Huhitaji passport kuvuka mipaka ya nchi hizi..

Apr 10, 2017
54
50
Mipaka ni miongoni mwa sababu ya vita nyingi duniani hivyo uwepo wake unasaidia kuepusha migogoro kati ya nchi moja na nchi nyingine kwa kuonesha nchi ilipoanzia na inapoishia, lakini kuna baadhi ya mipaka inayotenganisha kati ya nchi na nchi nyingine ambayo inaweza kukushangaza.leo nimekuatana na hii mipaka kumi inayo shangaza duniani.

Marekani na Mexico

Hizi ni miongoni mwa nchi zenye migogoro ya kisiasa duniani lakini hii haijawazuia wananchi wa nchi hizo mbili kufurahi pamoja. picha ikionesha wananchi wa Marekani na Mexico wakicheza mchezo wa Volleyball kupitia uzio unao tenganisha nchi hizo mbili.

2:Slovakia,Austria na Hungary

Miongoni mwa mipaka inayovutia duniani ni kati ya nchi hizi tatu ambapo imeweka meza na viti kwenye mpaka huo kama ishara ya umoja na mshikamano wa nchi hizo tatu.

3:Netherland na Belgium

Mpaka unao tenganisha nchi hizi mbili ni miongoni mwa mipaka inayovutia watu wengi ambapo kwa kukadiria kuna umbali wa mita moja kutoka nchi moja kwenda nchi nyingine.

4:Sweden na Norway

Ni nchi ambazo hazina migogoro ya kivita hivyo nchi hizi mbili zinatenganishwa na barabara tu.

5:German ,Poland na Czech

Kiwanja hiki cha kucheza mchezo wa golf ndio miongoni mwa mpaka unao tenganisha nchi nyingi zaidi duniani ambapo German ,Poland na Czech zinapakana na uwanja huu unaonesha kila nchi inapoishia.

6:Spain na Portugal

Hii inaweza kukushangaza lakini mpaka unaotenganisha kati ya nchi hizi mbili Spain na Portugal ni waya.

7:Marekani na Canada

Marekani na Canada ni nchi zenye ushindani mkubwa sana hasa kiuchumi lakini kuna baadhi ya nyumba ambazo zipo katikati ya nchi hizo mbili hivyo kuzifanya nyumba hizo kujigawa.
 
Kama ni hivyo basi hata Tanznaia na Zambia hatuhitaji passport mana tunatenganishwa na barabara pale Tunduma
 
Screenshot_2017-04-21-19-03-07.png
Screenshot_2017-04-21-19-02-59.png
baarle-nassau_frontiere_cafe.jpg
 
  • Thanks
Reactions: Pep
Kwa hiyo huu ni utani au ukweli hali wa hii mikapa?
Kama siyo, kwanini usiiweke kwenye jukwaa lenye kufaa?
Maana huu ukumbi ni kupunguza mihemuko ili kupoza ubongo ,
sasa ndugu unaleta tena kitu ya kuuchosha ubongo.
 
Back
Top Bottom