Hujuma bandari ya Dar es Salaam | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Hujuma bandari ya Dar es Salaam

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by Lutala, Sep 30, 2010.

 1. Lutala

  Lutala JF-Expert Member

  #1
  Sep 30, 2010
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Wakongo waandamana Dar  na Mwandishi wetu
  WAFANYABIASHARA na waagizaji wa magari kutoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), wameandamana wakiilalamikia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kuwazuia kutoa magari yao bandarini bila kuwapa sababu za msingi.

  Tukio hilo lilitokea mjini Dar es Salaam jana, ambapo wafanyabiashara na waagizaji hao walilazimika kuandamana kutoka bandarini hadi kwenye ukumbi wa Karimjee kwa ajili ya kumtafuta Kamishna wa TRA, ambaye alikuwepo hapo kwa ajili ya kuhudhuria mkutano.

  Wakizungumza na waandishi wa habari, Wakongo hao walisema magari yao yamezuiliwa kwa kipindi cha muda mrefu na ilidaiwa magari hayo yana mfumo wa usukani wa upande wa kushoto badala ya upande wa kulia, kitu walichosema eti ndio sababu ya kutopewa na kusema si sababu ya msingi kwao.

  “Sababu iliyotolewa si ya msingi kutokana na nchi yetu kutojali mfumo wowote wa usukani wa gari. Sisi tunataka Mamlaka ya Mapato waruhusu tuchukue magari yetu hata kama yana matatizo yatajulikana huko nchini kwetu Kongo, wala si hapa Tanzania,” alisema mmoja wa Wakongo ambaye hakutaka jina lake litajwe.
   
 2. Brown73

  Brown73 JF-Expert Member

  #2
  Jun 6, 2011
  Joined: Aug 24, 2010
  Messages: 868
  Likes Received: 347
  Trophy Points: 80
  Kwa kweli afrika hatuta endelea hata siku mmoja. Hata kama watu watakwenda shule gani african will always be african.
  Ni vizuri sana hawa wakongo wameajitokeza na kuandamana ili wananchi wajue tatizo liliokwepo hapo bandarini. Na ingekua vizuri watu watanzania pia kufanya hivyo. Umeleta container au gari na ukababishwa hapo na TRA basi ni vizuri kuweka wazi kwenye magazeti na vyombo vya habari ili ujulikane sababu ya kizuizi. Watanzanai tutumieni sana vyombo vya habari na internett.
   
 3. K

  Koba JF-Expert Member

  #3
  Jun 7, 2011
  Joined: Jul 3, 2007
  Messages: 6,144
  Likes Received: 495
  Trophy Points: 180
  pale Airport ndio balaa zaidi,wanakuomba rushwa waziwazi kabisa...wale mabwege wanafikiri wanamkomoa mtu pale na kupata utajili lakini soon wote watapoteza kazi kwa ajiri ya uzembe wao wa rushwa na kutofanya kazi,polisi barabarani ni kama haki yao uwape pesa la sivyo utabandikwa mauwongo amabayo hujawahi kuyasikia,dawa inabidi wananchi waanze kugoma na kuwatoa nishai hawa mafisadi wanaolipwa na kodi yetu maana serikali imeshindwa kazi,hawa mafisadi ni kuwarecord na kuwachoma all over the news na sura zao wazi wakiomba rushwa na ikibidi private citizens waanze kuwashtaki la sivyo hakuna kitu kitabadilika...hakuna kitu kibaya kama rushwa ni sumu kwa kila mtu kwenye society na inarudisha sana maendeleo nyuma kwa kila mtu,kila mtu lazima aichukie rushwa na kusema au kufanya kitu na ukiombwa rushwa kataa no matter what the outcome,private citizens waanzishe fund za kuwatetea walioathiriwa na rushwa pia.
   
Loading...