Huduma za afya nchini: Mkapa vs Kikwete.

Hacha uongo kumtetea mhuza sura CT scaner zilikuwepo toka 2004 pale BUGANDO, KCMC,na MHUHIMBIL mie nimetibiwa pale BUgando kwa 2004 zilikuwepo

Weka ushahidi wa ripoti yako ya CT scanner (i scan) uiweke hapa. Wewe umefanyiwa cardiograph unasema CT scan.
 
Porojo zinazosaidia ni njema sana kuliko porojo zisizo saidia.

Utawala wa kabla ya Kikwete ulikuwa wapi? usiwe wa mwanzo? mpaka anakuja Kikwete ku rescue bado ni mbaya? au UNFPA ilikuwa haipo? fikiri.

zomba, unajua kitu kinaitwa UNDAF? Au unafikiri wengine wanafanya mambo kwa mtindo wa zima moto kama serikali ya CCM inayoongozwa na matukio?
 
zomba, unajua kitu kinaitwa UNDAF? Au unafikiri wengine wanafanya mambo kwa mtindo wa zima moto kama serikali ya CCM inayoongozwa na matukio?

Wewe utaishia kuuliza maswali tu kwa sababu huna explanation ambayo ni plausible.
 
Lipi ambalo limeisha au limepungua? Tatizo la njaa na umeme lipo pale pale, na pengine limeongezeka. Juzi tumetangaziwa TANESCO imefilisika. Ujambazi umebadilika tu, kutoka ule wa kutumia silaha mpaka ule wa kwenye mtandao! TUWE WAKWELI.

Tatizo la njaa halijauwa mtu toka Kikwete ashike madaraka, leo hii tuna chakula cha akiba.

Tatizo la umeme, sijui kama unaelewa miradi inayoendelea kuanzia wakati wa Kikwete tu ili kutatua hili tatizo, au unataka vielelezo?

Ujambazi alioukuta Kikwete unatisha, watu walikuwa wanafunga mitaa na barabara. Ukitoka Dar kwenda Singida tu, ukitoka Dodoma tu ilikuwa lazima uende na escort ya polisi wenye silaha, hakuna malori yalikuwa yanatembea usiku na hiyo ilikuwa ni kila siku kwa muda wote wa utawala wa Mkapa. Nenda leo ukaone.

Ma escorst ya polisi wenye silaha yamepunguwa kutoka kila pembe za Tanzania, au hilo hulijui? leo unasikia Mtoni kumefungwa mtaa watu wanapora? umesikia Kariakoo kumefungwa mtaa watu wanapora? hayo yalikuwa ni mambo ya kawaida wakati wa Mkapa.

Leo unasikia EPA, unasikia Radar, unasikia Kiwira, unasikia BOT. Unajuwa uhalifu huo ulifanyika wakati upi? Kikwete anayaibua na anayatibu hayo maradhi (waulize madaktari kama haujumuwa na kuugunduwa ugonjwa utatibu nini?).

Life span ya Mtanzania ni miaka 57.4 kwa miaka 7 tu ya Kikwete, niambie kabla ya Kikwete ilikuwepo hiyo?
 
hii ya MRI na CT scan ni sawa na mtu kulinganisha uwepo wa androids kipindi cha mkapa

na pia kutokana na mfumo wa afya.... na hasa in our developing countries kipimo kikubwa cha afya ni basics health care package na sio 4th generation interventions kama mleta mada anavyotumia vigezo

tunatakiwa tuangalia minimum health care packages at all levels, service delivery success nk

nina wasiwasi na watu wanotumia na JK kumtetea... nivi hana hata epidemiologists wawili wamuandalie a good document kuliko hawa wawili anaowatumia humu??
 
zomba, unajua kitu kinaitwa UNDAF? Au unafikiri wengine wanafanya mambo kwa mtindo wa zima moto kama serikali ya CCM inayoongozwa na matukio?

Mimi sikijuwi hicho kitu wala sina haja ya kukijuwa, nikifikia kutaka kukijuwa ntakijuwa bila ya kukuuliza wewe.

Huko juu Nilisema Maisha ya Mtanzania yamepanda kwa miaka 5 kwa miaka saba tu ya Kikwete, nimeambiwa hiyo data ilikuwa ya miaka 5 ya mwanzo wa uongozi wa Kikwete na kwa sasa ni miaka 57.4 ikimaanisha kuwa imepanda kwa miaka 9 kwa miaka 7 ya uongozi wa Kikwete (hii ni rikodi ya dunia) Unalijuwa hilo? Ushahidi huu hapa:


Google Public Data Explorer 57.4 years - 2010
Source: World Bank

 

Hivi katika mgomo unaoendelea hivi sasa umesikia kuna daktari anayezungumzia minimum healthcare package? Sote tumesikia CT scanner na MRI zikitajwa kuwa ni miongoni mwa vitu muhimu vinavyokosekana, ndio tukajiuliza, kwani hizo zimeanza kuja lini Tanzania? Jibu liko kwenye thread...
 
Kama vifaa hivyo vimenunuliwa wakati huo ni kwa sababu alikuta kuna reserve ya fedha za kutosha. Leo inabidi wakope kwa mabenki kwa shughuli za serikali!
 
Nimesikia kuanzia Sasa Ruhusa ya Kutoka Bungeni au Kutohudhuria vikao atakuwa anatoa Spika pekee... hali naona imekuwa Tete...

