Hujafa hujaumbika

Hujafa hujaumbika

mwengeso

JF-Expert Member
Joined
Nov 27, 2014
Posts
9,286
Reaction score
6,729
Naileta hapa kama nilivyoipata. Naamini ni somo zuri linalotukumbusha utu maana yake nini, hasa tunaopenda kuchangia humu kwa maneno na lugha isiyo ya kistaarabu. Hata kama umechukia, unalaumu au unakosoa, tanguliza ubinadamu kwanza katika mawazo yako.

"Baada ya kumaliza kulinda amani na kupigana vita dhidi ya waasi huko mashariki ya kati, kijana ambae alikuwa ni mwanajeshi katika kikosi cha umoja wa mataifa aliamua kuwapigia simu wazazi wake.

Mtoto: "Baba na mama, ninarudi nyumbani, ila nina ombi moja kwenu. Ninae rafiki yangu nataka nije nae huko". "Sawa njoo nae tu tutafurahi sana kumuona", wazazi wake walimjibu.

"Kuna kitu mnapaswa mjue wazazi wangu, huyu rafiki yangu aliumizwa vibaya na waasi baada ya kutekwa, amepoteza mkono wake wa kulia na mguu wa kushoto! Hana pa kwenda na ninataka nije nae tuishi wote pamoja hapo nyumbani", mtoto aliwaomba wazazi.

"Poleni sana mwanangu, labda tukusaidie kupata sehemu nyingine ambako huyo rafiki yako ataishi, lakini sio hapa nyumbani.", wazazi walimjibu.

"Hapana baba na mama mimi nataka aishi pamoja na sisi" Mtoto alisihi. "Mwanangu mlemavu kama huyo atakuwa mzigo kwetu kumuhudumia"[/I], mzazi aling'aka, na kuongezea, "tunayo maisha yetu ya kuishi, na hatuwezi kukubali kitu kingine kiingilie haya maisha yetu ya furaha, ninafikiri wewe rudi tu nyumbani na usahau kuhusu huyo rafiki yako, atakuja kupata namna ya kuishi"

Kufikia hatua hii kijana alikata simu, wazazi hawakumsikia tena. Baada ya siku chache wazazi wake walipokea simu kutoka India, ilikuwa simu kutoka polisi katika mji wa New Delhi.

Wazazi waliambiwa kuwa Mtoto wao alikufa baada ya kuanguka kutoka juu ya jengo lenye ghorofa kumi, polisi walithibitisha pasina chembe ya mashaka kuwa kijana alijiua.

Wazazi walisafiri mpaka India, huko walienda katika mochwari ya jimbo kutambua mwili wa mtoto wao. Ni kweli alikuwa ni yeye, lakini kwa mshangao wakaona kitu ambacho hawakukitarajia kabisa! Kijana wao alikuwa na mkono mmoja na mguu mmoja.!

______________________________
TAFAKARI
Wazazi wa kijana katika hadithi hii ni kama wengi wetu tulivyo humu. Tunaona ni rahisi zaidi kuwapenda wale wenye muonekano mzuri, ila hatupendi sana watu wenye kasoro mbalimbali mwilini.

Tumewatenga na kuona kama hawana umuhimu wowote, kwamba maisha yao hayana thamani sawa na yako. Hii sio sawa kabisa.

Tuonyeshe upendo kwa wale wenye ulemavu, tuwapende na juwajali, dharau si jambo jema hata kidogo.

Tuombeane kwa Mungu atupe moyo wa ujasiri wa kuwakubali watu jinsi walivyo, na atupe uelewa wa kuwatambua wale walio tofauti na sisi.
 
Siku hz mafundisho yamekua mengi sana, sijui ndio kiama kinakalibia
 
Duh nimejifunza kitu hapa,ubarikiwe mkuu
 
Huyo Kijana kwa nini hakusema ukweli, hiyo ndiyo adhabu ya mtu muongo
 
Kipimo kikubwa sana cha upendo hicho!

Upendo wa Agape wanao wachache sana na ngumu sana kuupata.
 
Huyo Kijana kwa nini hakusema ukweli, hiyo ndiyo adhabu ya mtu muongo

Alikuwa anawapima je wanaweza wakaishi na mtu wa namna hiyo? Ili apate ukweli pindi atapofika nyumbani apate upendo ule ule aliokuwa anapewa hapo awali.

Lakini akapewa jibu la kukataliwa hivyo hali yake ilikataliwa nyumbani.
 
Constructive thoughts.............................
 
Mi nakuwa tofauti na wachangiaji wote, kwann hakuwambia wazazi ukweli?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom