Hujuma ya necta dhidi ya waislamu

makwesa

Member
Jun 17, 2012
48
4
nadhani hakuna asiyefahamu kuwa sasa waislam wanapigana kulipinga kwa kile walichofanyiwa ktk somo la islamic knowledge,hivyo kufikia uamuzi kutofanya mtihani mpaka livunjwe,mimi cdhani km hii ni haki kwani hawapaswi kusahisha mitihani kwa mujibu wa dini ya mtu
 
nadhani hakuna asiyefahamu kuwa sasa waislam wanapigana kulipinga kwa kile walichofanyiwa ktk somo la islamic knowledge,hivyo kufikia uamuzi kutofanya mtihani mpaka livunjwe,mimi cdhani km hii ni haki kwani hawapaswi kusahisha mitihani kwa mujibu wa dini ya mtu

Naomba nikuulize,
Je Islamic Knowledge ina mchango gani katika career za wanafunzi? Je inachangia vipi katika kuendelea kusoma masomo ya mbele.
 
Nawashauri waisilamu wagome kufanya tena somo la islamic knowledge
 
hivi ndugu zetu mtakuwa na maamuzi ya ajabu mpaka kalne ipi? gomeni ss bibleknowledge twa fanya kama kawa,mbona umeshaelezwa tatizo na necta!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
kama lingekuwa hali umuhimu wacngekata kwa makusudi,na km amujui umuhimu wake kwanza uhesabiwa km somo lingine hivyo ikitokea somo lingine umefeli islamic linareplase na ktk kujaza tcu zinakiwa 2 plinciple haijalishi somo gani.
 
nadhani hakuna asiyefahamu kuwa sasa waislam wanapigana kulipinga kwa kile walichofanyiwa ktk somo la islamic knowledge,hivyo kufikia uamuzi kutofanya mtihani mpaka livunjwe,mimi cdhani km hii ni haki kwani hawapaswi kusahisha mitihani kwa mujibu wa dini ya mtu

jamani unajua kukosa uelewa wa mambo ni kubaya sana tena sana. Istoshe pia kuwa na uhakika na unachokifanya ni kosa jingine baya zaid kuliko hata la kutokuwa muelewa. labda ndugu zangu tujiulize haya maswali:-
a) mitihani ya baraza inatugwaga na nani?
b) nani anayeifanyia moderation?
c) nani anaye ichapa?
d)nani anaye ifanya?
e)nani anyesahihisha?
f)nani anyetangaza matokeo.

nianze kujibu swali moja baada ya jingine
a) mtunzi wa mtihani wowote ni waalimu wa somo husika. kwenye hii ya kitaifa waalim walioteuliwa hupeleka maswali tena moja moja au hata mawili. haya hukusanywa na baraza la mitihani. so wao wanapokea maswali kulingana na jinsi yanavyotakiwa kwamba yawe na qualities zinazopima 5 bloom's taxonomy of hierarchy. kwa jinsi mwalimu alivyoagizwa na mwalimu huyu lazima awe ni mwalimu wa somo husika tu.


b) moderation, wanaofanya kazi ya kumoderate na kuuandaa mtihani uwe kama mtihani sasa ni baraza lenyewe chini ya majopo husukia ya academician ambao ni qualified kwa ajilia ya masomo husika. hawa huchambua maswali yote vizuri kisha hupata maswali yanayotakiwa kwa kufuata hizo 5 blooms taxonomy kisha hutengeneza table of specifications juu ya mtihani husika.

c) nani anayeuchapa mtihani ni baraza lenyewe, ila proof reading inafanywa na jopo husika lililotumika kufanya moderation ya somo husika.

d) anayefanya mtihani ni mwanafunzi husika wa somo lenyewe. na hapa ni yule aliye jiandikisha kufanya mtihani huo na s vinginevyo

e)msahihishaji wa mtihani huu huwa ni waalim husika waliopendekezwa na shule zao ambao ni wa masomo husika na hwa wakifika kwenye ushaihishaji huandaa kama jopo marking scheme ya mtihani husika kabla hata ya kushika hizo karatasi za wanafunzi kuanza kusahihsha. kwa kua ndio subject experts basi hutakiwa kuandaa marking scheme kwa umakini mkubwa sana na kamwe huwez kukuta mwl wa hesabu ameandaa ya kiswahili. Baada ya hapo husahihisha mtihani husika kisha pitiwa tena kuhakiki kama wamesahihisha kihalali na hapa kwenye jopo waweza kuta kila mwana jopo anasahihisha kaswali kamoja tu na ndivyo ilivyo.

