HRW: Polisi na wanajeshi walitenda unyanyasaji wa kingono wakati wa uchaguzi Kenya

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,252
Wanaharakati wa haki za binadamu wanasema kuwa vikosi vya usalama nchini Kenya vilitekeleza vitendo vya ukatili wa kingono wakati na baada ya uchaguzi wa urais wa mwezi Agosti.

Shirika la haki za binadamu la Human Rights Watch linasema kuwa liliwahoji wanawake 68 na waathiriwa watatu wa ubakaji watatu katika mji mkuu Nairobi, na katika maeneo kadhaa magharibi mwa Kenya .

Wengi miongoni mwa wanawake na wasichana waliohojiwa walisema kuwa walibakwa na wanaume kadhaa, na wengi wao walikuwa ni polisi ama wanajeshi .

Mwandishi wetu Nasteha Mohamed alizungumza na waathiriwa wawili wanaoelezea masaibu yao.

Chanzo: BBC Swahili
 
Polisi tunawajua hawa, ni majangili ya serekali, lakini wanajeshi hapo siamini, mwanzo ni nani aliona wanajeshi wakidhibiti maandamano mwaka huu au hata 2007?
 
Back
Top Bottom