Huawei Yadai Ascend P2 Ndio Simu Yenye Kasi Duniani?

ManiTek TV

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2011
Posts
410
Reaction score
159
07/03/2013

​
Huawei ni kampuni ya tatu kuuza simu nyingi aina ya smartphone katika robo ya mwisho ya mwaka 2012, mzungumzaji wa Huawei Technologies, Tatiana Debra alidai katika mahojiano na WSJ kwenye maonyesho ya MWC huko Barcelona, Tatiana amedai kwamba kinachoifanya simu hiyo iwe na kasi zaidi ni kuwa prosesa aina ya K3V2 inayotengenezwa na Huawei wenyewe ina nguvu na kasi kuliko prosesa nyingine kama vile Snapdragon.

Dai la Huawei ni dai zito, hivyo sio rahisi kulikanusha kwa sababu limetoka kwa mzungumzaji rasmi wa kampuni, na kulikibali pia sio rahisi hasa ukizingatia kwamba tayari kuna simu zenye prosesa yenye kasi ya 1.7 GHz katika soko, simu kama vile Sony Xperia Z na simu inayotarajiwa kutoka wakati wowote kuanzia sasa HTC One.

Hivyo muamuzi rahisi wa hoja hii ni Quadrant Professional Edition, ambapo inafanya benchmarking na kutoa matokeo ya kasi, hivyo tutaifananisha Huawei Ascend P2 na Samsung Galaxy SIII na Google/LG Nexus 4 ambazo ni simu za mwaka jana na pia Sony Xperia Z na HTC One ambazo ni za mwaka huu. Matokeo ya Benchmark ya Huawei yenyewe tumeyapata kupitia GSM Arena. Matokeo ya Quadrant Professional Edition Benchmarking, simu zimepangiliwa kwa ushindi, ambapo yenye score ndogo ndio ina nguvu zaidi:

​

Hivyo HTC One ndio mfalme wa kasi katika simu tano hizi, huku ikifuatiwa na Sony Xperia Z, hili halikutushangaza, kwa sababu HTC One ina prosesa ya 1.7 GHz na Sony Xperia Z ina prosesa ya 1.5 GHz, hivyo dai lililotolewa na Huawei kuhusu kasi ya simu yao sio la kweli, lakini tulichoweza kuona ni kwamba Huawei Ascend P2 imepitwa na simu mpya tu, kwa hiyo wakati Huawei wanafanya uchunguzi wa simu ipi ina kasi kabla ya kutoa dai hili bila ya shaka walikuwa bado hawajaziona na kuzipima kasi simu mpya katika jedwali letu yaani HTC One na Sony Xperia Z.

​
Hata hivyo simu hii ni mfalme wa kasi ya LTE ambapo simu hiyo iko kwenye LTE Cat 4 na kasi ya juu kabisa ya kundi hili ni 150 Mpbs, hakuna simu unayoizidi Hauwei Ascend P2 katika kasi ya intaneti. Ingawa upo uwezekano wa kutumia teknolojia ya category 5 au 6 katika simu, bado hakuna simu iliyotoka na cat hizo.

Kiujumla Huawei ni kampuni changa katika soko la simu lakini ni kampuni ambayo ina teknolojia ya hali ya juu na pia ina nafasi ya kufanya vizuri katika mauzo baada ya kuwa inakubalika nchini China, nchi yenye watu blioni 1.2, Huawei ilizundua simu yake ya kwanza ktika familia ya Ascend mwaka jana kwenye maonyesho ya CES huko Las Vegas, simu hiyo iliwavutia wadau wengi katika masuala ya gajeti na teknolojia kutokana na kuwa na wembamba wa milimeta 6.7 wakati huo na mpaka leo ikiwa ndio simu nyembamba zaidi duniani.
​

Chanzo: www.gajetek.com
 
Kasi sawa ila upevupicha vipi?..
 
mkuu simu yenye speed duniani inaitwa lenovo k900 ndio imevunja rekodi ya benchmark zote, imeidouble speed galaxy note II. Japokua processor yake ni dual core lakini lenovo kila benchmark wakiitest inavunja rekodi zote. Simu hii ipo powered na processor ya intel atom 2ghz dualcore.

Mfano kwenye benchmark za antutu(higher is better) lenovo hii imescore between 25,000 mpaka 27,000 kwahio highest score ni 27,000 wakati htc one anarange kwenye 22,000 na galaxy s3 kwenye 15,000, xperiza z ipo around 20,000 so kwenye benchmark za antutu king ni lenovo k900.
 
