Huduma ya bure ya ushauri kwa wakulima na wafugaji kwa njia ya simu

achengula

JF-Expert Member
Jul 30, 2009
380
225
logosua.gif


Pata ushauri wa bure kuhusiana na kilimo kwa njia ya simu kupitia mtandao wa ushauri kwa wakulima (MUWA). MUWA inaratibiwa na mradi wa EPINAV - 'MOBILE FOR IMPROVING AGRICULTURE EXTENSION SERVICE', uliopo Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo.

MUWA inawawezesha wakulima kupata ushauri katika mambo mbalimbali yanayohusu kilimo kama vile ukulima, uvunaji, ufugaji wa wanyama, utuzaji wa misitu, maendeleo ya jamii, masoko na msaada wa kiuchumi katika kuendeleza kilimo.

Kama unapenda kupewa ushauri kupitia simu yako ya mkononi unaweza kutuma swali lako kupitia namba 0688099408 na mabwana na mabibi shamba watakujibu mara moja!

NB: Huduma hii ni bure ila mkulima utalipia gharama ya ujumbe mfupi wa simu kwa kampuni husika ya simu. Mradi utalipia gharama ya ujumbe mfupi wa simu wenye majibu ya swali la mkulima.

TOVUTI: MUWA
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom