Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,899
Wagombea udiwani wa CHADEMA katika Kata ya Tindabuligi, Ndugu Zunzu Ndatulu Humu na Kata ya Kisesa, Ndugu Shanemhanga Mabula Makonge , Wilaya ya Meatu, mkoani Simiyu, wamenyimwa fomu za kukata rufaa baada ya kuenguliwa kwenye uchaguzi jana usiku.
Jitihada za wagombea hao na viongozi wa Chama kupata fomu hizo na. 12(c) kwa Msimamizi wa Uchaguzi ambaye ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Meatu, Ndugu Manoza, hadi sasa hazijafanikiwa baada ya Msimamizi huyo kutoonekana ofisini tangu asubuhi tofauti na alivyokuwa amewaahidi na kuwataka wafike kwake wachukue fomu hizo. Hata simu zake ambazo alikuwa anapokea hadi jana usiku, hazipatikani.
Wagombea hao walirejesha fomu zao za kugombea kwa Wasimamizi Wasaidizi wa Uchaguzi katika kata hizo Jumatatu, 20 Agosti, mwaka huu. Hadi majira ya jioni jana Jumanne Mgombea wa Kata ya Tindabuligi alikuwa hajawekewa pingamizi lakini ghafla saa 1.30 usiku kuwa akataarifiwa kuwa amewekewa pingamizi na akapewa barua ya kuenguliwa kwenye uchaguzi.
Taarifa za awali zimesema kuwa mgombea huyo pamoja na viongozi wa chama walipohoji kuenguliwa bila haki ya kujibu mapingamizi yaliyowekwa, waliambiwa hakuna fursa hiyo. Taarifa hizo zimedai kuwa kitendo hicho kilifanyika mbele ya Msimamizi wa Uchaguzi (Mkurugenzi) pamoja na maofisa wakuu wa vyombo vya dola ngazi ya wilaya waliokuwepo ofisini kwa Msimamizi Msaidizi wa Uchaguzi.
Kwa upande wa Kata ya Kisesa, mapingamizi yaliyowekwa saa nne asubuhi jana, yalijibiwa na mgombea na kurejeshwa kwa wakati jana hiyo hiyo, lakini ilipofika majira ya 2.30 usiku naye akataarifiwa kuwa ameenguliwa kwenye uchaguzi.
Jitihada za wagombea wote kuwataka Wasimamizi Wasaidizi wawapatie fomu na. 12(c) kwa ajili ya kukata rufaa zilishindikana kwa kile kilichodaiwa kuwa fomu hizo hazipo bali zinapatikana kwa Msimamizi wa Uchaguzi watazipata.
Walipowasiliana na Msimamizi wa Uchaguzi jana usiku, aliwataka wafike ofisini kwake Jumatano, Agosti 22, mwaka huu (leo) asubuhi ili awapatie hizo fomu waweze kukata rufaa. Hadi jioni hii hajaonekana ofisini wala hapatikani.
Kata ya Mwanhuzi, Simiyu
Katika Kata ya Mwanhuzi ambayo nayo inatarajia kufanya uchaguzi wa marudio, Msimamizi Msaidizi alikataa kuzipokea fomu za Mgombea wa CHADEMA, baada ya kuzipitia na kuzihakiki, akisema kuwa zipelekwe siku ya Alhamis, Agosti 23 ambayo ndiyo siku ya mwisho ya kurejesha fomu na kufanya uteuzi wa wagombea katika kata hiyo.
Makene