Hujuma zaanza 'Train ya Mwakyembe'

Tungeweza hata 'kuazima' utaratibu wa wenzetu wa kutumia kadi. Zifungwe system zitakazo-charge kadi ya mtu pale anapotumia usafiri huo, na siyo kumtegemea bwana konda. Na mtu ata-load kadi yake na pesa kama anavyofanya kwenye simu, kuwa aweke kutokana na uwezo wake na siyo kung'ang'aniza kuwa kuna kadi ya elfu tano na elfu kumi tu!

Anyways, safari hatua.

Itabidi wajenge na zile entrance za kuslidisha hizo kadi sasa.
 
Itabidi wajenge na zile entrance za kuslidisha hizo kadi sasa.

Sijui watadai gharama ni kubwa toba yarabi!! Au labda kila mlango wa behewa kuwe na zile za ku-punch hiyo kadi mtu aingiapo na atokapo.
 
jamani mi nafikiri hizi ni changamoto tu, tuzikabili maana ndo kwanza huduma yenyewe in siku ya pili, so tuwe wavumilivu kidogo. hata hivyo nikushukuru kwa observation umeyofanya, nafikiri itachangia sana kuboresha huduma hii muhimu kwa wakati wa dsm na taifa kwa ujumla
kuna haja ya kutoa tenda ya kukusanya mapato hayo kama itawezekana kwa kupiga hesabu za kawaida kabisa, kwa mfano, treni inaweza kufanya safari 10 kwa siku, na kila safari inaweza kubeba wastani wa abiria 1200 (kwa maana ya mabehewa 6 na kila behewa watu 200) na kila abiria atatoa nauli ya sh 500, kwa hiyo mzabuni atatakiwa kukusanya sh 6m kwa siku kwa tren 1, sasa tufanye 20% ni gharama zake, kinachobaki alete kwa shirika

au inawezekana kutangaza tenda, na highest bidder akapewa uwakala wa kukusanya hayo mapato
swala la ratiba kwa kila kituo, naunga mkono 100%
 
4. Watu wawe wananunua tiketi zao mapema na siyo kukatisha kwenye mabehewa hilo linaweza hata kupenyeza rushwa

Mfano Afrika kusini kuna mageti kwenye vituo vya treni. Labda hilo ni suala gumu hapa kwetu ila nashauri watu wanunue tiketi zao hapo kituoni. Atakayepanda awe ni yule mwenye tiketi tu. Na waweke ma-inspector kama kwenye UDA
 
Janana leo nilibahatika kupanda train ya TRC kutoka Tabata Matumbi hadi Posta ambayo ilinichua dakika 30 kufika Posta.

Ninawapongeza watanzania kwa kujitokeza kwawingi kupanda train na pia Mh. Mwakyembe kwa kusimamia kuanzishwa kwa trainhii. Lakini nimenisikitishwa ni hujama za wazi zinafanywa na watendaji pamojana wazabuni waliopewa kazi ya kukusanya nauli ndani train.

Train hii imekuwa ikiendeshwa bila kuwa na ratiba maalumu kitu ambacho kimekuwa kikikatisha tamaa abiria ambao wamekuwa wakisubiri kwa muda mrefu mathalani jana nilipanda train Tabata matumbi saa 2.15 asubuhi kuelekea post lakini leonilipofika saa 8.00 kituo niliambiwa kuwa train imechelewa kuanza safari asubuhi kwa sasa wapo safari ya kwanza bado posta eti kisingizio ni kuwa jana walichelewa kumaliza hadi saa 4.00 usku kwani hiyo driver amechelewa kuamka, jejambo hilo ni sahihi? Kwani hakuna driver mwingine ambaye angewahi kuamka nakuanza kuendesha train kulingana na muda?

Pia nimeshangazwa na wakatisha tiketi wa Selcom wireless ambao wako ndani train lakini hawafuati wateja kudai walipe zaidi ya hapo kwenye behewa nilolipanda waliakatisha ticketi sio zaidi ya 30 wakati ndani tulikuwa zaidi ya abiria 200 kwenye behewa moja na train yote ilijaa.

Sikweza kuvumilia nilipofika mwisho nilimuuliza kiongozi wa TRC kwanini watu hawadaiwi ticket/nauli wakajitetea kuwa wao wanashangaa. Niionavyo mimi hii ni hujuma ili ionekane kuwa gharama za uendeshaji ni nkubwa kuliko mapato na hivyo kupelekea kusimamishwa hudumu hii muhimu sana kwa wananchi wa Dar es Salaam.

