Huduma za Maktaba Nchini

Tangawizi

JF-Expert Member
Jun 25, 2009
6,465
6,339
Elimu ili iweze kuwa na tija na endelevu, lazima watu wapende kujisomea majarida na vitabu mbalimbali muda wote wa maisha yao.

Huduma zetu za Maktaba sio za kuridhisha. Maktaba zetu nyingi hazina vitabu wala vitendea kazi vingine vyenye kuzifanya kuwa chachu ya kuleta maendeleo yatokanayo na elimu.

Tumeteleza sehemu. ...tujipe wakati na kurekebisha hali hii ili wanafunzi na wale wanaopenda kujiendeleza kielimu waweze kufanya hivyo sehemu yoyote walipo Tanzania.

Naamini kwa sasa eneo hili linaangukia wizara ya elimu. Ingekuwa faraja kama huduma za Maktaba nchini zikapewa uzito unaostahili. Watu wakielimika watasaidia kusukuma mbele gurudumu la maendeleo ya nchi yetu.

Nawakilisha
 
Kwa kifupi hatuna maktaba za uma za kutosha kukidhi mahitaji ya walaji.
Hata hizi zilizopo vitabu vyao ni zilipendwa. Wadau wa maendeleo inabidi walitizame hili kwa jicho la tatu.
 
hii siri ya kusoma vitabu sijajua hawaijui au wanaijua ila hawataki tu watu wajue faida za kusoma vitabu,

inasikitisha sana serikali kutokuhimiza usomaji wa vitabu na uwepo wa maktaba bora,
wanahimiza tu watoto wasome vitabu ili wajibu mitihani....

tujifunze kusoma vitabu waTZ.
 
Kusoma vitabu kutasaidia sana watu kuwa wabunifu na kupata njia mbadala ya kupambana na changamoto zilizopo.

Mikoa mingi na wilaya zake Maktaba hakuna za kutosha.
 
hii siri ya kusoma vitabu sijajua hawaijui au wanaijua ila hawataki tu watu wajue faida za kusoma vitabu,

inasikitisha sana serikali kutokuhimiza usomaji wa vitabu na uwepo wa maktaba bora,
wanahimiza tu watoto wasome vitabu ili wajibu mitihani....

tujifunze kusoma vitabu waTZ.
Itabidi ipigiwe debe kama mambo mengine. Wizara ya Elimu ibebe hili suala kama ajenda muhimu kwa kuiboresha nchi yetu
 
Good Thinking, Comrades.

Bado nafanya Tafiti. Ni Taifa gani limewahi kupiga hatua za kimaendeleo, kiuchumi, kisiasa na kiutamaduni bila watu wake kupenda kujifunza, kusaili na kudadisi ila jitihada zangu zinagonga mwamba. Sipati jibu kwa urahisi na labda, Jibu ni HAKUNA.

Kwanini sisi tunadhani hili linawezekana?, au pengine litaanzia kwetu?. Kwanini tunapenda kujiondoa ufahamu kwa kiasi hiki?. Siyo baba, mama, jamii na Taifa kwa ujumla.

Rafiki yangu (asiyepungukiwa na kumbukumbu) aliwahi kuniambia "Hakuna kazi rahisi kama kuwaongoza watu wasiopenda kusoma, mbaya zaidi hakuna kitu kibaya kama kuongozwa na watu wasiopenda watu wasome".

Ili ubongo uwe na manufaa kwa binadamu ni sharti uendelezwe, unolewe, ufunzwe, ulindwe, ufanyiwe usafi na kadhalika. Na huku kote husaidiwa kwa kusoma vitabu, kutizama na kusikiliza vipindi vya msingi, kusafiri macho na masikio vikiwa wazi na kadhalika. Huu ndiyo uwezo wa pekee alioutupa Mungu.

