O-man
JF-Expert Member
- Nov 17, 2011
- 323
- 65
Nimepata tetesi kwamba Hospitali ya Temeke kuna kijipu uchungu kinahitaji tiba ya haraka kabla hakijageuka kuwa tambazi. Ipo wadi moja (Wadi namba 4) ambayo mgonjwa wako akilazwa humo basi anza kufanya mipango ya mazishi. Nikahoji, kulikoni na kuambiwa kwamba mgonjwa akiingizwa humo hapati aina yoyote ya tiba na wala hakuna uangalizi wa daktari wala wahudumu. Mwenye taarifa zaidi hebu tujuze.