Uchaguzi 2020 Huenda CCM na Dkt. Magufuli hawakujiandaa kwa upinzani huu

MFIZIGO

JF-Expert Member
Sep 30, 2014
374
232
Wanajamvi Salam,

Zikiwa zimebaki siku kumi na nne (14) tu kwenda kushuhudia historia ikiandikwa Tanzania, kwa ama wananchi kuendelea kuchagua ccm ambayo kiukweli imeshindwa kutatua matatizo yanayowakabili watanzania walio wengi au wananchi kwenda kuchagua Uhuru Haki na Maendeleo yao kwa kufanya mabadiliko ya uongozi hasa katika nafasi nyeti ya uraisi wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

Kampeni za vyama vyote shindani zinaendelea na huku wadadisi na wachambuzi wa kisiasa wakipima upepo wa kisiasa hasa kwa kuangalia Sera za vyama vyote na idadi ya watu wanaohudhuria katika mikutano ya kampeni kwa vyama tofauti. Hali imekuwa si shwari kwa chama tawala, imekuwa kana kwamba wanapumulia mashine. Kampeni zao zimekuwa zikiratibiwa kwa kiasi kikubwa nje ya chama, hapa nikimaanisha kwa kutumia vyombo vya Dora pamoja na wasanii. Huku upande wa chama kikuu Cha upinzani CHADEMA Mambo ni bul bul. Hali hii imekuja baada ya ccm kukosea hapa

1. Wamefanya siasa kwa miaka mitano peke yao, hivyo ni Kama vile wananchi wamewachoka, wananchi wanataka kusikia mawazo mapya. Wanataka kusikia kile ambacho walikuwa wanafichwa kuambiwa kwa miaka mitano huku ccm wakisema peke yao. Ndiyo maana unaona kwenye mikutano ya chama kikuu Cha upinzani wananchi wanajazana pasi na aina yoyote ya ushawishi wa wasanii. Kwenye hili ccm imewakinaisha wananchi hivyo wanataka mawazo mapya.

2. Kizazi kilichokuwa ccm kufa na kuzikana kinazidi kuisha. Wale wazee waliokuwa 60+ mwaka 2015 wakati Magufuli anaingia madarakani wamezidi kuisha, hivyo kuja damu mpya ambayo bado haioni hayo maendeleo ambayo ccm wanajivuna kuwaletea wananchi zaidi ya maumivu makali kila uchwao.

3. Ccm wanecheza karata mbaya kwa Bernard Kamiliud Membe. Najua hii ndiyo ilikuwa kete pekee ya ccm kwenye uchaguzi huu. Maandalizi makubwa waliyafanya hapa kwa kumuweka Membe kuwa Kama kibaraka kwa wapinzani, lakini CHADEMA waliliona hilo wakaruka kihunzi hicho. Rejea maneno ya Membe baada ya kikao maalumu Cha kuhojiwa na kamati ya nidhamu ya chama. " Tumeongea Mambo mazuri kwa mustakabari wa taifa letu na chama chetu." Lakini pia wanaccm waliokuwa wakimshinikiza Membe kwenda upinzani walikuwa ni wengi kuliko upinzani wenyewe. Hii maana yake walijipanga kwenye hili.

4. Magufuli amechagua timu mbovu ya kampeni ambayo haina uzoefu na masuala haya ya pilika pilika. Watu wengi ikiwemo Mimi, tulitarajia kwenye timu ya kampeni ya ccm mwaka huu wangeweka full mkoko. Pale Kuna Nape, Makamba, Mzee Mangula pamoja na viongozi wengine wabobezi ndanibya chama. Lakini uwepo wa watu Kama Polepole na Bashiru kumefanya timu ya kampeni kupwaya sana ndani ya CCM. Angalia hata upangaji wa ratiba tu unawacost.

Sioni wapi CCM watashinda iwapo uchaguzi huu utafanywa kwa kufuata misingi ya Sheria ambazo wao wenyewe ndiyo wameziweka. Iwapo tume watakuwa tayari kumtangaza hata wasiyempenda, sioni CCM watashinda vipi.

Asalam Alleykum
 
Wamejiandaa tokea 2015,kilichowakuta ni matokeo wa ubovu walio nao,wameona kujenga miundo mbinu ndio itawakomboa wananchi,imemaliza miaka mitano mwanancho wa leo hana tofauti na hajabadilika yuko vilevile kama 2015,kilichoongezeka ni madeni njaa.

Mwananchi huyo hana sababu ya kuichagua tena CCM,ndio ukaona sasa waTanzania wameamka na maendeleo yao dhidi ya chama kilichopo madarakani.

Jingine,kama unavyojua CCM wamekandamiza sana uhuru wa wananchi kwa ujumla wao,kuna mchwa wanaowala CCM na hawana dawa tena nimekusudia viongozi wa dini na zaidi waliovinja rekodi ni wale aliobebeshwa Magufuli na serikali inayoondoka madarakani ,serikali ya Zanzibar iliyoongozwa na Ali shein, unajua maraisi wa Zanzibar huchaguliwa na watanganyika wa CCM na ajabu watu hawa wakifika Zanzibar hugeuka kuwa mazezeta,unaweza ukamkuta anacheka tu.
 
Kitu pekee ninacho kipenda CCM wana mikakati ya kudumu na endelevu.

Mfano: kabla hata rais kutoka madarakani huwa kuna kijana anaandaliwa zaidi ya miaka mitano a kuwa mgombea wa urais miaka ijayo.
Na hii ndio hufanya CCM kuwa stable kila Mwaka.

Lakini hili kimbilio la wapotevu "CHADEMA" hawajawahi kuwa na long plan yeyote ili kusaidia chama chao.
Bali wao hujikuta tu anayetaka kuwa mgombea wao wa urais anajichagua tu kama mnaada vile.

Angali mh. Lowassa katoka zake CCM kaenda mnadani CHADEMA akasema nataka kuwa rais WAKAMKUBALIA..akakosa urais akaamua kusepa zake "Wakabaki midomo wazi" hahaha 😂
 
Cd zao za sgr, ndege, flyover, mabeberu, corona zimebuma haziuziki vijijini Wala mjini. Bashiru na polepole si wanaccm awaijui ccm awajawahi udhuria vyuo vya chama wakasoma siasa Hawa ni wachumia tumbo hata ccm ikifa watakuwa washapiga vya kutosha hawana uchungu na ccm.
Hivi kweli mtu unatoa wazo la kununua wanaopigiwa kura badala ya kununua wapiga kura ili uuuwe upinzani huna akili wwe!
 
Kitu pekee ninacho kipenda CCM wana mikakati ya kudumu na endelevu.

Mfano: kabla hata rais kutoka madarakani huwa kuna kijana anaandaliwa zaidi ya miaka mitano a kuwa mgombea wa urais miaka ijayo.
Na hii ndio hufanya CCM kuwa stable kila Mwaka.

Lakini hili kimbilio la wapotevu "CHADEMA" hawajawahi kuwa na long plan yeyote ili kusaidia chama chao.
Bali wao hujikuta tu anayetaka kuwa mgombea wao wa urais anajichagua tu kama mnaada vile.

Angali mh. Lowassa katoka zake CCM kaenda mnadani CHADEMA akasema nataka kuwa rais WAKAMKUBALIA..akakosa urais akaamua kusepa zake "Wakabaki midomo wazi" hahaha
Kwahiyo una maana hata jiwe aliaandaliwa kuwa Rais miaka mitano nyuma?
Kumbuka alisema yeye alikuwa anajaribu tu lakini akasukumiziwa ndani


Sent from my Infinix X680 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom