HUJUMA kwa Siyoi.. Hujuma kwa Chama | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

HUJUMA kwa Siyoi.. Hujuma kwa Chama

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by Eng. Y. Bihagaze, Mar 20, 2012.

 1. Eng. Y. Bihagaze

  Eng. Y. Bihagaze Verified User

  #1
  Mar 20, 2012
  Joined: Sep 8, 2011
  Messages: 1,481
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 145
  Mzee
  Najua huwa unapitia hapa ukikwanguiwa kule Facebook, au "mtuitui" anakujuza yanayoendelea, ila mchunge sana, ni mnafiki huwa anakumwagia porojo na umbeaumbea tu sanasana siku akiwa anasaka pesa za kujirusha. Si unajua ulipokuwa Botswana ukajizolea vikinda viwili ukaruka navyo Kilimanjaro kufanya "pandamlima tisha toto" na baadae "kuleee", kumbuka naye alichota kile kimoja. Nakwambia mpaka leo hakijarudi Botswana, kakisweka mahala.. fact, mie sichapi umbea ..manake hawachelewi sema weka source.. source si ndio hii hapa au wewe unataka ipi tena..we-mbaba unamambo..!!

  Mzee unakumbuka kilipotemwa kikao cha KK cha mwisho na kwa rungu tukagandamizia Siyoi for Arumeru, Siyoi for the Party, na baadae ukapokea msg kutoka kwa "kiraka" kwamba mc alikuwa anachonga mbovu nje ya kikao kwamba kwa mtaji huu ni bahati kushika nafasi ya pili au tatu kwa chama letu kwenye kinyang'anyiro hicho cha Ubunge, huko kwa wameru kutokana na sababu walizozungumzia zungumzia wajumbe za vijiubabevijiubabe na kama kuburuzana flan-hivi, dhana iliyotokea kule Dodoma wakati wa kupitisha ile karata ya mabadiliko ya katiba ......... ila ukapuuzia kamsemo kake, nadhani sasa kuna sababu ya kuanza Tathimini kwanini Tumeshindwa.

  Werevu hawasubiri mavuno ndipo wafanye tathimini, wapumbavu husubiri hadi nukta ya mwisho ya tone la mvua ndipo huamka kwamba mwaka huu ni wa njaa na kukurupuka kuomba msaada.


  Kuna Uzi unatembea Chini kwa Chini wa Kukiangamiza Chama, ni HUJUMA iliyokamilika yenye Lengo la Kukomoana na kulipizana Visasi. Ukweli usemwe hata kama unauma.. look here..

  1.
  Wakati Benja akifungua kampeni, kule Igunga alielezea kwa madaha jinsi Serikali kupitia chama letu ilivyoleta maendeleo ya miundombinu ya Barabara, Toka Dar hadi Igunga ni lami, Chama letu limefanikisha kufungua matawi ya benki (NMB) Igunga ambapo sasa wananchi wanaweza kukopa na kuweka vijisenti-pesa vyao akaenda-mbali na kusema atahakikisha wanajengewa daraja la Mbutu, matamshi yaliyoleta mashiko kwa wakaazi wa Huko.. tofauti na matamshi aliyoendanao Arumeru mashariki, Benja katumia muda mwingi akijisafisha mwenyewe mbele ya jamii ya wameru na watanzania kwa ujumla kwamba hahodhi ardhi kubwa kama "inavyosemekana" (sijui inasemekana wapi maana mwoga hukimbia hata kivuli chake), lakini pia akaeleza anayo orodha ya watu waliokwiba ardhi na ataipeleka kwako ili uwashughurikie. (kha sasa orodha inapelekwa kwa rais?

  Yeye Benja kaipatawapi orodha, Kumbe kuna watu wamekwiba ardhi na yeye anawatambua ila kawakumbatia hadi Leo sa ya kampeni.. hivyo kusingekuwa na kampeni ina maana wangekumbatiwa forever, kama kwenye jimbo moja ana uwezo wa kukumbatia uhaini na Uhalifu(ukabaila) mkubwa kiasi hiki je Tanzania Yote mbaba huyu kakumbatia mangapi??!!) hoja hii mzee ni kama kuishtaki serikali mbale ya wananchi wake kwamba inajua matatizo yao ila kwa maksudi imekumbatia wahalifu na haitaki kuwasaidia wananchi wake. Akaenda mbali kwa kwa kutamka kwamba kiongozi mmojawapo wa kambi ya chama cha upinzani, ambaye ni kiungo muhimu kwanye kampeni za chama chake huko Arumeru si mwana ukoo wa Juliasi ..

