wanasheria Watanielewa..
 
Mkuu utakuwa unaongelea watoto wa miaka ya nyerere walikuwa hawadanganyi.sio kizazi hiki cha watoto wa bongo movie wakipangwa wanaitendea haki script
Sio chini ya vitisho, ukimtisha atasema tu, mtoto hajui kudanganya! Atasema mama kaniambia niseme!
 
We unadhani kwa nn walionewa tuanzie hapo,pili kwa hyo watoto watunge kila wanapohojiwa wasisahau,imagine mtoto wako wa miaka 5 alawitiwe na MTU mzima au hata na mtoto mwenzake utajiskiaje,we we ushabiki unakupoteza,daktari atunge ripoti,hawa watu hawajui watoto walipelekwa kupimwa wp na want wnasheria wao?rufaa zote ziwe zinatupwa tu,unanikumbusha bibi mmoja alimfuata baba mkwe wangu akaongee na mwanawe kW kijana wake hajaua,mke wangu na babake wakaenda kumuona jaji manento during lunch,manento akamjibu baba ukiona kesi imefika kwangu ujue ushahidi wote umekamilika,alikuwa mahakama kuu au ya rufaa kipindi kile
Mijitu bhana sijui akili zenu zimejaa mavi, kama MBASHA walisema kabaka na daktari ka confirm ,sembuse hao unaowasema???? Jiulize kwann yupo nje hadi sasa....
 
mi hii kesi siijuagi naiskiaga tu bora nipite hivi?
 
Wewe kwa akili yako mahakama za Tanzania zipo huru au zimebanwa angalia kesi ya uchaguzi mita200 inavyofinyangwa. Yule mwalimu kowadi wa kina babu Sega unaeambiwa alikuwa anawatoa darasani hakufungwa na hata sura yake haikuwekwa hadharani na alipewa ukuu wa cwt Kagera na yule hakimu akaenda kusomeshwa ujaji jamhuri ya Czech! Mahakama zetu no full magumashi ushahidi unafinyangwa
Mahakama zipo huru, kama kuna hakimu au jaji mmoja anakula rushwa hiyo haina maana kwamba mfumo mzima wa utoaji haki ni mbaya. Kuhusu hii kesi kama kweli kuna uonevu tuhoji sheria yenyewe. Sheria ya makosa ya kujamiina imejaa ukatili dhidi mwanaume. Ni rahisi sana mbaya wako kukuangamiza kupitia sheria hiyo.
 
Nadhani wakili Nyaucho Marando alifanya kazi iliyotakiwa vyema na ishu hii ilishaisha hizi ni highlights tu
 
Wabongo wanafiki sana,yani majitu yanaacha kusikitikia watanzania wenzetu walioko huko magerezani kwa makosa ya kusingiziwa.yenyewe yamekalia kusikitikia hawa wabakaji waliobaka kikwelikweli.
Uliwashikia miguu?
 
una
Wabongo wanafiki sana,yani majitu yanaacha kusikitikia watanzania wenzetu walioko huko magerezani kwa makosa ya kusingiziwa.yenyewe yamekalia kusikitikia hawa wabakaji waliobaka kikwelikweli.
unavoandika kwa uchungu bila shaka na wewe ulikua mmoja kati ya waliobakwa pole sana mkuu!
 
wafungwe tu hawana faida kwa jamii, Watanzania kwa kujikwezaaaaa, kwani Watanzania wangapi wamefungwa nje ya Nchi na hamuwasemi humu ndani? Au nanyi ni wateja wa babu seya sasa mmekosa wa kuwakuna?
 
Mahakama ilitenda haki, Asante wana sheria, watoto hawadanganyi,
Mijitu mingine mi pumbavu inazusha hadithi iliionekane alionewa,
 
Wanasheria mnisaidie, kesi kama hii katika mahakama hii ya Afrika huwa ni kwa ajili ya kuangalia sheria kama ni kandamizi na kuagiza nchi husika kufanya marekebisho au hata kesi za rufaa za jinai dhidi ya serikali husika?
 
Wabongo wanafiki sana,yani majitu yanaacha kusikitikia watanzania wenzetu walioko huko magerezani kwa makosa ya kusingiziwa.yenyewe yamekalia kusikitikia hawa wabakaji waliobaka kikwelikweli.
Hivi inaingia akilini kweli familia yote kubaka? Yan baba mpk watoto?
 
Back
Top Bottom