Huduma ya Taaj Express Money Transfer

BusinessTZ

Member
Apr 24, 2018
13
10
Husika na kichwa cha Habari
Naomba kuambiwa huduma ya Taaj Express Money Transfer inatolewa na Bank gani au taasisi gani ya fedha Tanzania?
Iko hivi kuna Rafiki yangu kanitumia kiasi cha pesa kupitia Huduma ya Taaj Money Express Transfer, nimejaribu kwenda ofisi za Western Union, wamesema hawaifaham hiyo Huduma, nimeenda Benki ya DTB kitengo cha Western Union, Money Gram na Express Money, pia wamesema hawaifaham hiyo Huduma ya Taaj Express Money Transfer.
Sasa najua humu JF kuna wabobezi na wataalam wa mambo mengi naomba msaada na Taarifa ya taasisi inayohusika na hiyo Huduma ya Taaj au Tawakal Express Money Transfer ili niweze kuchukua dollar Zangu wadau
 
Livingstone ya Kariakoo Mkuu nimewahi kumsindikiza ndg yangu alitumiwa pesa kwa njia hiyo ni karibu na NMB
 
Sina hakika ila maeneo yale ukifika ulizia huduma ya hawala kwa wasomali
 
Mara nyingi hao Wasomali wanapewa namba ya receiver na Sender, then pesa ikiingia wanakutumia kwa Mpesa au tigo pesa....nimeshatumiwa pesa kupitia hao Wasomali 2 times.
 
Mara nyingi hao Wasomali wanapewa namba ya receiver na Sender, then pesa ikiingia wanakutumia kwa Mpesa au tigo pesa....nimeshatumiwa pesa kupitia hao Wasomali 2 times.
Sijakuelewa Ndugu, watakutumia vip kwa m-pesa au tigo Pesa na wakati Pesa ni Us Dollar?
 
Iko hivi, kama ni wa Somali mwambie sender wako apewe details za ofis yao ya huku ipo mitaa gani maana wa somalı wanao toa hiyo huduma wako wengi wengine ni from their home
 
Sijakuelewa Ndugu, watakutumia vip kwa m-pesa au tigo Pesa na wakati Pesa ni Us Dollar?
Huwezi kutumiwa sarafu ya kigeni then ukaenda kuichukua kama ilivyo.....kwa mishe zangu nimeshapokea pesa kwa Western Union, Money Gram, Bank Transfer, World remit, Payoneer na nyingine inatumiwa na International Bank moja nimesahau, pesa itatumwa iwe $ au yoyote, but ukienda Ku withdraw unapewa pesa za madafu....

Mfano World remit ni International, pesa ikitumwa, Sender ana uchaguzi wa kutuma hiyo pesa ama iingie kwa Bank, wakala wao au straight mpesa yako au tigo pesa, unampa namba Sender then anatuma pesa, inaingia straight kwa mobile wallet yako, na hao Wasomali wa Kariakoo ni the same.

Ni lazima kuwe na Mawasiliano kati ya Sender na Receiver kabla pesa kutumwa.
 
Mkuu habari. Vipi ulifanikiwa kufika maana na mimi Nina shida nao pia leo
 
Back
Top Bottom