  Alifanya hivyo maksudi kwa sababu yeye anamjua Vicent, (tena wanajuana fika sitaki niseme zaidi) .. sasa kuropoka mbele ya wananchi waziwazi vile analenga kuwaamsha watanzania Juu ya Ule uvumi ambao Chama kilitumia Nguvu Nyingi sana Kuufukia. Na Uvumi huu ameshauchokonoa na umefunuka sasa, unadhani utauzibaje.. ?? sasa kama hii si hujuma wewe Utaiitaje.?

  Waandishi wa habari wakim-mwagikia mama Maria , na kumchabanga maswali bibi yetu huyu atajikuta akiongea mambo ambayo chama hakitayabeba siku za Usoni. Tunaweza tukamlinda kwa sasa ila hatujui siku chama letu likipewa talaka na Watanzania, kichwa kitakachoshika dola hatujui kitaamua nini, jamaa wanaweza kumwita bibi ili wamhoji "on Public devote" na akasema kila kitu, unadhani utakuwa wapi wewe.. ona Juzi kati bibi kamtetea Benja kwamba hakumuua Juliasi, na kwamba yeye bibi anajua SIRI, sasa hilo ni swali la Pili, siri gani bibi yetu huyu amejikunjia.. watanzania watataka aiweke wazi, hapo.. ???!! kwa Kweli mzee Benja Katumaliza...


  2.
  Kingine Ratiba anaichakachua Sana mwigulu huyu bwana, mtu mbishi na mgomvi sijapata ona .. watu hawa wana Lao mzee, Kumbuka vikao kadha na masimu kadha wa kadhaa yalitembea usiku kucha kutuliza mashambulizi haya, na tukaazim Mzee Tendwa kwa Rungu alilopewa akemee Kumtamka Marehem Juliasi kwenye kampeni Hizo, But see what happens,Stephen kwa majigambo nae karudia kauli ile le tuliyoikataa, kwamba Nyerere hayuko Upinzani, yeyote aliyeko Upinzania sio Nyerere hata kama katokea ukoo wa Juliasi, wamkatae.. sasa anachokifanya hapa ni kumwagilia zaidi mbegu ile tunayotaka ilale.

  Alipoulizwa na Tendwa kwa ubabe alijibu yeye ni wa ukoo wa Julias ingawa kwa barua hivyo hakuna kinachomzuia kuongelea juu ya ukoo uliomkubali awe mtoto (ngawa wa mbali-kambo). Stephen ameenda mbali na kuzua hoja ya Uraia wa Siyoi. Sasa ndio amewaamsha wananchi na waliodhani ni uvumi kumbe ni kweli hakuzaliwa kwenye ardhi ya Tanzania, jambo ambalo limezua mstuko wa wananchi wengi hapa. Akasema Siyoi amezaliwa Kenya kwa sababu wazazi wake walikuwa wanaishi na kufanya kazi huko, jambo ambalo tena limewastua sana wananchi ambao awali walijua ni uzushi.

  Maneno haya yana maana kwamba damu ya kitovu cha sioi haikumwagika kwenye ardhi ya Meru, hivyo hawezi akawa na uchungu na ardhi ambayo haina damu yake, kitu ambacho kwa wameru na wazee wa kimila ni mwiko. Amamtukanisha waziwazi mgombea kwa ukoo wake.

  Sendeka nae kaja na Gia ya Ubaguzi wa kikabila kwamba watu wa Musoma(Mara) wasiwachagulie nani anafaa nani hafai maneno ambayo unakumbuka kwenye kinyang'anyiro cha kugombea urais, 1995, Marehem alikataa kukanyaga zuria la ukumbi mpaka majina kadhaa ya wagombea yaondolewa, na kijivurugu kikatokea na mmoja wa wagombea akaropoka "huyu mtu wa mara akakae butiama apumzike asituchagulie nani anafaa nani hafai kwani sisi hatuna akili", .. na kamsemo hako kamerudia kinywani mwa Ole sendeka!! Kuna Jambo hapa mzee, ni HUJUMA inatembea..