f) anayecompile matokeo na kutangaza ni baraza.

baada ya kuyafafanua hayo naomba niseme kuwa matatizo yaliyojitokeza kwenye mtihani wa dini wa kiislamu ulitokana na watunzi wenyewe ambao ni waalim wa somo husika na pia wasahihishaji ambao ni waalimu wa somo husika. kwanini nasema hayo inamaana waali walitunga ntihani ambao haukuwa sawa kwa anafunzi na mwenye uhakika wa mwanafunzi huyuatamudu kufanya mtihani huu ni mwalimu wala siyo chombo kinachoratibu. kufeli kwa wanafunzi kunatokana na ukweli kwamba mtihani ulikuwa mgumu terminologies za kiarabu kwenda kiingereza ni utata mtupu yaani kiingereza abda utumie kamusi ya kiarabu halafu leo wanamlaumu Dr Ndalichako lolz siwaelewi kwa kweli.
 
umejitahid sana kufafanua bt umeshindwa kuilewa ishu mzima jinsi ilivyo,ni hivi matokeo yaliyotangazwa ni tofauti na matokeo halisi na imegundulika baada ya wahusika kukuwa na imani na matokeo na kuiandikia barua necta na kukiri kosa baada ya uchunguz na kutoa matokeo mengine ambayo ni mazuri tofauti na mwanzo kuumfukuza kazi msimamiz kuyaingiza kwenye kompyuta, lakini waislamu wanahoji kwa nini iwe islamic na sio masomo mengine? tatizo ni hilo na siyo uliyoelezea.
 
umejitahid sana kufafanua bt umeshindwa kuilewa ishu mzima jinsi ilivyo,ni hivi matokeo yaliyotangazwa ni tofauti na matokeo halisi na imegundulika baada ya wahusika kukuwa na imani na matokeo na kuiandikia barua necta na kukiri kosa baada ya uchunguz na kutoa matokeo mengine ambayo ni mazuri tofauti na mwanzo kuumfukuza kazi msimamiz kuyaingiza kwenye kompyuta, lakini waislamu wanahoji kwa nini iwe islamic na sio masomo mengine? tatizo ni hilo na siyo uliyoelezea.

kama ni mfuatiliaji, swali lako lilishajibiwa na Waziri Kawambwa kwenye mkutano wake na waandishi wa habari, kimsingi majibu Waziri yanaeleweka na uzuri tatizo liligundulika na kupatiwa ufumbuzi mapema, kila mmoja kapata haki yake.
Haya maswali ya kwa nini kwa sasa sidhani kama yana umuhimu tena.
 
umuhimu upo kwani kwa taarifa nilizopata hata hayo matokeo yaliyotolewa kwa mara ya pili cyo sahihi na haijulikani yametolewa wapi
 
umejitahid sana kufafanua bt umeshindwa kuilewa ishu mzima jinsi ilivyo,ni hivi matokeo yaliyotangazwa ni tofauti na matokeo halisi na imegundulika baada ya wahusika kukuwa na imani na matokeo na kuiandikia barua necta na kukiri kosa baada ya uchunguz na kutoa matokeo mengine ambayo ni mazuri tofauti na mwanzo kuumfukuza kazi msimamiz kuyaingiza kwenye kompyuta, lakini waislamu wanahoji kwa nini iwe islamic na sio masomo mengine? tatizo ni hilo na siyo uliyoelezea.