Ubongo wa binadamu usipofanyiwa hivi, kisilika hufanana na ubongo wa mbuzi ambao kimantiki husibiri kuliwa na binadamu. Ni lazima tuwe RESTLESS, tusaili, tutafiti, tuulize. Ndivyo walivyofanya kina Gallileo, Copernicus, Socrates, Nyerere, Lumumba na orodha inaendelea.

Ni lini uliwahi kumuona Public Figure (Rais, Waziri, Mbunge, Askofu, Padre) Maktaba?, japo kuhimiza tabia ya Usomaji vitabu?. Sina kumbukumbu vizuri, zaidi tu Namuona Mh Zitto, Makamba, Padre Amigu wakihimiza mitandaoni na kuweka List ya vitabu walivyosoma. That's good somehow, how about others?.

Lakini, Je ni wangapi wenye access ya kuingia mitandaoni na kuona idadi ya vitabu walivyovisoma?. Hatuoni kwa wenzetu utofauti ulivyo mkubwa?. Kila mwisho wa mwaka wanaweka List ya vitabu walivyosoma (kwa kusailiwa), huku ni siasa, siasa, siasa!!

Nashauri, Serikali, Wizara husika iliangalie hili kwa jicho la kipekee. Taifa lisilohimiza watu wake wapende kusoma vitabu linajichimbia kaburi na kuzalisha Taifa la watu wa hovyo kwa miaka na siku za usoni.

Baba akisoma vitabu, mama akisoma vitabu na mtoto pia atasoma vitabu.

Asalaam.
 
wengi ukiwa unasoma vitabu wanakuona kama mtu uliye na majivuno,wanapenda kukulinganisha pia maisha yako una mafaniko gani nk,ila kiukweli mimi nimeanza kusoma vitabu seriously nina mwaka na kidogo,nimeshuhudia tofauti kubwa sana,sana sio kidogo,ni kweli naamini kila tatizo unaloliona duniani,suluhisho lake limeaandikwa kwenye vitabu
Nakumbuka usemi wa FaizaFoxy ushauri wake humu jf aliwahi kusema ''soma chochote unachokiona mbele yako,aliongea kitu kikubwa sana
BOOKS CAN MAKE SOME ONE RICH IN MIND EVENTHOUGH POOR I POCKET ingawa pia possibility ya kuwa rich in pocket ni kubwa sana kwa 200%
 
hii siri ya kusoma vitabu sijajua hawaijui au wanaijua ila hawataki tu watu wajue faida za kusoma vitabu,

inasikitisha sana serikali kutokuhimiza usomaji wa vitabu na uwepo wa maktaba bora,
wanahimiza tu watoto wasome vitabu ili wajibu mitihani....

tujifunze kusoma vitabu waTZ.
Tunaishi Kusini mwa jangwa la Sahara Mr Miller .

Ni huku ndiko ambapo mwananchi akierevuka basi mwanasiasa anakuwa mashakani. Ni huku ndiko ambapo bajeti ya Wizara Mama kama Elimu inapangwa na kiongozi ambaye mwanae hasomi katika shule anakopangia bajeti ielekezwe. Unategemea akutengee bajeti nzuri?. Sitaki unijibu.

Ni huku ndiko ambapo Mazingira ya ufundishaji hayaboreshwi. Sasa unajiuliza, Je mtoto ataipendaje shule wakati hakuna dawati na zanambiu ya Elimu?. Akifika shule anakaa chini, maktaba hakuna, Serious?... Thomas Edison (Mgunduzi wa balbu) anasema hivi "Bila mazingira bora ya ufundishaji, hakuna mwanafunzi atakayeipenda Elimu". Elimu bora kichwani huchangizwa na mazingira bora.

Ni huku ndiko ambapo Wanasiasa wengi hawaipendi siasa. Wanapenda madaraka. Sasa utegemee nini?.