Tatizo kubwa la brand za Kichina (Lenovo na Huawei) mpaka sasa wameshindwa kuji-position kama Global brand. Ingawa hii inachangiwa na ukweli kwamba soko la China ni kubwa mno, lakini nadhani wanahitaji mikakati zaidi kuweza kukua na kutanuka kama true MNCs
 
07/03/2013

​
Huawei ni kampuni ya tatu kuuza simu nyingi aina ya smartphone katika robo ya mwisho ya mwaka 2012, mzungumzaji wa Huawei Technologies, Tatiana Debra alidai katika mahojiano na WSJ kwenye maonyesho ya MWC huko Barcelona, Tatiana amedai kwamba kinachoifanya simu hiyo iwe na kasi zaidi ni kuwa prosesa aina ya K3V2 inayotengenezwa na Huawei wenyewe ina nguvu na kasi kuliko prosesa nyingine kama vile Snapdragon.

Dai la Huawei ni dai zito, hivyo sio rahisi kulikanusha kwa sababu limetoka kwa mzungumzaji rasmi wa kampuni, na kulikibali pia sio rahisi hasa ukizingatia kwamba tayari kuna simu zenye prosesa yenye kasi ya 1.7 GHz katika soko, simu kama vile Sony Xperia Z na simu inayotarajiwa kutoka wakati wowote kuanzia sasa HTC One.

Hivyo muamuzi rahisi wa hoja hii ni Quadrant Professional Edition, ambapo inafanya benchmarking na kutoa matokeo ya kasi, hivyo tutaifananisha Huawei Ascend P2 na Samsung Galaxy SIII na Google/LG Nexus 4 ambazo ni simu za mwaka jana na pia Sony Xperia Z na HTC One ambazo ni za mwaka huu. Matokeo ya Benchmark ya Huawei yenyewe tumeyapata kupitia GSM Arena. Matokeo ya Quadrant Professional Edition Benchmarking, simu zimepangiliwa kwa ushindi, ambapo yenye score ndogo ndio ina nguvu zaidi:

​

Hivyo HTC One ndio mfalme wa kasi katika simu tano hizi, huku ikifuatiwa na Sony Xperia Z, hili halikutushangaza, kwa sababu HTC One ina prosesa ya 1.7 GHz na Sony Xperia Z ina prosesa ya 1.5 GHz, hivyo dai lililotolewa na Huawei kuhusu kasi ya simu yao sio la kweli, lakini tulichoweza kuona ni kwamba Huawei Ascend P2 imepitwa na simu mpya tu, kwa hiyo wakati Huawei wanafanya uchunguzi wa simu ipi ina kasi kabla ya kutoa dai hili bila ya shaka walikuwa bado hawajaziona na kuzipima kasi simu mpya katika jedwali letu yaani HTC One na Sony Xperia Z.

​
Hata hivyo simu hii ni mfalme wa kasi ya LTE ambapo simu hiyo iko kwenye LTE Cat 4 na kasi ya juu kabisa ya kundi hili ni 150 Mpbs, hakuna simu unayoizidi Hauwei Ascend P2 katika kasi ya intaneti. Ingawa upo uwezekano wa kutumia teknolojia ya category 5 au 6 katika simu, bado hakuna simu iliyotoka na cat hizo.

Kiujumla Huawei ni kampuni changa katika soko la simu lakini ni kampuni ambayo ina teknolojia ya hali ya juu na pia ina nafasi ya kufanya vizuri katika mauzo baada ya kuwa inakubalika nchini China, nchi yenye watu blioni 1.2, Huawei ilizundua simu yake ya kwanza ktika familia ya Ascend mwaka jana kwenye maonyesho ya CES huko Las Vegas, simu hiyo iliwavutia wadau wengi katika masuala ya gajeti na teknolojia kutokana na kuwa na wembamba wa milimeta 6.7 wakati huo na mpaka leo ikiwa ndio simu nyembamba zaidi duniani.
​

Chanzo: www.gajetek.com
Huawei Ascend P2 ni mbaya usipime,kuna mtu/jamaa yangu anayo,its an excellent phone hasa kwenye internet speed yake,ni balaa jamani kama alivyozungumzia Millah .
 
