Hujuma kutoka NEC kwa nchi yetu! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hujuma kutoka NEC kwa nchi yetu!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by MTWA, Oct 26, 2010.

 1. MTWA

  MTWA JF-Expert Member

  #1
  Oct 26, 2010
  Joined: Aug 5, 2009
  Messages: 1,026
  Likes Received: 53
  Trophy Points: 145
  Kuonesha kuwa NEC siyo chombo huru na ni part ya CCM tulitazame hili kutoka Chanzo cha NIPASHE newas paper!
  Ni kutokana na vurugu za Maswa
  [​IMG]
  Shibuda, mgombea CCM waachiwa
  [​IMG] DCI Manumba asema hana hatia


  Tume ya taifa ya uchaguzi (NEC).  Chama Cha Demokrasia na Maedeleo (Chadema) kiko hatarini wagombea wake wa ubunge na udiwani kuenguliwa katika Jimbo la Maswa Magharibi katika Uchaguzi Mkuu utakaofanyika Jumapili kutokana na kuhusishwa na vurugu zilizotokea wiki iliyopita na kusababisha kifo cha mtu mmoja.
  Tishio la wagombea wa Chadema kuenguliwa linatokana na Kamati ya Maadili ya Uchaguzi ya Jimbo la Maswa Magharibi kupendekeza wagombea wa Chadema waenguliwe kwa madai ya kuwa chanzo cha vurugu hizo.
  Msimamizi wa Uchaguzi wa Wilaya ya Maswa, Magharibi Elizabeth Kitundu, alisema jana kuwa kamati hiyo ilikutana Jumamosi iliyopita kujadili hoja ya kuwaengua wagombea wa Chadema kushiriki katika uchaguzi.
  Kitundu alisema kuwa tume hiyo imepeleka mapendekezo hayo kwa Kamati ya Maadili ya Uchaguzi ya Tume ya taifa ya uchaguzi (NEC).
  Aliongeza kuwa Chadema nao tayari wamepeleka barua ya kujitetea kupinga kuenguliwa katika uchaguzi huo. Hatua ya kamati hiyo inadaiwa kuchukuliwa kufuatia vurugu zilizotokea Oktoba 21 na kusababisha kifo cha mfuasi mmoja wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Stephen Kwilasa, ambaye alipigwa jiwe na kuchomwa na kitu chenye ncha kali na kufariki papo hapo katika vurugu zilizotokea katika kijiji cha Kizungu wakati mgombea ubunge wa Jimbo la Maswa Magharibi kupitia Chadema, John Shibuda, alipokuwa akijinadi mbele ya wananchi wa kijiji hicho.
   
Loading...