  Lusinde na Ole sendeka wameng'ang'ana mpeni kura Siyoi atunze familia kubwa aliyobebeshwa na Babake. Huu ni Upuuzi, yaani Mzee wa watu alikuwa akirundika watoto kwa mategemeo kwamba watalelewa na Mwanae. Huu mtindo wa kumfanya mtoto kuwa mtaji ulianza wapi.. matamshi haya yana lengo la kuidharau, kuinyanyapaa Familia hiyo ya marehem mbunge wetu kwamba ina njaa, na isipopewa kudra ya mtoto kuwa mbunge basi ndo imekwisha hivyo, lakini pia ni ujumbe kwamba kama uko kwenye Chama letu, na Ukapatwa na Umauti, basi na jina lako linafutika na Chama hakikujui tena hivyo ili kuonekana chama kinajali basi afadhali member mmoja wa familia husika aendelee kuwa kiongozi.. aise Karume, Ali mwinyi, Nape, shelu nk pokeeni msg hiyo.

  Hii yote ni Hujuma. Kuhusu Mgombea Siyoi , Ingawa hajui kuongea, na anaonekana mwenye aibuaibu, anaongea akitazama juu, akisimama kuzungumza mara nyingi anaongelea mambo ambayo nadhani ilimchukua usiku kucha kuyakariri na mara zote anakosea, mara mradi wa maji unaoanzia ngarenanyuki, badala ya kusema unatokea ngarenanyuki(manake upo), unasimamiwa na NEMCO (mazingira)na pia kasema wanangojea kibali cha TANAPA waendelee na mradi, wakati ambapo TANAPA hawatoi kibali cha maji bali wanaruhusu tu mradi upite kwenye hifadhi ndogo ya Arusha National Park, ambapo MT Meru upo, na si kwamba kuna mazingira yatakayoathirika kwa sababu mradi unapita kandokando ya barabara ambayo ipo toka zamani..

  Anyway ingawa mgombea anajiumauma meno ila anajikakamua kuelezea hasa kile ambacho wananchi wanakitaka. Ila anvunjwa moyo na Timu yake inayosheheni maneno yenye kila viashirio vya kumuhujumu yeye na Chama kwa Ujumla..  mie niwakilishe..
   
 2. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #2
  Mar 20, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Duuuuh watu kama nyie ndiyo mnaoifanya JF iwe juu siku zote. Kifupi baba umetambaa na rula balaa.
   
 3. Kurunzi

  Kurunzi JF-Expert Member

  #3
  Mar 20, 2012
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 4,006
  Likes Received: 328
  Trophy Points: 180
  Kiukweli sijakusoma kabisa.
   
 4. Kingo

  Kingo JF-Expert Member

  #4
  Mar 20, 2012
  Joined: May 12, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 153
  Trophy Points: 60
  Good comment
   
 5. Mzee wa Rula

  Mzee wa Rula JF-Expert Member

  #5
  Mar 20, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 8,177
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Wapi hujamsoma au kote hujaelewa kabisa? Mkuu huju Salma2015 ameandika vizuri sana na ningetamani Nape aje asome aone nini cha kufanya maana jamaa japokuwa kaweka kama tetesi lakini kuna element ya ukweli by 75%.
   
 6. DSN

  DSN JF-Expert Member

  #6
  Mar 20, 2012
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 2,745
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Du umemkaanga jamani na wanaccm umewakaanga!!!!!!!!Inatia shaka kwa tafsiri ya kila mmoja ndani ya CCM kweli zinaonekana kama ziko kihujuma hujma vile.Lakini yote tisa ccm wanajua ngoma wanayoicheza!!!!!!!!Ila iko kazi!!
   
 7. MAMA POROJO

  MAMA POROJO JF-Expert Member

  #7
  Mar 20, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 4,966
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 135
  sijakusoma kabisa labda ulidhamiria tusipate ujumbe uliotaka kutueleza.

  waliomuelewa endeleeni mimi najitoa.
   
 8. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #8
  Mar 20, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Sijaielewa ngoja nisome tena kwa vituo...
   
 9. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #9
  Mar 20, 2012
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,474
  Likes Received: 4,134
  Trophy Points: 280
  Kumbe tupo wengi ambao hatujaelewa, mimi nakomaa nayo hadi nipate ujumbe.
   