Serikali (Mwanasiasa) kuhimiza wananchi kusoma vitabu ni sawa na hadithi za Alfu lela Ulela. Si utaerevuka na kuanza kumpinga kimantiki?. Ni suala la kujengwa kwa misingi bora ya kifamilia, kijamii na Kitaifa. Sidhani kama kumsubiri mwanasiasa kutatutoa. Ni shughuli pana kidogo aise..

Karibu tuelekezane..
 
We are masters of our destine...kwanini kila kitu tunaamini ni sababu ya viongozi? Sisi sio sehemu ya tatizo hilo?

Maktaba ni kitu muhimu mno...kujisomea ni muhimu zaidi. Tunakesha bar na kumbi za starehe kuliko sehemu ambazo zinaweza kubadili kabisa sisi tulivyo na mustakabari wetu kama Taifa.

Watoto toka wadogo wahimizwe kutumia maktaba.
 
Kumradhi..

Nimejaribu kumjibu Mr Miller kwa mtazamo wake wa kuwatizama wanasiasa wayatatue masuala ambayo yapo ndani ya uwezo wetu. Lakini pia sipo mbali, japo sikutaka kumuunga mkono wala kutomuunga.

Kiongozi ni mimi. Kiongozi ni wewe, ni yule na kadhalika. Nimemzungumzia mwanasiasa, mtumishi wa Serikali. Ni tatizo gani ambalo mwanasiasa hahusiki hapa nchini?. Kuwepo kwa tatizo, kuenea, kukua n.k?. Wanasiasa wanachangiza, believe me or not..

Kuanzia Miundombinu, maji, elimu na kadhalika?. Wanasiasa hawahusiki?.

Nakuunga mkono. Maktaba ni pahala muhimu. Ni sharti kujengwe, kuendelezwe na kuimarishwa ili kukapate kuwa na manufaa kwetu. Nje ya hapo kunakuwa ni gofu tu.
 
Shule zetu zote, za umma na za binafsi zilazimishwe kuwa na maktaba yenye vitabu vya kujisomea kwa ajiri ya watoto. Watoto waanze mapema kufundishwa kujisomea vitabu.

Zamani kila mkoa ulikuwa na maktaba..sijui kama bado hilo lipo...na maktaba zenyewe zina vitendea kazi kiasi gani.
Nimeipenda sana hii mada...ni muhimu ndio maana haina wachangiaji wa kutosha
 
Tunaishi Kusini mwa jangwa la Sahara Mr Miller .

Ni huku ndiko ambapo mwananchi akierevuka basi mwanasiasa anakuwa mashakani. Ni huku ndiko ambapo bajeti ya Wizara Mama kama Elimu inapangwa na kiongozi ambaye mwanae hasomi katika shule anakopangia bajeti ielekezwe. Unategemea akutengee bajeti nzuri?. Sitaki unijibu.

Ni huku ndiko ambapo Mazingira ya ufundishaji hayaboreshwi. Sasa unajiuliza, Je mtoto ataipendaje shule wakati hakuna dawati na zanambiu ya Elimu?. Akifika shule anakaa chini, maktaba hakuna, Serious?... Thomas Edison (Mgunduzi wa balbu) anasema hivi "Bila mazingira bora ya ufundishaji, hakuna mwanafunzi atakayeipenda Elimu". Elimu bora kichwani huchangizwa na mazingira bora.

Ni huku ndiko ambapo Wanasiasa wengi hawaipendi siasa. Wanapenda madaraka. Sasa utegemee nini?.

Serikali (Mwanasiasa) kuhimiza wananchi kusoma vitabu ni sawa na hadithi za Alfu lela Ulela. Si utaerevuka na kuanza kumpinga kimantiki?. Ni suala la kujengwa kwa misingi bora ya kifamilia, kijamii na Kitaifa. Sidhani kama kumsubiri mwanasiasa kutatutoa. Ni shughuli pana kidogo aise..

Karibu tuelekezane..

What could we do differently to change this status quo?
 
Back
Top Bottom