Tatizo kubwa la brand za Kichina (Lenovo na Huawei) mpaka sasa wameshindwa kuji-position kama Global brand. Ingawa hii inachangiwa na ukweli kwamba soko la China ni kubwa mno, lakini nadhani wanahitaji mikakati zaidi kuweza kukua na kutanuka kama true MNCs

dah mkuu unafananisha huawei na lenovo?

-lenovo ni wa pili kwa mauzo ya laptop duniani
-ndio most trusted company ulaya na marekani baada ya dell kuanguka na hp kuanza kutoa vitu ovyo.

Maneno kama idea, thinkpad au yoga ni maneno ya kawaida kuyaona kwenye web za tech lenovo mziki mwengine kaka
 
Usishtuke kwamba Lenovo ni wa pili kwa kuuza PC ulimwenguni kwa sababu Lenovo wanashikilia 90% ya soko la China, labda nikukumbushe kuwa Quarter ya mwisho ya 2013 Huawei ni watatu kwa kuuza Smartphone Duniani. Nao kama Lenovo wanategemea soko la nyumbani (China).

China ni soko lenye watu Bilioni 1.2, ni kubwa kuliko soko zima la Afrika lenye nchi 53 au Europe lenye nchi 52. Ukitaka kupata picha halisi Lenovo walikuwa wa 5 kwa mauzo ya PC mwaka 2002 wakati huo hawaku-export hata PC moja (yaani 100% China sales). Mwaka 2005 Lenovo ndio wameanza campaign ya kujaribu kuwa Global Brand baada ya kununua IBM.

Sasa hivi Lenovo wamejiweka vizuri kimauzo katika nchi zote za Asia Pacific kasoro Japan bado imewashinda ku-penatrate. North America na Europe bado ni wachanga mno. Ninakupa mfano Lenovo IdeaCentre (ambayo ni convertible PC 27" screen yenye betri [arguably the biggest tablet in the world]) mapaka leo bado haijaingia kwenye European Market, so this is not their play ground. However I fully understand and appriciate the quality of their devices.

Hivyo basi nilichofananisha kuhusu kampuni mbili hizi ni kwamba zote ni China based. Vile vile usiidharau Huawei kwa sababu Lenovo total revenue 2012 ni $29,574,000,000 na Huawei ni [FONT=Arial, Helvetica, sans-serif] $[/FONT]35,419,285,361.54 (Kwa mujibu wa 2012 financial report zao). Hivyo basi Lenovo ni mtoto mdogo kwa Hauwei kwa mtazamo wa mapato.
 
Mkuu si kweli. Kwenye soko la marekani lenovo ni wa 4 kwa computer zote na ni wa tatu kwa computer za windows. Na pia ndio kampuni pekee ambayo ina positive growth. Angalia dell, hp, apple na acer wote wana negative growth mauzo yameshuka lenovo peke yake mauzo ndo yamepanda.

gartner_3Q12_us.png

hizi ni data za marekani na source ni hii kwa 3q 2012
apple-hits-new-high-with-13-6-share-of-u-s-pc-shipments-in-3q-2012

quarter ya 4 mambo yakaja yale yale lenovo ndio pc pekee yanye positive result nafasi ya 3 dell na hp wanaendelea kuanguka
gartner_4Q12_us.png

haya computer inayoshika nafasi ya tatu marekani ni mchanga??? Amempita hadi acer na toshiba ni mchanga tu huyu bado.

Na mkuu huwezi fananisha product za za lenovo na huawei. Lenovo vitu vyao vina quality ya hali ya juu si sawa na cheap plastic za huawei. Huawei wanaekewa vikwazo kibao soko la ulaya na marekani kwa quality ndogo.

Nafkiri mwaka huu 2013 lenovo atachukua position ya 1 hadi marekani ndo utaamini
 
@chief-mkwawa mimi huwa ni mwenye kupenda sana data, ahsante kwa data hizi lakini ziko poorly constructed, yaani HP wameuza 4,142? (table hii tunadhani imekusudia in milions, ingawa haisemi hivyo), hebu tupe source kabla hatujaendelea na mjadala huu.

Angalia maajabu ya table uliyotuletea, figure za Others zinaonyesha (4Q12 ni 4,494 na 4Q11 ni 5,638) halafu growth ni -2.0 huyu aliyetengeza table hii hata hesabu hajui.
 
Back
Top Bottom