Hujuma za Oxford kwenye Kamusi ya Kiswahili Sanifu

Mphamvu

JF-Expert Member
Jan 28, 2011
10,702
3,288
Kamusi hii ingali inachapichwa na Oxford Kenya, mawakala wa Oxford University Press ya Uingereza.

TUKI wenyewe wanayo Idara ya Uchapishaji pamoja na Mtambo wa kuchapisha vitabu na kamusi kadhaa kama Kamusi ya Kiingereza - Kiswahili na Kamusi ya Kiswahili - Kiingereza huandaliwa, lakini bado kazi ya kuchapisha Kamusi ya Kiswahili Sanifu inafanywa na Kampuni ya Uingereza chini ya makubaliano ya Kikoloni, ambayo yaliongezwa kinyemela wakati huu wa Uhuru.

Wakati Kamusi hii ikiwa na mauzo, labda kuliko chapisho lolote linalosimamiwa na Oxford tawi la Afrika Mashariki, gawiwo la waandikaji, yaani TUKI (sasa TATAKI) ni kiduchu sana, chini ya asilimia 20% kufikia mwaka 2013 mwishoni.

upload_2016-1-8_16-4-40.jpeg

Mkataba wa karne moja(sina hakika sana) waliosaini TUKI na Oxford uliongezwa kinyemela mwishoni miaka ya 2000 bila kuzingatia malalamiko ya wanazuoni wa Kiswahili kuhusu uhuni wa mirabaha.

Hiki ndicho kitabu kinachouza sana miongoni mwa vitabu vya Kiswahili Duniani kote, kimeandaliwa na Wana wa Mataifa haya mawili, Tanganyika na Zanzibar lakini udambwidambwi wote unaenda kwa mzungu na mshenga wake aliyeko Kenya...

Sio fedha tu, na ajira vile vile, kwani hata ukitazama orodha ya awali wa walioshiriki kukiandaa, akina sisi unatukuta kwenye utaalamu wa Kamusi tu, ila kazi zingine nyingi zimepeanwa kwa watani.

Lakini kuna na nafasi ya propaganda pia tuliyowapa bure Kenya, au niseme waliyojipa.. Ninayo nakala ya hiki kitabu ikiwa imetapakaa bendera na tamaduni za Kenya kwenye michoro mingi, naapa!

Hizi taarifa ni matokeo ya uchakataji wangu mwenyewe, uliochagizwa na taarifa nilizopewa tukiwa Darasa la Kozi ya Leksikografia na aliyekuwa Mhadhiri na Mtaalamu wa Leksikografia kutoka Idara ya Lugha ya Kiswahili na Isimu, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Marehemu Eliezar Chiduo...

aione; Bisansaba
 
Kama chura kaingia kisimani usimpige mawe ingia hukohuko mtoe asitumie maji yako! Usilalamikie pembeni wafuateni weka mada mezani
 
Mleta mada ungeweza kusaidiwa iwapo ungeamua kuandika kwa ufasaha zaidi. Hujatuma misingi ya uandishi. Mada yako haisomeki. Kimsingi, ujumbe umepotea na hili ni tatizo linalowakuta Watanzania wengi siku hizi

Ama hamtaki kuandika kwa ufasaha, na pia, mnapenda kuandika kwa madoido mengi, kwa mfano, vifupisho visivyo na maana.

Unachokipigania kingeeleweka vizuri zaidi iwapo ungejipanga vizuri zaidi ili ueleweke.
 
Mimi sio mwandishi, ni mtoa mada wa JF. Kama kuna kitu hujaelewa sema, sio uanze kusema sieleweki na kukosoa uandishi... Na mimi sitaki msaada, nataka tujadili.
 
Mimi sio mwandishi, ni mtoa mada wa JF. Kama kuna kitu hujaelewa sema, sio uanze kusema sieleweki na kukosoa uandishi... Na mimi sitaki msaada, nataka tujadili.

Mjadala wa kina hautaweza kupatikana iwapo mtoa mada haandiki kwa Kiswahili fasaha, chepesi, kinachoeleweka bila utata.

Jipange. Andika ueleweke. Kiswahili ni lugha mama, iliyokulea. Sidhani kama unashindwa kutuelewesha chanzo cha tatizo unalotaka lizungumziwe.
 
Ufasaha wa lugha hautokani na maamuzi ya mtu au taasisi, Waswahili wa Kongo Mashariki na Tanga sidhani kama wanafanana usemaji, lakini wanaelewana. Tatizo lenu ni viswahili mlivyojifunza shule kuwa lahaja sanifu ni ile na hizi zingine takataka.
Kwa taarifa yako hata Kiswahili cha Mtaani nacho ni Kiswahili, tena sahihi.
 
Wakati mwingine tujifunze kuelewa ujumbe na mleta mada alitaka kumaanisha nini lakini watu mmetanguliza makosa kwenye habari bila kuchunguza ujumbe uliomo ndani
kwa upande wangu sio mtaalamu wa kiswahili ila nimeelewa ujumbe wa mleta mada
 
Back
Top Bottom