HUDUMA ZA STAR TIMES KWA WATEJA

Koryo2

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
2,056
2,515
Kwa siku za karibuni channels za ITV, EATV na STAR zilipotea kwenye Star times ikanilazimu kumtafuta fundi wao ili kuja kurekebisha kasoro iliyotokea. Yule fundi alitumia kama dakika kumi kwa kuchomoa waya na kwenda kuelekeza dish mahali inapotakiwa kuelekea. Alipomaliza akaniambia nimpe Tshs.10,000 na mimi nikamueleza kuwa natumaini kuwa hii ni huduma kwa mteja. Makosa siyo ya kwangu na kila inapotokea makosa kama haya mnatakiwa muwatembelee wateja na kuwapa huduma ya bure. Baada ya kubishana sana nikamwambia kama unaitaka hiyo hela nipe rsiti halali ya kieletroniki al maarufu kama risiti za Mhe. Magufuli. Yeye akanieleza hana na mimi nikamueleza sikupi hela yangu bila risiti za kielectroniki. Ikabidi tuachane hivyo. Sasa swali langu kwa Star times, Kwa nini huduma kwa mteja mnatoza hela?. Ninaomba sana mjirekebishe.
 
Sasa mku unataka ukifingiwa dish likileta Shida utimiwe Fundi bure??? Hata kufungiwa Dish tu wanatoza helaa... Wewe ulizurumu jasho la mtu.. Tapeli mkubwaa
 
Back
Top Bottom