Hukumu Rufaa ya Godbless Lema yaiva

Hivi Lema akishinda rufaa baadaye CCM wakaipinga kwa kigezo cha jopo la majaji ku- include mtu ambaye si jaji itakuwaje? Technically huyu mzanzibar si jaji.
'Patamu' sana hapo!
 
Yule jaji aliyetoa hukumu nasikia yupo India kapooza na ameshakua kichaa.

Hilo ni somo muhimu sana kwa wakina jaji
Natalia Kimaro, Mbarouk Salim Mbarouk na Salum Massati kuwa Lema yupo pale kwa matakwa ya wananchi kwahiyo laana za wananchi huwa hazichelewi kupatiwa majibu na Mungu
 
Hapo hukumu itatoka kwa Jaji Massati na Kimaro,huyu mwingine jaji voda faster atawasindikiza tu.

Wakiambiwa wanateua majaji vihiyo wanabisha,sasa Werema aje abishe kuwa huyu jaji hasomi chuo kikuuu huria. Sasa kati ya Werema na Lissu nani anatumia kichwa chake kufuga nywele na sio kufikiri.
 

Kama huu ushahidi wa Mh Tundu Lissu ni wa kweli basi sijui hii nchi tuiiteje? Mtu anapanda vyeo hadi kuwa jaji wa mahakama ya rufaa huku akiwa hajawahi kusoma japo shahada ya kwanza ya sheria? Ajabu mno! Tusishangae kuambiwa ana sifa zaidi ya mwenye LLB, maana tumeshasikia sana hadithi zinazosema advanced diploma ni sawa na degree ya kwanza, lakini hatuambiwi kwa nini universities zinaendelea kutoa degrees badala ya advanced diploma, au kwa nini hiyo diploma isiitwe degree kama ziko sawa. Nashangaa mno!
 
Huyu kwenye red si ndiyo Mwanafunzi wa LLB Open university aliyetajwa na Tundu Lisu kuwa Kiwango Duni! Sina imani Naye atakomoa CDM.
 
Kama kuna mtu ana access na profile ya Lema pls ningependa kuona CV yake hapa JF! Asije akawa naye ni kihiyo tu asiye deserve kuwakilisha wananchi Bungeni!
 
Tundu Lissu kafanya 'timing' nzuri sana kwa sababu Mbarouk kashatajwa mapungufu yake kwenye utetezi wa Lissu, atafanya makosa ili Lissu apate sema 'si mnaona.

I told you! Naamini Mbarouk atakuwa makini kulinda integrity yake, by the way jamaa anamalizia LLB pale OUT soon.
 

Mhhhh sidhani kama Lema atashinda kesi hii maana Naliona jina la Jaji Mbarouk Salim Mbarouk ambaye ametajwa kwenye Ripoti maalum ya TUNDU LISSU aliyoitoa kwenye kamati ya Haki, Kinga na maadili ya Bunge. Hofu yangu ni kuwa Watataka kuionesha Chadema kuwa wao ni Majaji makini!!! Hebu Tusubiri tuone, ila dalili nayoiona ni GIZA kwa Lema
 
hapa hamna kitu lema atulie tu aendeleee na kazi yake ya ujangiri kama zamani na kukwiba magari ya watu arusha kama alivyotuhumiwa na zombeee kwakuwa wanajuana vizuri..ubunge asahau kwa sasa

kumbe bado una ule ugonjwa wa kichwa! samahan sikufahamu mapema
 
Nina imani kubwa na Mahakama ya Rufaa kuliko mahakama yoyote Tanzania..
 
Angalizo:

Huyo jaji mbarouk salum mbarouk,ni jaji kwa magamba na jk lakini kikatiba si jaji wa jmt na lolote atakalo fanya ama maamuzi atakayotoa hayatambuliki
(kwa sasa ndio mwanafunzi wa sheria chuo kikuu huria)

akataliwe ili awekwe jaji anaestahili kwa mujibu wa katiba ya jmt

nawakilisha
 

kweli.. Kwa mujibu wa Katiba hajakidhi vigezo vya kuwa Jaji huyu jamaa.. Ni vyema akakataliwa mapema (Japokuwa sijui taratibu za kumkataa jaji wa mahakama ya Rufani)
 
Imekaa vizuri Lema atarudi bungeni namuamini sana jaji Salum Massati 99.9% pia na Natalia Kimaro 80% lakini huyu walakini Mbarouk Salim Mbarouk 50%

Mkuu naunga mkono hoja ila Mbarouk 30% namwamini. Huyu yuko kwenye orodha ya Tundu Lissu.
 
Kuna tetesi zilishaletwa hapa kuwa huyu Jaji Gabriel Rwakibarila alipooza miguu. Hebu mtu athibitishe pls
 
Uzuri katika case hii ni kwamba tuna majibu ikiwa itaamuliwa tumeshindwa. Itakuwa ni yale yalee. Kesi ya nyani kapewa ngedere wakati nyani ni boss wake ngedere. Ki-ukweli kwenye jamii ya kimasai mwanamke hawezi kuwa kiongozi na hizo ni mila zao hazihusiani na watu wengine na lema alikuwa anawaambia wamasai japo wagogo, wazaramo etc.. walisikia pia
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…