Waziri wa Elimu Mh. Shukuru Kawambwa alitoa ufafanuzi, Namnukuu:
"Baada ya kupitia hatua za uhakiki kuhusu usahihishaji na utoaji wa matokeo, ilibainika kuwa alama za mwisho katika somo la Islamic Knowledge zilizokokotolewa na Mfumo wa Kompyuta ZILITOFAUTIANA na alama zilizopatikana kwa kutumia kikokotozi. Uchunguzi zaidi uliofanyika kwa lengo la kubaini chanzo cha tatizo katika uchakataji wa matokeo hayo
kwenye Mfumo wa Kompyuta ulionesha kuwa uchakataji uliotumika awali kutoa matokeo ya mwaka 2012 ulitumia jumla ya "Paper" tatu kama ilivyokuwa mwaka 2011.

"Kutokana na mabadiliko ya Fomati ya Mtihani wa somo la Islamic Knowledge yaliyoanza kutumika rasmi katika Mtihani wa Kidato cha Sita 2012, mtihani huo kwa sasa una "paper" mbili na siyo "paper" tatu. Hivyo, tofauti ya alama iliyobainika imetokana na Mfumo wa Kompyuta kuendelea kutumia "paper" tatu katika kupata wastani wa alama za mwisho badala ya kutumia "paper" mbili."

Waziri anaongeza:
Viongozi wa Baraza la Wakuu wa Shule za Kiislamu waliridhika na hatua zilizochukuliwa na Wizara na wameandika barua ya kuishukuru Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuhusu namna walivyoshughulikia malalamiko yao.

Nini hakieleweki hapo?

Format ya Islamic Knowledge imebadilika mwaka huu na kuwa na paper mbili badala ya tatu. Masomo mengine yote formats hazikubadilika. Ndio maana matatizo yametokea kwenye somo hilo tu.

Human error iliyokuwepo ni kujisahau kubadili formula ya kukokotoa wastani kwenye program ya computer ili igawanye kwa 2, ikabaki kama zamani kugawanya kwa 3.

Tamko la Mh. Shukuru Kawambwa naliambatanisha hapa.
 

Attachments

  • IslamicstudiesFinal1.pdf
    201.6 KB · Views: 85
umuhimu upo kwani kwa taarifa nilizopata hata hayo matokeo yaliyotolewa kwa mara ya pili cyo sahihi na haijulikani yametolewa wapi
Wewe mzushi.

Tamko la Waziri Kawambwa linasema:

Viongozi wa Baraza la Wakuu wa Shule za Kiislamu waliridhika na hatua zilizochukuliwa na Wizara na wameandika barua ya kuishukuru Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuhusu namna walivyoshughulikia malalamiko yao.
 
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA

WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI

TAMKO LA SERIKALI KUHUSU MALALAMIKO DHIDI YA MATOKEO YA SOMO LA ISLAMIC KNOWLEDGE KATIKA
MTIHANI WA
KIDATO CHA SITA 2012


1.0 UTANGULIZI

Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha sita 2012 yaliyotangazwa rasmi tarehe 01/05/2012. Tarehe 28/5/2012 Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ilipokea barua kutoka Baraza la Wakuu wa Shule za Kiislamu yenye Kumb. Na. BSK/W/012/01 ya tarehe 22/5/2012 iliyoeleza kutoridhika na ufaulu wa watahiniwa waliofanya somo la Islamic Knowledge kwa kuwa waliona matokeo yaliyotangazwa hayakuwa na uhalisia wa uwezo wa wanafunzi. Kutokana na barua hiyo, Serikali ilifanya uchunguzi kwa kuangalia mambo yafuatayo:

. Kulinganisha alama za watahiniwa zilizojazwa katika vituo vya usahihishaji mitihani na zile zilizohifadhiwa katika Kompyuta, yaani database ya Baraza la Mitihani ili kubaini kama kuna tofauti yoyote; na

. Kulinganisha alama za somo la Islamic Knowledge zilizochakatwa na Mfumo wa Kompyuta na sampuli ya alama zilizokokotolewa kwa kutumia kikokotozi (calculator).


2.0 MATOKEO YA UCHUNGUZI
. Baada ya kupitia hatua za uhakiki kuhusu usahihishaji na utoaji wa matokeo, ilibainika kuwa alama za mwisho katika somo la Islamic Knowledge zilizokokotolewa na Mfumo wa Kompyuta ZILITOFAUTIANA na alama zilizopatikana kwa kutumia kikokotozi. Uchunguzi zaidi uliofanyika kwa lengo la kubaini chanzo cha tatizo katika uchakataji wa matokeo hayo kwenye Mfumo wa Kompyuta ulionesha kuwa uchakataji uliotumika awali kutoa matokeo ya mwaka 2012 ulitumia jumla ya "Paper" tatu kama ilivyokuwa mwaka 2011.

