Hukumu ya Babu Seya, Papii, Mapya tena yaibuka

Hukumu ya Babu Seya, Papii, Mapya tena yaibuka

Wabongo wanafiki sana,yani majitu yanaacha kusikitikia watanzania wenzetu walioko huko magerezani kwa makosa ya kusingiziwa.yenyewe yamekalia kusikitikia hawa wabakaji waliobaka kikwelikweli.
Kimsingi hata Babu Seya pia ni binadamu mwenzetu na akionewa tunasikitika pia kama alivyoonewa mtu yeyote.
Tusaidie kutuambia watanzania walioonewa maana watakuepo ila hatuwezi kuwajua kutokana na kutokua maarufu kama Babu Seya
 
Wabongo wanafiki sana,yani majitu yanaacha kusikitikia watanzania wenzetu walioko huko magerezani kwa makosa ya kusingiziwa.yenyewe yamekalia kusikitikia hawa wabakaji waliobaka kikwelikweli.
Alikubaka wewe Papy hana uhaba wa wanawake mpaka abake watoto. Kumbuka hii kesi walipewa familia nzima sasa mbona wengine waliwatoa kama so uonevu
 
images.jpg

Tumaini jipya! Mtoto wa kiume wa mfungwa anayetumikia kifungo cha maisha jela, Nguza Viking ‘Babu Seya’, Mbangu Nguza ameibuka na kusema kuwa, mwaka 2017 ndiyo wa mwisho kwa baba yake na mdogo wake, Johnson Nguza ‘Papii Kocha’ kuendelea kutumikia kifungo chao cha maisha jela.

Akizungumza katika mahojiano maalum na Gazeti Amani mwanzoni mwa wiki hii, Mbangu alisema kuwa, turufu ya mwisho ya hukumu ya ndugu hao ipo kwenye mikono ya Mahakama ya Haki za Binadamu Afrika (AfCPHR) yenye makazi yake jijini Arusha ambayo kimsingi vikao vitatu vya awali vimeshakaa na kubaini kuwa, hukumu ya Babu Seya na Papii ilikuwa na kasoro.

“Unajua watu hawafahamu, kule ambako hukumu ya mzee na bwana mdogo (Papii), ilipelekwa kuna hatua. Kwanza kabisa, wale majaji wanatoka nchi mbalimbali, kwa hiyo siyo kwamba wanakwenda tu Arusha na kupitia hukumu, hapana.

“Kilichofanyika ni kwamba, kuna watu walikaa mara tatu kupitia hukumu ili wajiridhishe kama kuna makosa ambayo majaji wakikaa watayaona?

“Kwa hiyo vile vikao vimeshakaa mara tatu zote na kubaini kuwa, kweli hukumu ya baba na bwana mdogo ilikuwa ina kasoro.

“Sasa ndiyo majaji wameitwa ili kupitia na kutoa hukumu yao ya haki. Hii kazi ingekuwa imeshafanyika muda mrefu ila sasa, kilichotokea ni kwamba, kuanzia Novemba mwaka jana kama sikosei, watu wa mahakamani walikuwa likizo ndefu mpaka kwenye Februari mwaka huu, ndiyo wamerudi.

“Kingine kimechelewesha ni mwaka jana kustaafu kwa rais wa ile mahakama, Jaji Augustino Ramadhani (kutoka Tanzania), kukawa na kitambo cha kusubiri kumpata rais mpya, tayari yupo (Sylvain Ore kutoka Cote d’Ivoire).

“Kwa hiyo bwana, baada ya sasa, wakati wowote ule, majaji watatua Arusha na kukaa kupitia, naamini, tena narudia kusema, naamini, baba na bwana mdogo wangu mwaka huu watakuwa huru.

“Hili suala la wao kuwa huru liko pia kiroho, hata kama mahakama hiyo isingekaa, bado wale ndugu wangetoka tu, lazima. Kwani Mungu ninayemtegemea mimi ameshaniambia watatoka,” alisema Mbangu ambaye kwa sasa ni Mwinjilisti wa Neno la Mungu.

Chanzo: http://www.muungwana.co.tz/2017/04/exclussive-babu-seya-kuachiwa-huru.html?m=1
 
Alikubaka wewe Papy hana uhaba wa wanawake mpaka abake watoto. Kumbuka hii kesi walipewa familia nzima sasa mbona wengine waliwatoa kama so uonevu
We unadhani kwa nn walionewa tuanzie hapo,pili kwa hyo watoto watunge kila wanapohojiwa wasisahau,imagine mtoto wako wa miaka 5 alawitiwe na MTU mzima au hata na mtoto mwenzake utajiskiaje,we we ushabiki unakupoteza,daktari atunge ripoti,hawa watu hawajui watoto walipelekwa kupimwa wp na want wnasheria wao?rufaa zote ziwe zinatupwa tu,unanikumbusha bibi mmoja alimfuata baba mkwe wangu akaongee na mwanawe kW kijana wake hajaua,mke wangu na babake wakaenda kumuona jaji manento during lunch,manento akamjibu baba ukiona kesi imefika kwangu ujue ushahidi wote umekamilika,alikuwa mahakama kuu au ya rufaa kipindi kile
 
Duh! Ila maisha ya jela jamani,, nimeangalia hiyo picha ya band wakitumbuiza, nimetafakari sana na hata kushangaa nyuso zao zikiwa nafuraha tu, ina maana wamepewa kitengo cha band sio!!?
 
Wewe kwa akili yako mahakama za Tanzania zipo huru au zimebanwa angalia kesi ya uchaguzi mita200 inavyofinyangwa. Yule mwalimu kowadi wa kina babu Sega unaeambiwa alikuwa anawatoa darasani hakufungwa na hata sura yake haikuwekwa hadharani na alipewa ukuu wa cwt Kagera na yule hakimu akaenda kusomeshwa ujaji jamhuri ya Czech! Mahakama zetu no full magumashi ushahidi unafinyangwa
 
Kama ni kweli walibaka, waozee huko huko, kama hawakubaka justice will prevai, ila mtoto hajui kudanganya!
Mkuu utakuwa unaongelea watoto wa miaka ya nyerere walikuwa hawadanganyi.sio kizazi hiki cha watoto wa bongo movie wakipangwa wanaitendea haki script
 
Duh! Ila maisha ya jela jamani,, nimeangalia hiyo picha ya band wakitumbuiza, nimetafakari sana na hata kushangaa nyuso zao zikiwa nafuraha tu, ina maana wamepewa kitengo cha band sio!!?
Sometimes unaweza ku create heaven in Hell! Utanuna vipi wakati una namba ya kuingia jela tu ila ya kutoka huna?
 
Back
Top Bottom