 10. N

  Nteko Vano JF-Expert Member

  #10
  Mar 20, 2012
  Joined: Feb 28, 2012
  Messages: 436
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Nakubaliana na wewe. Inaonekana bora liende.
  Pia siri aliyokuwa mama Nyerere ni ya wahusika wakuu, muuaji sio BEN ila alishindwa kuzuia hilo ndio lawama zake.
   
 11. Adrian Stepp

  Adrian Stepp Verified User

  #11
  Mar 20, 2012
  Joined: Jul 1, 2011
  Messages: 2,222
  Likes Received: 596
  Trophy Points: 280
  Ama kweli kuchelewa kufa ndio kuona mengi..kwahiyo huyo bwana asie oa anapakwa mafuta kwa mgongo wa chupa tu sio??
   
 12. Prishaz

  Prishaz JF-Expert Member

  #12
  Mar 20, 2012
  Joined: Nov 18, 2011
  Messages: 1,931
  Likes Received: 1,465
  Trophy Points: 280
  Mbona anaeleweka vizuri sana?tulia usome tena,Kimsingi mleta thread umeeleza vema kinachoonekana kiko nyuma ya pazia na ambacho Siyoi hakijui! Na kwa mtazamo huu nami naona ni ukweli usiopingika,hawa wanaomnadi ni bora liende! Huwezi mnadi mgombea kwa kutaka aonewe huruma eti kaachiwa familia kubwa inahitaji matunzo!dirty politics
   
 13. K

  Kaseisi Member

  #13
  Mar 20, 2012
  Joined: Mar 6, 2012
  Messages: 99
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Mwenye masikio na asikie, waliomfikisha hapo Sioi sasa wamemuacha katika mikono ya wagalatia na wao kubaki wakizunguka makanisani
   
 14. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #14
  Mar 20, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Mtaelewa tu habari ndiyo hiyo.
   
 15. L

  Lyabangi Member

  #15
  Mar 20, 2012
  Joined: Mar 1, 2012
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuchelewa kuoa,na kuoa ovyo ovyo kp bora,mwenyekiti wenu anaoa2 kila kukicha c ni upuuzi huo
   
 16. Mwanajamii

  Mwanajamii JF-Expert Member

  #16
  Mar 20, 2012
  Joined: Mar 5, 2008
  Messages: 7,080
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 0
  Umemaliza kazi kachukue posho yako pale KINONDONONI mtaa wa UFIKA NA TOGO
   
 17. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #17
  Mar 20, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Kwa kifupi mwandishi anaelezea sabotage inayofanywa na timu ya kampeni, wewe mtu anasema mchagueni ili asaidie familia inaingia akilini kweli si kuwatia hasira wananchi wenye familia zao, mwingine anasema hatutaki watu wa Mara watuchangulie wakati Wassira naye ni wa huko huko, mwingine anazidi kupigilia msumari kwenye kidonda cha Mkapa na VN hizo zote hamuoni kuwa ni hujuma. Lakini kama mtu umekunywa maji ya bendera ni vigumu sana kuona kama hizi ni hujuma.
   
 18. n

  nketi JF-Expert Member

  #18
  Mar 20, 2012
  Joined: Feb 15, 2012
  Messages: 555
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Ccm chama cha kinafiki na wanafiki wote wamejaa huko........hakuna mwenye uchungu na nchi hii kutoka ccm...........wote ni walewale hata aje nani...........wote ni chukua chako mapema (ccm)
   
 19. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #19
  Mar 20, 2012
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Kuhusu kifo cha Mwalimu: kusema kweli kitakitikisa chama lenu jkisawsawa. soma gazeti la leo la JAMHURI lina habari nzito. Mmoja wa wahariri wa gazeti hilo ni Manyerere Jackton, kutoka ukoo wa Nyerere kwa mbali na aliyelelewa na Juliasi.

  Pili Makongoro yuko kimya katika hili, bila shaka kutokana na wadhifa wake alio nao katika chama. Madaraka ndiyo amewahi kuzungumza kuhusu hilo ingawaje hakuenda kiundani.
   
 20. S

  Skillionare JF-Expert Member

  #20
  Mar 20, 2012
  Joined: Nov 6, 2011
  Messages: 1,158
  Likes Received: 35
  Trophy Points: 145
  Sioi kushinda arumeru ni ndoto..
   
Loading...