. Kutokana na mabadiliko ya Fomati ya Mtihani wa somo la Islamic Knowledge yaliyoanza kutumika rasmi katika Mtihani wa Kidato cha Sita 2012, mtihani huo kwa sasa una "paper" mbili na siyo "paper" tatu. Hivyo, tofauti ya alama iliyobainika imetokana na Mfumo wa Kompyuta kuendelea kutumia "paper" tatu katika kupata wastani wa alama za mwisho badala ya kutumia "paper" mbili.


3.0 HATUA ZILIZOCHUKULIWA NA SERIKALI
. Baada ya kugundua dosari hiyo kwa somo la Islamic Knowledge, uhakiki ulifanyika kwa masomo yao yote ya Mtihani wa Kidato cha Sita 2012 yaliyokuwa na "paper" zaidi ya moja ili kujiridhisha endapo uzito sahihi ulitumika katika kupata wastani wa alama za watahiniwa. Matokeo ya uhakiki huo yalionesha kuwa alama sanifu zilizokokotolewa na mfumo wa kompyuta ni sawa na alama zilizokokotolewa na Kikokotozi. Hivyo hakuna dosari yoyote iliyobainika katika masomo mengine.

. Matokeo ya somo la Islamic Knowledge yaliyotangazwa awali yamerekebishwa kwa kutumia Paper mbili kama inavyotakiwa ili kuendana na mabadiliko ya Fomati ya somo hilo. Marekebisho hayo yaliridhiwa na Baraza la Mitihani katika Kikao chake Maalum kilichofanyika tarehe 31/05/2012.

Aidha, Kikao kati ya wajumbe wa Baraza la Mitihani na wawakilishi wa Baraza la Wakuu wa Shule za Kiislamu kilifanyika tarehe 31/05/2012 ambapo walielezwa kuwa Wakuu wote wa Shule wenye watahiniwa waliofanya somo la Islamic Knowledge wataandikiwa barua rasmi kufahamishwa kuhusu marekebisho yaliyofanyika na barua hizo ziliandikwa tarehe 01/06/2012. Pia walifahamishwa kuwa matokeo yao yote ya masomo mengine hayana dosari yoyote na yanabaki kama yalivyotangazwa na Baraza la Mitihani la Tanzania. Matokeo hayo yamewekwa kwenye tovuti ya Baraza la Mitihani na pia yatatangazwa kwenye magazeti.

. Pamoja na marekebisho hayo, Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi itaunda Kamati ya wataalamu kuiwezesha serikali kujiridhisha zaidi na hatua zilizochukuliwa na Baraza la Mitihani ili kuepuka dosari ya aina hiyo isijitokeza tena kwa siku zijazo.

. Viongozi wa Baraza la Wakuu wa Shule za Kiislamu waliridhika na hatua zilizochukuliwa na Wizara na wameandika barua ya kuishukuru Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kuhusu namna walivyoshughulikia malalamiko yao.


4.0 HATMA YA WANAFUNZI WALIOREKEBISHIWA MATOKEO KATIKA MAOMBI YA KUJIUNGA NA VYUO VIKUU

Wizara inapenda kuwahakikishia watahiniwa waliorekebishiwa matokeo yao kwamba, kwa kuwa zoezi la usajili bado linaendelea hadi tarehe 30/06/2012, waliorekebishiwa matokeo yao watapata fursa ya kuwasilisha maombi ya kujiunga na vyuo vikuu endapo wana sifa stahiki. Aidha, kwa upande wa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, maombi ya mikopo hufanyiwa kazi rasmi baada ya Tume ya Vyuo Vikuu kukamilisha mchakato wa udahili wa wanafunzi wa elimu ya juu. Hivyo, hapatakuwa na athari yoyote kwa watahiniwa husika kupata mikopo endapo watakidhi vigezo vinavyotakiwa.

