Huduma za BRELA ni changamoto

Huduma za BRELA ni changamoto

queen of the jungle

JF-Expert Member
Joined
Mar 17, 2017
Posts
228
Reaction score
430
Ukienda ofisini kwao unaambiwa unatakiwa uombe online, unaomba online wanakuambia majibu ndani ya siku tatu. Hizo siku tatu zinaenda mpaka kumi unawafata tena wanakuambia tutakujibu ndani ya masaa, unasubiria jibu mpaka unakata tamaa.

Kuna haja gani ya kuwambia watu waombe online kama hamuwezi kuwajibu? Pili mnataka watu tuende wapi kupata majibu ya maombi yetu kama hamuwezi kutujibu kwa wakati?

Toka Kibaha nafatilia jambo moja tuu na nikija hapo tutakujibu online lakini hakuna majibu hii ni chamgamoto sasa mtu unaamua kufanya bila usajili mtatulaumu pia.
Kama ni hivyo hakuna muongozo wa mtu ukishindwa kujibiwa kwa wakati uende wapi pa kupeleka malalamiko yako. Kama mko busy watu wamejaa wanatafuta kazi ongezeni watu au ondoeni hao ambao hawataki kujibu kwa wakati.

Mbali zaidi mtu umehangaika kuilipia matokeo yake unazurura tuu karibu mwezi mzima na hapo Serikali inataka uchumi ukue ngoja tuendele kufanya bila usajili mi binafsi nimechoka na hili jambo la kuhangaika na BRELA mwezi mzima.
 
Ukienda ofisini kwao unaambiwa unatakiwa uombe online, unaomba online wanakuambia majibu ndani ya siku tatu. Hizo siku tatu zinaenda mpaka kumi unawafata tena wanakuambia tutakujibu ndani ya masaa, unasubiria jibu mpaka unakata tamaa.

Kuna haja gani ya kuwambia watu waombe online kama hamuwezi kuwajibu? Pili mnataka watu tuende wapi kupata majibu ya maombi yetu kama hamuwezi kutujibu kwa wakati?..............

Mkuu wamezoea rushwa sio rahisi kabadilika hao
 
Back
Top Bottom