Spika you can lie People but you cant lie your self and You can fool people sometimes but not all the times... Tafakari zingatia Nchi ni yetu na sio Yako au Yenu
 

Duduwasha, hii taarifa mpya sana!
 
kwa mara ya kwanza mtu apasuliwa kichwa badala ya mguu?????

Kwa mara ya kwanza mawaziri wa afya mfululizo wakosa mashiko na kuachia ngazi

kwa mara ya kwanza madakitari waendesha migomo mfululizo kwa kuzorotata secta ya afya

Kwa mara ya kwanza viongozi kwa asilimia kubwa kutibiwa pia kucheki afya zao ng'ambo ya inchi

kwa mara ya kwanza dawa feki/bandia zimeenea inchi nzima

Kwa mara ya kwanza ............. wagonjwa hawana wakuwatetea.........mara ya kwanza....serikali yaishi maisha ya propaganada secta ya afya ........mara ya kwanza............

1. huduma za afya kwa ujulma wake zimezolota kupita wakati wowote ule wa maisha yangu.
2. Rushwa katika wizara ya afya imepita aibu na mipaka, kama mnasilikiza BBC swahili asubuhi utaona idara ya afya ilivyooza na kupoteza njia.
3. Madawa hakuna wala vitendea kazi, hili halihitaji data, ushahidi, wala maelezo yoyote vinginevyo unatibiwa hospitali binafsi. (BBC swahili inasaidia sana kutoa utata huu maana wanawahoji raia moja kwa moja na kuepuka porojo na uongo wa serikali)

Tatizo ninaloliona Serkali na wapiga debe wake ni wahuni wa kupika data, kuwakilisha data fake na kuuhadaa uma wa watanzania. Haiwezekani reseach data zivary inversely proportional ukizipeleka kwenye uhalisia.

Nirahisa sana kujidanganya mhusika, kwa dunia ya leo si lahisi kuwahadaa watanganyika na walimwengu kwa ujumla wake.
 
Wote (Fisadi Mkapa na DHAIFU) ni sifuri tu hakuna hata aliyekuwa na afadhali.
 
Nyerere alishajua Safari za Nje Ni Tamu so alifanya Jitihada Kikwete asiingie Madarakani akimjua Fika Jamaa anavyopenda Kusafiri kwani alijua Kikwete akianza kusafiri basi atazidi na kuzidi... ni hili Yunaliona...


Nasikitikia Vijana wenzangu Wabunge wa CCM kwa kumsifia Raisi kwa kuteua Wakuu wa Wilaya...!!!! wakai hiyo ni kazi yake!
Itafikia Siku watamsifia Raisi kwa Kunywa Maji!...By Sugu MB..


Huduma ya Afya Haijafikia kama tunavyohitaji Raisi bado anakazi Nzito kulingana na Muda wake Madarakani... Na Hii tabia ya kusikiliza Vilaza badala ya Wananchi itamcost katika Historia...
 
hakuna lolote! mwaka 2005 mwishoni mwa kipindi cha Mkapa kulikuwa na mgomo mkubwa sana wa Madaktari hapa TAnzania, hii pia ilileta changamoto kubwa sana kwa serikali ya CCM kuwa makini zaidi na sekta ya afya, wakapanisha mishahara na kuanzanza kuboresha sehemu kadhaa za skta hio. Tatizo ni kwamba uboreshaji wao ni duni mnooo! kama umeamua kununua CT scan, nunua za kutosha nchi nzima! mbona mashangingi huwa yananunuliwa ya kutosheleza viongozi wote kuanzia ngazi za wilayani? Tusifanye watanzania kuwa ni vipofu, tunatupiwa kamfupa kamoja basi turidhike, ati kwa kuwa aliyepita hakututupia hata kamfupa kamoja! kwa kifupi, MKAPA na KIKWETE wanaweza kutofautiana katika jinsi walivyoijenga secta ya afya, LAKINI MKAPA WALA KIKWETE KIUJUMLA HAWAJAIJENGA SECTA HIYO KABISAAA SERIOUSLY SPEAKING! ni kama wanapaka rangi nyumba ili ipendeze kwa nje, waweze kuipiga picha na kuitoa magazetini na kuwaambia watanzania jinsi gani wao ni wazuri, lakini ndani hakuna nyumba!
 
AAAAAAAAA ZEMARKOPOLO!!!!!!!! karibu katika uwanja wa JF na nia zako zijulikanazo DR IMANI KONDO MPONDA!
 

Urgument za kitoto peleka kwenye NEC ya magamba, aliyekwambia lifespan inaongezeka kutokana na vibajaji nani?
Umefikiria suala la usahihi wa takwimu (reliability) hizo, vifo vingapi vinavyotokea vijijini haviripotiwi?? Mara ngapi takwimu zimechakachuliwa kufurahisha wakubwa??

Wakati unafanya inference ya lifespan inatokana na uongozi wa JK impact ya ongezeko la wasomi ambao wanajua umuhimu wa balanced diet na mazoezi uliiexclude vipi??
 
machine zilizoibiwa na kina Mahita kupelekwa Morogoro kwao watu wamekaa kimya? vifaa vimenunuliwa na serikali ya JK pia ila wasiseme hakukuwa na vifaa alipongia Mkapa au JK, labda vimeharibika au vimeibiwa au vinahitajika vifaa zaidi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…