5.0 HITIMISHO
. Napenda kuhitimisha kwa kuwasihi wazazi, walezi, wanafunzi na jamii kwa ujumla kuwa na imani na Baraza la Mitihani la Tanzania kama chombo chetu chenye dhamana kisheria ya kuendesha mitihani nchini.
Hapakuwa na hujuma yoyote iliyofanyika kwa watahiniwa ambao matokeo yao yamerekebishwa. Kosa lililojitokeza ni la kibinadamu, halikufanywa kwa makusudi wala kwa lengo lolote la kuhujumu kundi fulani la watahiniwa. Marekebisho yameshafanyika na matokeo stahiki yameshatolewa. Aidha, uhakiki uliofanyika kwa masomo yao mengine unaonesha kuwa hakuna dosari yoyote iliyobainika katika masomo yote.
. Kutokana na dhana ya baadhi ya watu kuwa kunakuwa na upendeleo kwa baadhi ya watahiniwa wa makundi fulani katika usahihishaji napenda kuwakumbusha kuwa wakati wa mitihani, watahiniwa huandika namba zao za mitihani na siyo majina. Katika taratibu za usajili wa Baraza la Mitihani hakuna kipengele chochote kinachomtaka mtahiniwa kuonesha kabila yake, dini au itikadi ya kisiasa. Vilevile, utaratibu unaotumika kuwapata wasahihishaji huzingatia uwezo wao kitaaluma na uzoefu kazini.

Aidha, katika fomu ya mapendekezo ya uteuzi wa wasahihishaji hakuna mahali popote ambapo Mkuu wa Shule hutakiwa kuonesha kabila yake, dini au itikadi ya kisiasa ya mwalimu anayependekezwa kusahihisha mitihani.


. Utaratibu unaotumika kusahihisha mitihani hautoi mwanya wa upendeleo. Katika kudhibiti uwezekano wa kupendelea mtu yeyote kila msahihishaji husahihisha swali moja tu na kisha humpatia msahihishaji mwingine asahihishe swali linalofuata. Aidha, kila msahihishaji hutakiwa kuweka vifupisho vya majina yake (initials) ili ufuatiliaji uweze kufanyika kadri itakavyohitajika. Pia uhakiki wa usahihishaji hufanyika kwa lengo la kujiridhisha na usahihi wa kazi na kuhakikisha kuwa kila mtahiniwa amepata alama anazostahili. Dosari zinazobainika zimekuwa zikirekebishwa katika mchakato wa usahihishaji na wasahihishaji wanaobainika kuhusika na dosari hizo wamekuwa wakichukuliwa hatua stahiki mara zinapobainika.

. Pamoja na hayo niliyoyaeleza nina taarifa kuwa yanapangwa maandamano ambayo yanalenga suala hili hili la kutoridhika na matokeo ya awali ya somo la Islamic knowledge. Kwa kuwa suala hili limeshapatiwa ufumbuzi, nawasihi wananchi wajiepushe kushiriki maandamano hayo kwa sababu suala la msingi lililo wafanya watake kuandamana limeshatolewa maelezo. Hivyo, maandamano hayo hayatakuwa na tija.


IMETOLEWA NA DKT SHUKURU JUMANNE KAWAMBWA


WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI


TAREHE 07/06/2012
 
Kwani tatizo si lishasulihiswa na waziri ameshatoa tamko,na viongozi wa shule za kiislam si wamesharidhia.Sasa iweje hadi leo mnatuletea sredi hizi?
 
Naomba nikuulize,
Je Islamic Knowledge ina mchango gani katika career za wanafunzi? Je inachangia vipi katika kuendelea kusoma masomo ya mbele.
na ile bible knowledge in a faida gani, think twice!
 
Naomba nikuulize,
Je Islamic Knowledge ina mchango gani katika career za wanafunzi? Je inachangia vipi katika kuendelea kusoma masomo ya mbele.
Inasaidia kuleta viongozi bora na sio mafisadi?
 
Mbona sijaona course ya chuo chochote kati ya vyuo vikuu inayohitaji pass ya somo la dini? Wapeni A wote.
 
Back
Top Bottom