How to get money from your youtube channel.

How to get money from your youtube channel.

Mhafidhina07

JF-Expert Member
Joined
Aug 1, 2014
Posts
3,679
Reaction score
5,165
Habari zenu wakubwa kwa wadogo!!juzi kati niliomba ufafanuzi wa hili jambo katika jukwaa halisi ya hii mada lakin sikupata ufumbuzi leo naona bora nililete huku munisaidie kuhusu hili jambo la kupata pesa kupitia youtube channel.je vitu gan vinahitajika kupata hizo pesa?je kuna mashart?n.k naomba munisaidie wakubwa.
 
We unakuwa unaweka tu video zako nzuri na unawatangazia watu waende kuziona unapokuwa na watazamaji wengi google wanakuona na wanakurudishia kamusheni ambayo ni pesa......ila ngoja waje wajuzi zaidi!!
 
unata
Habari zenu wakubwa kwa wadogo!!juzi kati niliomba ufafanuzi wa hili jambo katika jukwaa halisi ya hii mada lakin sikupata ufumbuzi leo naona bora nililete huku munisaidie kuhusu hili jambo la kupata pesa kupitia youtube channel.je vitu gan vinahitajika kupata hizo pesa?je kuna mashart?n.k naomba munisaidie wakubwa.
unatakiwa uwe na gmail account ambayo una ADSENSE ACCOUNT.. kwenye hiyo account ya gmail ndio una upload video zako mwenyewe(hairuhusiwi ku-copy video za wengine), pesa ndio zinaingia kwenye adsense account yako ya youtube. huwezi kupewa pesa kama hauna adsense account ...JARIBU KU-GOOGLE UPATE UFAHAMU MKUBWA ZAIDI
 
hzo pesa wanatumia kupitia account gani??

Mkuu kwnz unatakiw kuw na google account ambyo itakuwezesha ku-upload videos lakini pia wakat umeingia youtube ukiwa unasign in kwny hyo account yako kuna sehem unatakiw kuweka credit number/ payment number ambyo ni visa na master card kwa Tanzania..........

Kwaiy unatakiw ume na master card au visa ambyo ndo utaweka namba zake kwny payment number........

Hvyo bas ukiwa unapost videos youtube kuptia gmail yako ambyo umesign in. Kwaiy kadri watu wanavyoangalia video yako ndvyo unapopata faida na kuwekew fedha kwny master account yako........

[HASHTAG]#StepByStep[/HASHTAG]
 
hzo pesa wanatumia kupitia account gani??
Hili swali halina jibu la moja kwa moja kwani hata ukifanya utafiti unakutana na majibu mengi tofauti.

Ila la muhimu zaidi kuhakikisha unakuwa na akaunti ya google ya ADSENSE....ukijiwekea tu video zako you tube bila hiyo akaunti hupati chochote.

Pia kuna masharti na vigezo vya kuzingatia, kama vile kuhakikisha Video unazoweka hujakopi kwingine, au la uwe na mkataba na mwenye haki miliki ya video hiyo, kama umetumia muziki sio wako lazima uambatishe ruhusa/haki kutoka kwa mmiliki halisi, Video zisiwe zenye ukosefu wa maadili mfano Picha za uchi, matusi, unampiga Paka au Mbwa, Mtoto anateswa n.k. hata kama utapata mamilioni ya views kwa video za aina hiyo haupati kitu...na kubwa na muhimu Video ziwe na Watazamaji wengi.

Pia kuna njia ya Matangazo...ambapo Tangazo linapotokea kwenye Video yako na mtazamaji aka 'gonga' basi una asilimia zako hapo.

Huu mfumo unafanya kazi vizuri na manufaa iwapo utakuwa wewe ndio muandaaji/mmiliki wa video hizo...kwa mfano kama wewe ni mpishi na ukaanzisha channel yako ya mapishi na Watu wakaipenda basi una nafasi nzuri ya kunufaika kuliko kutegemea Video za kuokoteza na kuziweka.
 
dah ahsante umedadavulia fresh.subir nikupe like.
 
Back
Top Bottom