Ninamshauri Mh. Mwakyembe na TRC ya yafuatayo:

  1. Kuweka ratiba makini ya train kwa kila kituo ili abiria ajue muda gani atapanda train katika kituo gani na kuelekea wapi
  2. Kuteua kampuni nyingine au watendaji wengine watakao husika na ukatishaji ticket ili kampuni iweze kupata mapato stahili yatakayopelekea kuboresha train hii na
  3. Kuongeza idadi ya Train au mabehewa kwa kila train kwani tumekuwa tukibanana sana kiasi inaweza kuatarisha afya za watumiaji.

Nafikiri kama mambo haya yatatekelezwa basi usafiri huu utakuwa mkombozi kwa watu wengi sana.

Mkuu hapo kwenye RED ningeomba usivumilie vilevile na umfikishie Mwakwembe ili achukue hatua, Japo naamini humu JF anapita pita lakini naye hakawii kusema hakuona hizi hujuma!

Salute!

 
Watu mnatoa hoja kama kwamba hamjui mashirika ya umma yalikufa vipi. Ama wengi wenu mlikua hamjazaliwa? Hizo ni tabia zetu Watanzania! Abiria unataka upande bure/nauli pungufu na mkata tiketi yupo radhi apokee pesa pungufu,asikupatie tiketi,pesa aweke mfukoni kwake!
 
Wiki hii itakuwa ni wiki ya kutathmini mapato ya kila siku, sasa kuna uwezekano mkubwa hao waliopewa dhamana ya kukusanya nauli, kukusanya kwa watu wachache ili baada waweze kuchukulia kwamba hayo ndio makusanyo; kumbe wanapiga bao zaidi. Tunajimaliza wenyewe, wala tusitafute mchawi; nawe abiria ukiona hakuna mtu aliyekuuliza nauli ni wajibu wako kuhakikisha unalipa nauli na kupata tiketi.
 
Ngoja niwape akili enyi wadanganyika.

Hii dili ya mapato wawekeane target na huyo silicomu sijui milicomu. Lete hesabu ya kila behewa mfano Tzs 300,000 zinazobaki zako.

Ukipata chini ya hapo hatujui.
Ukipata zaidi ya hapo hatujui.

Period
 
Katika Hali yoyote Haya unayoyasema Niliyategemea!! Ila cha Muhimu ni Kuwa na Uwajibikaji siku Zote!! Fikiria kuweka ratiba Kwenye Kila kituo sio Kitu Kigeni katika Jamii yoyote iliyostarabika!! Huwezi Kwenda Kupanda Train bila kujua ratiba yake!

Sasa Hawa wafanyakazi wa TRC mbona wanaonekana kama wanahujumu Kazi yao wenyewe?? Ni bora Mheshimiwa Mwakiembe akapendekeza responsible person incharge of complains!

And make a quick solution, Tupo karne ya 21, Haya madogo kwa nini yatushinde??


Hawa ndio Watanzania waliolaanika...sio ajabu kwa haya yanayo fanyika sasa...mashirika yote ya Umma yaliyobinafsishwa yalikufa kwa mitindo type hiii....sasa kwa hili kama style ndio hii kuna picha kama mbili hivi hapa..inawezekana ikawa ni maagizo rasmi kutoka kwa kundi flani kukwamisha jitihada za Muheshimiwa ionekane kuwa alitaka sifa lakini si mnaona imeshindikana...au ni kwa makusudi linafanyika hili kwa sasa kwasababu ni mwanzo ili iwe ndio mpenyo wa hujuma za mapato kuingia kwenye mifuko ya watu...kwa kutengeneza mazingira from the day one kwamba matapo halisi Train inapojaa au kuwa tupu yasijulikane huu uwe uchochoro mzuri wa kuiba...kwa sababu kwa vyovyote vile huduma hiii haiwezi kuendeshwa kwa hasara..hapa ni faida tupu kwa hali ya usafiri ilivyo Dar es salaaam.

Sasa Muheshimiwa mimi nafahamu wewe ni mtembezi sana mitaaa hii....Kaka usicheke na Kima..kama ukicheka na Kima aibu itakuwa yennu...Fukuza watu hapa kama huna akili sawasawa..usicheke nao hawa Fisi maji kabisa...ni hayo muheshimiwa
 
katika nchi ya Tanzania, sijui kwanini MKOLONI hakutuachia accountability na reasoning capacity.Yani kila kitu kina kasoro mpaka inatia kichefuchefu, swali ambalo nimekuwa najiuliza kila siku lakini majibu sipati ni "kwanini kama mzungu anaweza sisi hatuwezi?" Sababu waliyo toa ya kuwa walichelewa kumaliza hadi saa nne ni upumbavu mkubwa sana ambao hautakiwi hata kutamkwa.

Hivi kweli kuna haja ya hawa watu kukumbushwa au kuambiwa kuwa wanahitaji kuweka mda maalum kwa kila kituo na kuajiri madereva wengine ili watu waweze kufanya shughuli za maendeleo?Yani kuna vitu vinasikitisha sana.
 
Posted: 6th November 2012 by MillardAyo in News

.

millardayo.com imetumiwa hii ripoti kuhusu hujuma zilizoanza kufanywa kwenye moja kati ya treni maarufu kama treni ya Mwakyembe inayosafirisha abiria kati ya Ubungo na Posta Dar es salaam.
Taarifa yenyewe inasema “Tumepandia mabibo mwisho hakukuwa na mkatisha tiketi ndani ya treni, abiria waliongezeka zaidi tulipofika buguruni kwa mnyamani, ila bado hakuingia wakala yeyote mkata tiketi lakini gari lilipofika kamata ambapo abiria wengi wanaoelekea k/koo na mitaa ya karibu hushuka, so huyo
jamaa mwenye cap nyeupe alikuwa upande wa kutokea akaanza kuchukua pesa kwa abiria bila kutoa tiketi, baada ya treni kutoka kamata akaona amepata chance ya kuwa konda, akaja huku nyuma ambapo hutumika kupandia akaungana na huyo jamaa mwenye t shirt ya mistari”
“Nikawaambia ebwana mbona mnachukua pesa pasipo kutoa tiketi wakajibu tutaenda kununua, nikawaambia yangu hamchukui bila kunipa tiket, kama unavyomuona mkononi kachukua nyingi huyo jamaa na hilo ni behewa moja nadhani na mengine ilikuwa hivyo kwa sababu kama wangekuwepo wahusika basi wangeamia letu baada ya kukatia mengine.

.

.


source:
Millard Ayo
 
Ndiyo maana hatuendelei!sasa hivi utasikia shirika limeshindwa kujiendesha!
 
Nadhani wahusika wamewaona. Kama ni wafanyakazi wa TRL, Lazima wawajibishwe; kama ni waganga njaa, watafutwe na wafikishwe mbele ya vyombo husika. Hou ni wizi 100%.
 
Hata USA ilikuwa hivyo MPAKA wakaweka CAMERA ndani ya TRENI na MAOFISA wanaovaa kiraia kukamata Makondakta WEZI
 
Hizi hujuma ni kama uongozi wa TRL wamezifumbia macho. haiwezakani treni inapakia abiria bila kuwa na ticket, au angalau mtu maalum mwenye uniform na kitambulisho anaechukua nauli. Kwa mwenendo huo hata kibaka anaweza kukusanya nauli kwenye hii treni. Kama hawana watu wakufanya hiyo kazi basi waweke utaratibu vituoni wakukusanya nauli kabla abiria hajaingia kwenye treni.
 
Wanatakiwa wavae sare zinazotambulika rasmi na wawe na vitambulisho wanavyovibandika kifuani.
 
Ndiyo maana hatuendelei!sasa hivi utasikia shirika limeshindwa kujiendesha!

Ni ulegevu wa SHERIA KAZINI; Wakiweka SHERIA kali - Kama Ukionekana Unapokea RUSHWA Unafukuzwa kazi HAPO HAPO na SIO UKIMBILIE kwenye UNION yenu na kuhamasisha KURUDI kazini

Na pia Waweka CAMERA sio kila behewa ni kuchagua randomly; Watu wa IT na MAKONDAKTA kutakuwa hakuna UHUSIANO - Hata TRENI za US kutoka GRAND CENTRAL Station to WHITE PLAINS na kwingineko ilikuwa hivyo Mpaka wakaweka SHERIA kali kwa MAKONDAKTA
 
Back
Top Bottom